Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres awasilisha mapendekezo ya kurahisisha majukumu kama sehemu ya ajenda kubwa ya mageuzi UN.

Wafanyakazi wanaendesha mashine ya kukusanya vitu ya Sheridan yenye kishona waya katika Kitengo cha Utoaji wa Vitu cha Huduma ya Uchapishaji UN mnamo Juni 1969.
UN Photo/Yutaka Nagata Maelfu ya kurasa za nyaraka zilikuwa zikichapishwa kila siku katika Umoja wa Mataifa kama inavyoonekana kwenye picha ya Juni 1969.

Guterres awasilisha mapendekezo ya kurahisisha majukumu kama sehemu ya ajenda kubwa ya mageuzi UN.

Masuala ya UM

Mamilioni ya maisha ya watu yameboreshwa kutokana na majukumu yaliyopatiwa Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, kazi moja kufanywa na watu wengi, kusambaratika kwa majukumu, na kazi za zamani kupitwa na wakati vinazingatia rasilimali na kudhoofishwa uwezo wa shirika kutoa huduma kwa wale wanaohitaji zaidi.

Katika mwendelezo wa Marekebisho ya Umoja wa Mataifa wakati  ukitimiza miaka 80, au UN80, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres siku ya Ijumaa Agosti 1, amewasilisha kwa nchi wanachama mikakati ili kufanya UN iwe na ufanisi zaidi, yenye muungano thabiti na yenye matokeo yaliyo dhahiri.

Majukumu — ambayo ni maombi au maagizo ya hatua za kuchukua yanayotolewa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, na Baraza la Uchumi na Kijamii — yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu 1945 Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa.

Leo hii, kuna zaidi ya majukumu hai 40,000, yanayofuatiliwa na takribani vyombo 400 vya kijamii na kimataifa. Pamoja, yanahitaji zaidi ya mikutano 27,000 kwa mwaka na kuzalisha takriban kurasa 2,300 za nyaraka kila siku, kwa gharama ya kila mwaka ya takriban dola milioni 360.

Changamoto inayoongezeka

Majukumu yanaelekeza kazi za UN katika zaidi ya nchi na maeneo 190, kuanzia utulivu, hatua za kibinadamu hadi maendeleo. Lakini mengi yamepitwa na wakati au yanajirudiarudia, na utata wake unazidi kuongezeka.

Tangu 2020, hesabu ya wastani ya maneno kwenye maazimio ya Baraza Kuu imeongezeka kwa asilimia 55, wakati azimio za Baraza la Usalama sasa ni mara tatu ya urefu wake uliokuwa miaka 30 iliyopita.

“Tutambue ukweli,” amesema Katibu Mkuu António Guterres alipokuwa akiwasilisha taarifa kwa Baraza Kuu, “hatuwezi kutegemea matokeo makubwa zaidi bila njia za kutekeleza. Kwa kugawa uwezo wetu kwa udogo mkubwa, tunakumbwa na hatari ya kuzingatia taratibu zaidi kuliko matokeo.”

Kutokuwepo kwa uratibu kweli kunachangia umahiri huo. Taasisi kadhaa za UN hutumia majukumu yale yale kuhalalisha mipango na bajeti tofauti, na kusababisha kurudiwa na kupungua kwa matokeo. Zaidi ya asilimia 85 ya majukumu hayana kifungu cha mapitio au kuondolewa. “Mapitio yenye ufanisi ni nadra, si tatizo la kawaida,” amesema Bw. Guterres. “Majukumu hayo yale hujadiliwa mwaka baada ya mwaka – mara nyingi na mabadiliko madogo tu kwenye maandishi yaliyopo.”

Safu za masanduku ya kura yaliyoandikwa 'CANADA' yamepangwa katika ukumbi katika viwanja vya maonyesho vya Windhoek kwa ajili ya kuhesabiwa wakati wa uchaguzi wa Namibia.
UN Photo/Milton Grant

UN imefanya utekelezaji wa majukumu duniani kote ikiwemo uthibitisho wa uchaguzi nchini Namibia mwaka 1989.

Jitihada za UN80: mtazamo wa mfumo mzima

Ripoti ya Mapitio ya Utelekezaji wa Majukumu, iliyotolewa tarehe 31 Julai, ni sehemu ya jitihada pana za Katibu Mkuu na ni mradi wa miaka mingi wa kuboresha namna UN inavyofanya kazi. Badala ya kuchambua majukumu kwa kila moja, ripoti hii inafuata mtazamo wa “mzunguko wa maisha”, ikichunguza jinsi majukumu yanavyoundwa, kutekelezwa na kupitiwa, na kupendekeza njia za kuboresha kila hatua.

“Niweze kuwa wazi kabisa: majukumu ni shughuli ya nchi wanachama,”. Guterres ameliambia Baraza Kuu. “Ni mwonekano wa matakwa yenu. Ndiyo mali na jukumu la pekee la nchi wanachama. Jukumu muhimu la kuyaunda, kuyaangalia au kuyapanga kuondolewa liko kwenu – na kwenu pekee. Wajibu wetu ni kuyatekeleza – kikamilifu, kwa uaminifu, na kwa ufanisi.”

“Ripoti hii inaenzi mgawanyo huo,” ameongeza. “Inachunguza jinsi tunavyoyatekeleza majukumu mnayotupa.”

Kutoka kuundwa hadi utekelezaji

Ili kukabiliana na kurudiwa na utata, ripoti inapendekeza kuwepo kwa masjala ya kidijitali ya majukumu ili kurahisisha kufuatilia yaliyopitishwa katika vyombo mbalimbali. Pia inahamasisha maazimio mafupi, wazi na yenye mahitaji ya rasilimali halisi. “Hatuwezi kutegemea matokeo makubwa zaidi bila njia za kutekeleza,” amesema Guterres.

Ripoti pia inaonesha mzigo unaoongezeka wa shughuli ya mikutano na ripoti. Mwaka jana, mfumo wa UN ulisaidia mikutano 27,000 na kuzalisha ripoti 1,100 – tatu kati ya tano kwa mada zinazojirudia. “Mikutano na ripoti ni muhimu,” amesema Katibu Mkuu. “Lakini tunapaswa kujiuliza: Je, tunatumia rasilimali zetu chache kwa njia yenye ufanisi zaidi?”

Walinda amani wawili UNMISS wa Bangladesh waliovalia kofia za bluu wakipeana mikono na mwanamume wa eneo hilo mbele ya kundi la watoto huko Tonj, Sudan Kusini.
© UNMISS

Ufadhili na matokeo

Mapendekezo ni pamoja na kupunguza idadi ya ripoti na mikutano, kurahisisha muundo na kufuatilia matumizi ya ripoti ili kuhakikisha umuhimu wake. Katibu Mkuu pia anataka uratibu thabiti zaidi kati ya vyombo vya UN ili kuepuka kurudiwa na kuhakikisha kila jukumu linaelekezwa kwenye matokeo yanayoonekana.

Ripoti inaonya kuwa ufadhili uliogawanyika unachangia utekelezaji uliogawanyika. Mwaka 2023, asilimia 80 ya fedha za Umoja wa Mataifa zilikuja kupitia michango ya hiari, asilimia 85 ya hiyo ikiwa imeelekezwa kwenye malengo maalum. “Ufadhili uliogawanyika, unaunganishwa na utekelezaji uliogawanyika, unaonyesha athari zilizo mgawanyiko,” amesema Guterres. “Kila mmoja wetu ana jukumu la kushiriki kupambana na hili. Na kila mmoja wetu lazima atumie nguvu zilizo ndani yetu.”

Kupatia vipaumbele binadamu

Kwa Katibu Mkuu, mageuzi haya si tu kuhusu taratibu lakini kuhusu athari. “Majukumu si mwisho wao wenyewe,” amesema. “Ni zana – za kutoa matokeo halisi, katika maisha halisi, katika dunia halisi.”

Amewashukuru wafanyakazi wa UN ambao amesema ni nyenzo kuu za juhudi hii. “Hakuna kazi yoyote ya utekelezaji wa majukumu ambayo ingewezekana bila wafanyakazi wetu – wanawake na wanaume wa Umoja wa Mataifa,” amesema Guterres. “Utaalam wao, kujitolea na ujasiri wao ni muhimu katika juhudi hii. Ikiwa tunataka kuboresha jinsi tunavyotekeleza majukumu, lazima pia tuwasupport na kuwawezesha watu wanaotenda hayo.”

Chumba cha Baraza la Usalama na nyundo ya Rais na bamba la jina mbele.
UN Photo/Rick Bajornas

Wito kwa nchi wanachama

Katika maneno yake ya hitimisho, Katibu Mkuu amesisitiza kwamba hatua zinazofuata lazima zitoke kwa Nchi Wanachama. “Mwelekeo wa mbele ni ninyi kuamua,” amesema. “Jukumu langu ni kuhakikisha kwamba Kitengo cha Katibu Mkuu kinatoa uwezo na michango inayohitajika kwa kitendo chochote mnachochagua.”

Ripoti inaalika nchi wanachama kushughulikia pendekezo la mchakato wa kimataifa wa muda maalum ili kuenzi mapendekezo haya na kuhakikisha juhudi hii ina fanikiwa pale ambapo nyingine zimekosa. Matokeo, kwa mujibu wa ripoti inasema, yatakuwa UN yenye ufanisi, muunganisho thabiti na yenye athari wazi, bora katika kutekeleza mipango na huduma.