Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na ulinzi wa raia, walinda amani wa UN Ituri waendesha kampeni ya afya

Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kutoka Bangladesh wanapatia wakimbizi wa ndani kwenye kituo cha Rhoo, matibabu kutokana na ugumu wa…
MONUSCO
Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kutoka Bangladesh wanapatia wakimbizi wa ndani kwenye kituo cha Rhoo, matibabu kutokana na ugumu wa kupatikana huduma kwenye eneo hilo lenye migogoro.

Pamoja na ulinzi wa raia, walinda amani wa UN Ituri waendesha kampeni ya afya

Afya

Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wameendesha kampeni ya afya na kusaidia wakimbizi wa ndani kupata matibabu katika eneo hilo lililogubikwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi.

Kampeni hiyo ya matibabu imeanza mwezi Januari mwaka huu ambapo walinda amani hao wa  ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO nchini  DRC wanatoa huduma kama vile vipimo vya shinikizo la damu, na wagonjwa wanapatiwa dawa.

Josee Ndroy Dz’Da, mnufaika hakuficha furaha yake akisema, “nina furaha sana kwa sababu wanatusaidia dawa za kuhara, malaria, vidonda vya kila aina na wanatupatia dawa bure.”

Rais wa vijana hapa kambini Daniel Lokana anaeleza kwamba wanaosaka huduma ni wengi sana. “Tunaona mara nyingi wagonjwa wengi wanakuja hapa kituo cha MONUSCO na wanapatiwa dawa. Pia majeruhi kama hawawezi kupatiwa dawa hapa, MONUSCO huwasafirisha kwa helikopta hadi Bunia.”

Bunia ni mji mkuu wa jimbo la Ituri.

Meja Zadid Bossais, Mkuu wa kitengo cha Afya cha Kikosi cha Bangladesh hapa Rhoo anasema kwamba jukumu letu ni ulinzi wa raia chini ya Umoja wa Mataifa. Lakini raia wanakabiliwa na shida nyingi za kiafya kwani eneo hili halina vituo vya afya vya kutosha kuhudumia watu wengi. Kwa ushirikiano na mamlaka za afya hapa tumeendesha kampeni mbili za afya kila siku kwa wakimbizi wa ndani. Tangu Januari hadi mei 2025 tumetoa huduma kwa wakimbizi wa ndani 400.