Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili kitukuzwe shairi: Jescah Muyia UNV

Mwanamke aliyevaa hijab na msichana mdogo wakijipiga picha ya selfie pamoja kwenye meza ya mikutano iliyoandikwa kwa ishara ya #KiswahiliDay.
UN /Manuel Elias Miongoni mwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani kwenye makao makuu ya UN, New York, Marekani. Mwaka 2021 UNESCO ilitangaza Julai 7 kuwa siku ya Kiswahili duniani

Kiswahili kitukuzwe shairi: Jescah Muyia UNV

Utamaduni na Elimu

Leo Julai 7 dunia inaadhimisha siku ya Kiswahili duniani ikibeba maudhui “Kiswahili: zama zilizopita, sasa na zijazo” kwa lengo la kutathimini ukuaji na mabadiliko katika lugha hiyo adhimu. Huko Nairobi Kenya kwenye mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNV mmoja wa wafanyakazi wa mpango huo mghani wa mashairi Jescah Muyia ameamua kuienzi lugha hiyo kwa shairi murua.

Shairi

Leo twajivunia Kiswahili duniani. Lugha yetu ya Kiafrika. Lugha tunayoienzi lugha ya kimataifa.

Utambulisho wetu Leo tunaadhimisha.

Kiswahili duniani. Kiswahili kimekuwepo ila kilipunguzwa. Sasa cha kujitambulisha na kusimama kidete. Ni utamaduni wetu kielelezo cha historia.

Leo tunaadhimisha Kiswahili duniani. Hakika tunatambua hakika twajivunia Waswahili twa ringa kutambuliwa duniani sasa itajulikana kote ulimwenguni.

Leo tunaadhimisha Kiswahili duniani. Hongera kwa mashirika yatumiayo Kiswahili. Hongera kwa vyuo vya Kiswahili. Hongera kwa nchi zitumiazo Kiswahili.

Leo tunaadhimisha Kiswahili duniani. Unasubiri nini kujifunza Kiswahili? Unasubiri nini? Kutumia Kiswahili.

Usibaki nyuma. Safari imeshaanza. Leo tunaadhimisha Kiswahili duniani.