Ufadhili kwa ajili ya maendeleo ni nini?

Watoto huko N'Djamena nchini Chad wakicheza kama sehemu ya kujifunza
Ufadhili kwa ajili ya maendeleo ni nini?
Malengo ya Maendeleo Endelevu
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, dunia inahitaji dola trilioni 4 za ziada kila mwaka ili kushughulikia changamoto kubwa zaidi duniani ambazo ni kumaliza umasikini na njaa, kupambana na mabadiliko ya tabianchi, na kupunguza pengo la usawa.
Haya ni sehemu ya malengo 17 yaliyokubaliwa na karibu kila nchi duniani, yanayojulikana kama Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2030.
Lakini tuko nyuma kwa kasi. Sababu kubwa? Hakuna ufadhili wa kutosha na wa uhakika kufanikisha maendeleo ya kweli.
Ndiyo maana viongozi wa dunia, wachumi, na watunga sera wanakutana mwishoni mwa mwezi huu huko Seville, Hispania, katika mkutano mkubwa uitwao Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu Ufadhili kwa ajili ya Maendeleo FFD4. Mkutano huo unatajwa kuwa “nafasi ya kipekee ya mara moja kwa muongo mmoja ya kufikiria upya jinsi dunia inavyofadhili maendeleo endelevu”.

Ufadhili kwa ajili ya maendeleo ni nini hasa?
Kiini cha dhana hii ni kuuliza swali rahisi dunia inagharamiaje mfumo wa haki zaidi na wa usawa wa misaada, biashara na maendeleo?

Wafanyabiashara nchini Madagascar moja ya nchi zenye maendeleo duni Afrika wakisafirisha mkaa kwenda sokoni
Jibu kutoka kwa jamii ya kimataifa limekuwa ni kuanzisha mfumo unaohamasisha mfumo mzima wa kifedha wa kimataifa, kodi, ruzuku, biashara, sera za kifedha na za fedha kuunga mkono ajenda ya maendeleo.
Mfumo huu unalenga kuwa jumuishi iwezekanavyo, kwa kushirikisha vyanzo mbalimbali vya ufadhili na kuwezesha nchi kujitegemea zaidi, ili wananchi wake waishi maisha yenye afya, tija, ustawi na amani.
Kwa kifupi, ufadhili kwa ajili ya maendeleo ni kuhusu “kubadilisha jinsi mfumo unavyofanya kazi ili kuziwezesha nchi zinazoendelea kuwekeza katika mustakabali wao,” amesema Shari Spiegel, Mkurugenzi wa Ufadhili kwa Maendeleo Endelevu katika Idara ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ya UN (DESA).
Miongoni mwa vyanzo hivi vya fedha ni benki za maendeleo za kimataifa ambazo hutoa msaada wa kifedha na wa kiufundi kwa nchi zinazoendelea. Sera mpya za kibiashara na za ushuru kimataifa na kitaifa pia husaidia kuchochea uchumi wa nchi hizi.
Pia, msaada rasmi wa maendeleo (ODA) hutumika kama njia ya misaada kutoka kwa nchi zilizoendelea kwenda moja kwa moja kwa nchi zinazoendelea.
Pia, msaada rasmi wa maendeleo (ODA) hutumika kama njia ya misaada kutoka kwa nchi zilizoendelea kwenda moja kwa moja kwa nchi zinazoendelea.
Kwa nini ufadhili kwa ajili ya maendeleo ni muhimu?
Kuanzia ongezeko la madeni hadi kupungua kwa uwekezaji na misaada, mfumo wa sasa unashindwa kuwahudumia watu unaokusudiwa kuwasaidia.
Watu kote duniani wanabeba mzigo wa hali hii:
Watu kote duniani wanabeba mzigo wa hali hii:
- Madeni yanaongezeka, uwekezaji unapungua, na misaada ya wafadhili inazidi kupungua.
- Watu milioni 600 bado wanaweza kuwa wanaishi katika umasikini uliokithiri kufikia 2030 ikiwa hatutabadilisha mwelekeo, na itachukua miongo mingi kufikia SDGs.
- Leo, watu bilioni 3.3 wanaishi katika nchi zinazotumia fedha zaidi kulipa madeni kuliko kwenye afya au elimu.
- Aidha, mabilioni ya watu wataendelea kuishi katika nchi zinazolazimika kuwekeza zaidi katika kulipa madeni kuliko maendeleo.
- Hii ina maana ya fedha chache zaidi kwa ajili ya shule, hospitali, maji safi, na ajira mambo ya msingi yanayohitajika ili kustawi.
Kwa watu wanaoathirika moja kwa moja na hali hii, muda unaopotea si wa kukubalika.
Mabadiliko ya kimuundo yanayohitajika ni yepi?
Kwa kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara na kupungua kwa misaada ya maendeleo kila mwaka, mbinu ya kawaida ya ufadhili haiwezi kuendelea.

Kazi imeanza kwenye mfumo wa usafiri wa haraka unaounganisha Delhi na Meerut huko Uttar Pradesh, India.
Mkutano ujao wa Seville ni fursa ya kubadili mkondo, kuhamasisha fedha kwa kiwango kikubwa na kurekebisha kanuni za mfumo ili kuzingatia mahitaji ya watu.
Mkutano huo utawaleta pamoja wawakilishi wa nchi, asasi za kiraia na wataalamu wa kifedha kujadili mbinu mpya za ufadhili kwa ajili ya maendeleo.
Jambo muhimu ni kwamba mkutano huu utatoa nafasi kwa nchi zinazoendelea kushiriki kikamilifu kwenye maamuzi ya kifedha ya kimataifa.
Madeni yana jukumu gani?
Katika mfumo wa sasa, nchi zinazoendelea zinaendelea kulipa kiasi kikubwa cha fedha kuhudumia madeni yao huku zikikumbwa na gharama za mikopo ambazo zinaweza kuwa mara mbili au nne zaidi ya zile za nchi zilizoendelea.
Gharama hizi huongezeka hasa wakati wa majanga au baada ya majanga, na kusababisha mzunguko wa hali ya kifedha usioisha ambapo nchi zinashindwa kuwekeza kwenye maendeleo yanayohitajika ili kulipa madeni hayo.
“Kwa kukabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za mitaji, nchi zinazoendelea hazina uwezekano wa kufadhili malengo ya maendeleo endelevu,” alisema Katibu Mkuu wa UN, António Guterres.

Nini kinatarajiwa kutokana na mkutano wa Seville?
Katibu Mkuu amesema kwamba itahitajika “mawazo makubwa na maboresho makubwa” ili kurudi kwenye mkondo wa kumaliza umasikini, njaa na ukosefu wa usawa.
“Mkutano huu ni fursa ya kipekee ya kurekebisha mfumo wa kifedha wa kimataifa ambao umepitwa na wakati, hauna ufanisi, na haupo sawa,” amesema Guterres.

Watoto wakiwa mlangoni mwa nyumba yao katika eneo masikini nchini Lebanon
Nchi wanachama zimeafikiana juu ya rasimu ya mpango utakaotoa kifurushi cha mageuzi na hatua muhimu zinazohitajika kufungwa kwa pengo la ufadhili la dola trilioni 4.
Marekani imejiondoa katika mchakato huo siku ya Jumanne wakati wa majadiliano ya mwisho kuhusu hati ya matokeo, ikisema haiwezi kuunga mkono rasimu hiyo.
Mageuzi yatatokana pia na kuhamasisha wadau wote wa binafsi na wa umma, wa sekta rasmi na isiyo rasmi, kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea na kulinganisha malengo yao ya pamoja kuelekea mustakabali endelevu.
Hii ni pamoja na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kuwa msingi wa maendeleo yote, kuongeza mapato ya kodi kwa maendeleo ya kimataifa, kupunguza gharama za mitaji kwa nchi zinazoendelea, kurekebisha madeni yaliyopo, na kutafuta mbinu mpya na bunifu za ufadhili.
“Seville ni wakati wa kihistoria. Ni mwanzo, si mwisho wa mchakato. Sasa swali ni tunatekelezaje ahadi hizi?” amesema Bi. Spiegel.
Kurekebisha mfumo wa kifedha uliovunjika ni changamoto, lakini Bi. Spiegel ana matumaini kwamba ushirikiano wa kimataifa unaweza kufanikisha hilo.