Ni vizuri wanawake wengi washiriki uchaguzi ili wakae kwenye meza za uamuzi – Christina Ruhinda

Christina Kamili Ruhinda (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, akizungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani, Machi 2025.
Ni vizuri wanawake wengi washiriki uchaguzi ili wakae kwenye meza za uamuzi – Christina Ruhinda
Na Anold Kayanda - New York, Marekani
Malengo ya Maendeleo Endelevu Wanawake nchini Tanzania, kama ilivyo katika maeneo mengi ulimwenguni wanakumbana na changamoto mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali za kijamii zinazopata nguvu zaidi kutokana na wanawake kutokuwa na uelewa wa namna ya kuzidai haki zao.
Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.