Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko Texas: Umoja wa Mataifa waonesha mshikamano

Mafuriko ya Mto Guadalupe karibu na Kerrville, Texas yamesababisha makumi ya vifo.
© Wikipedia Mafuriko ya Mto Guadalupe karibu na Kerrville, Texas yamesababisha makumi ya vifo.

Mafuriko Texas: Umoja wa Mataifa waonesha mshikamano

Tabianchi na mazingira

Umoja wa Mataifa umeonesha mshikamano mkubwa na watu wa Jimbo la Texas, Marekani serikali kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea Ijumaa na kusababisha vifo hasa vya watoto na uharibifu mwingine mkubwa. 

Katika taarifa iliyotolewa na Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Julai 7 ametua salamu za rambirambi kwa watu wote walioathirika na janga hilo.

Taarifa inaeleza “Katibu Mkuu amesikitishwa sana na vifo hasa vya watoto katika mafuriko hayo yaliyotokea wakati ambao ulipaswa kuwa wa sherehe maadhimisho ya uhuru wa Marekani ambapo familia nyingi zilikuwa zimekusanyika pamoja na kwingine watoto wakiwa katika kambi ya majira ya joto ambayo ni kawaida watoto kukusanyika ili kushiriki shughuli mbalimbali za burudani na mafunzo wakati wa likizo za shule.

Mafuriko hayo yalitokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa mfululizo, na kuzidi uwezo wa mito na mifumo ya maji taka katika maeneo ya kati na kusini mashariki mwa Texas.

Maafisa wa mitaa wamethibitisha vifo vya watu zaidi ya 80 na uharibifu mkubwa wa mali. Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makazi yao huku juhudi za uokoaji zikiendelea katika mazingira magumu.

Texas, ambayo imekumbwa na majanga kadhaa yanayohusiana na hali ya hewa katika miaka ya hivi karibuni, ni miongoni mwa maeneo mengi duniani yanayokabiliana na athari.