Dola 1 kwa elimu ya msichana ni sawa na dola 3 kwa uchumi wa dunia hivi ndivyo maendeleo yanavyofanya kazi: UN

Wasichana wanapiga dole gumba katika shule moja nchini Ghana.
Dola 1 kwa elimu ya msichana ni sawa na dola 3 kwa uchumi wa dunia hivi ndivyo maendeleo yanavyofanya kazi: UN
Malengo ya Maendeleo Endelevu
Kuwasaidia wale walio na mahitaji zaidi si sadaka ni uwekezaji wa pamoja katika mustakabali bora. Hata hivyo, ufadhili wa maendeleo duniani uko katika shinikizo kubwa.
Mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa huko Sevilla, Hispania, unalenga kubadilisha hali hiyo kwa kuhamasisha uwekezaji mkubwa kwa ajili ya dunia yenye haki na endelevu.
Kila dola moja inayowekezwa katika elimu ya wasichana hutoa wastani wa faida ya dola dola 2.80 ambayo hutafsiriwa kama mabilioni katika pato la taifa duniani. Vivyo hivyo, kila dola inayotumika katika maji na usafi wa mazingira huokoa dola 4.30 katika gharama za afya.
Ni hesabu rahisi na si miujiza
Haya si miujiza ni matokeo yanayopimika. Hisabati haitambui jinsia wala miundombinu, inaonesha tu ukweli uliopo katika namba. Na namba hizo zina hoja yenye nguvu kusaidia nchi zenye rasilimali chache kunawanufaisha wote hata wale walio na mengi.
Hata dola moja, ikitumika kwa mikakati bora, inaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Kwa mfano, kutenga tu dola 1 kwa kila mtu kila mwaka ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kunaweza kuzuia vifo karibu milioni saba kufikia mwaka 2030. Vivyo hivyo, kila dola inayowekezwa katika kupunguza hatari ya majanga inaweza kuokoa hadi dola 15 za gharama za uokoaji.
Kwa mfano, kutenga tu dola 1 kwa kila mtu kila mwaka ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kunaweza kuzuia vifo karibu milioni saba kufikia mwaka 2030. Vivyo hivyo, kila dola inayowekezwa katika kupunguza hatari ya majanga inaweza kuokoa hadi dola 15 za gharama za uokoaji.
Haki na si sadaka
Pamoja na ushahidi huu mzito, msaada wa maendeleo mara nyingi hueleweka vibaya kwa baadhi huonekana kama sadaka, kwa wengine kama njia ya kujinufaisha.
Ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, kuhusu wanawake wajasiriamali wa Afghanistan inawapa changamoto wasioamini.
Inaonesha kuwa wanawake hawa hawatafuti msaada wa huruma wanataka tu nafasi ya haki kufanikiwa. Kipato chao kinawapa uhuru, ambao nao huimarisha jamii wanazoishi.
Inaonesha kuwa wanawake hawa hawatafuti msaada wa huruma wanataka tu nafasi ya haki kufanikiwa. Kipato chao kinawapa uhuru, ambao nao huimarisha jamii wanazoishi.

Sharifa mwenye umri wa miaka 15 anamsaidia mdogo wake Madi kusoma
Kupanuwa wig wa upatikanaji wa fedha kutoka sekta ya umma na binafsi, kutoa dhamana za mikopo, masharti nafuu katika masoko ya kimataifa, na kuimarisha mitandao ya usaidizi kunaweza kuchochea ukuaji wa biashara na mustakabali bora iwe Afghanistan, Ecuador au kwingineko.
FFD4 yakumbwa na changamoto
Mifano hii kutoka elimu na afya hadi ujasiriamali na mnepo dhidi ya majanga inaeleza kwa uwazi kwa kutumia takwimu uwekezaji wenye busara katika maendeleo hulipa faida kwa kila mtu.
Ujumbe huu unapaswa kuwa kitovu cha Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ufadhili wa Maendeleo FFD4 utakaofanyika Sevilla, Hispania, kuanzia 30 Juni hadi 3 Julai. Hata hivyo, mkutano huu unakabiliwa na changamoto kubwa.
Huku nchi zikiendelea kujadiliana katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, wiki moja iliyopita walikubaliana kuhusu waraka wa matokeo wa kina unaotarajiwa kupitishwa mwishoni mwa mkutano huo na kuongoza mustakabali wa misaada ya maendeleo duniani wakati baadhi ya mataifa yanajiondoa hasa, Marekani imetangaza kuwa haitatuma ujumbe wake Sevilla.
Ingawa zipo nchi chache kama Hispania ambayo imeongeza bajeti ya ufadhili wa maendeleo kwa asilimia 12, hali isiyotabirika imemfanya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kusikitika kwamba “ushirikiano wa kimataifa unapigiwa shaka.”
Mashaka haya yanaonekana pia katika nakisi ya dola trilioni 4 kwa mwaka katika ufadhili wa maendeleo, pamoja na kuvunjwa kwa ahadi za awali na utoaji wa misaada kwa kasi na kiwango ambacho Katibu Mkuu amesema ni “cha kihistoria.”
Zaidi ya hayo, Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs, yaliyotiwa saini na viongozi wote wa dunia miaka 10 iliyopita, yako mbali na kufikiwa.

Watoto kutoka mji wa Xochimilco wakiwa wamebeba mabango ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs
Nini kiko hatarini Sevilla?
Mafanikio huko Sevilla “yatahitaji nchi nyingine kujaza pengo la uongozi wa dunia na kuonesha ahadi ya kweli ya ushirikiano wa kimataifa jambo la muhimu kwa ajili ya kuendelea kuishi kwetu,” amesema Profesa Jayati Ghosh wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Massachusetts, Amherst.
Hatua za maana lazima zijumuishe mabadiliko ya kina ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Hali ilivyo sasa, mfumo huu haukidhi mahitaji ya nchi zinazoendelea huku ukilinda kwa nguvu masilahi ya mataifa tajiri.
Fikiria hili, nchi zinazoendelea hukabiliana na viwango vya riba mara mbili au zaidi ya vile vinavyolipwa na nchi zilizoendelea. Leo, viwango vya riba vinavyotozwa na wakopeshaji binafsi kwa nchi hizi vimefikia kiwango cha juu zaidi kwa miaka 15.
Msaada unatolewa, madeni yanachukua
Mwaka 2023, nchi zinazoendelea zililipa jumla ya dola trilioni 1.4 kwa huduma ya madeni ya nje kiwango cha juu zaidi katika miaka 20.
Mwaka 2023, nchi zinazoendelea zililipa jumla ya dola trilioni 1.4 kwa huduma ya madeni ya nje kiwango cha juu zaidi katika miaka 20.
Mwaka 2024, ilisemakana kuwa zaidi ya watu bilioni 1.1 wanaishi katika nchi zinazoendelea ambapo malipo ya madeni ya nje ni zaidi ya asilimia 20 ya mapato ya serikali, na karibu bilioni 2.2 wanaishi katika nchi ambako deni ni zaidi ya asilimia 10 ya mapato hayo.
Malipo ya riba kwenye madeni hayo yanazuia maendeleo kwa kukwamisha uwekezaji katika miundombinu ya afya na huduma za elimu, kwa mfano.
Kwa hiyo, marekebisho ya madeni ni ya lazima kwa sababu matumaini mengi ya maendeleo yanapotea kati ya utoaji wa misaada na mzigo wa madeni.

Wanawake wakifanyakazi katika sekta ya ushnaji Afghanistan
Kuongeza uwekezaji kwa kile kinachofanya kazi
Kutokomeza njaa, kuendeleza usawa wa kijinsia, kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuokoa bahari si fikra za msimamo mkali.
Kutokomeza njaa, kuendeleza usawa wa kijinsia, kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuokoa bahari si fikra za msimamo mkali.
Licha ya madai kutoka kwa baadhi ya mitazamo yenye msimamo mkali kwamba SDGs ni ajenda ya msimamo mkali, kwa kweli ni msingi wa pamoja orodha ya vipaumbele vya dharura vinavyohitajika na ubinadamu, ambavyo viongozi wa nchi 193 walikubaliana mwaka 2015.
Licha ya kelele za wanaopinga msaada wa maendeleo na ushirikiano wa kimataifa, wao ni wachache, anasema Katibu wa Jimbo la Ushirikiano wa Kimataifa wa Hispania.
Ana Granados Galindo anaiona Sevilla kama “taa ya mshikamano wa kimataifa.”
Wakati dunia ikijiandaa kwa FFD4, hesabu, takwimu, na wanawake wa Afghanistan wanaendelea kufanya ‘miujiza ya maendeleo kwa kutumia akili ya kawaida.”