Viongozi wa Afrika watambue wao ni watumishi wa wananchi - Odede
Viongozi wa Afrika watambue wao ni watumishi wa wananchi - Odede
Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.
“Kwanza nimefurahi sana kwa tuzo ambayo ni ya Mandela. Ningependa kusema ya kwamba mimi kama mwafrika na sio Mkenya tu, tunaishi wakati ambao bara letu la Afrika limegubikwa na vita, chuki, na njaa. Mfano Sudan, Ethiopia. Vita kila mahali. Na ndio wakati nakumbuka ile amani aliyoitetea Nelson Mandela.”
Amesema ni wakati wa kukumbuka kwamba ni lazima tukae pamoja kama waafrika, na sisi wenyewe tutasaidia bara la Afrika.
Amegusia pia suala la kusameheana, “tuanze kuwa kama ndugu. Madiba alitetea mambo ya amani.
Akagusia pia uongozi akisema, “na pia tuwe viongozi ambao wanajali. Tusiwe peke yake. Uongozi sio ukubwa. Uongozi ni utumishi. Viongozi wa bara la Afrika wanadhani wao ni malkia au wafalme. Hapana! Madiba alisema ya kwamba ukiwa kiongozi ni kufanyia watu kazi.”
Amesisitiza kuwa “wananchi ndio viongozi sio wewe, wewe ni mfanyakazi.”
Soma hapa mahojiano kamili ya Zipporah na Odede.