Takribani wakimbizi milioni 1 wapata njia halali na salama za kuendeleza maisha yao – UNHCR
Takribani wakimbizi milioni 1 wapata njia halali na salama za kuendeleza maisha yao – UNHCR
Utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa kwa Wakimbizi, GCR unaendelea kuzaa matunda kwani ripoti mpya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, (UNHCR) na Shirika la Muungano wa Ulaya la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) inaonesha ongezeko la wakimbizi waliopata vibali vya ajira, muungano na familia na masomo badala ya kutegemea mifumo ya jadi ya hifadhi,
Ripoti iliyotolewaleo Geneva, Uswisi inasema kuwa karibu wakimbizi milioni 1 walipata njia halali za usalama na mustakabali bora kati ya 2019 na 2023.
Ikipatiwa jina ripoti inaonesha kuwa kati ya 2019 na 2023, takribani wakimbizi 255,000 walipata vibali vya kuingia mwaka 2023 pekee—ikiashiria ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka 2022.
![]() | OECD-UNHCR: Safe Pathways for Refugees SHARE A GOOD PRACTICE. Share. OECD-UNHCR: Safe Pathways for Refugees globalcompactrefugees.org |
Nchi kidedea ni pamoja na Ujerumani
Nchi kama Ujerumani, Canada, Marekani, Uingereza, na Sweden zilichukua nafasi muhimu katika juhudi hizi, zikichangia pamoja katika lengo la kimataifa la vibali milioni 2.1 kwa wakimbizi.
Vibali vya kuungana na familia vilikuwa vya kawaida zaidi, vikichukua asilimia 68 ya viza zilizotolewa, ikifuatiwa na vibali vya kazi asilimia 19, na masomo, asilimia 18.
Ripoti inasema njia hizi halali zinawapa wakimbizi fursa ya kujenga upya maisha yao, wakiepuka utegemezi wa misaada ya kibinadamu na kuelekea kwenye kujitegemea na utulivu wa muda mrefu.
“Programu hizi zinawapa wakimbizi nafasi ya kuacha kutegemea msaada na kujenga mustakabali wa utulivu kwa ajili yao wenyewe,” amesema Ruven Menikdiwela, Msaidizi wa Kamishina Mkuu wa UNHCR, upande wa ulinzi.
Amesema “kwa kuunganisha wakimbizi katika mifumo ya uhamiaji iliyo tayari, tunajiepusha na kujenga miundombinu ya ziada, ikiwapa watu fursa ya kusafiri salama na kwa ufanisi.”
Njia halali ni jawabu la mifumo ya hifadhi inayokumbwa na shinikizo
Ripoti hii inakuja katika kipindi kigumu wakati ambapo idadi ya wahamiaji inazidi kuongezeka, ikiwaweka shinikizo kubwa mifumo ya hifadhi duniani kote.
UNHCR inasisitiza mataifa kuongeza njia hizi, kurahisisha upatikanaji wa nyaraka na uthibitisho wa ujuzi, na kushirikiana na sekta binafsi na jamii ili kuhakikisha suluhu endelevu na jumuishi kwa wakimbizi.
Licha ya changamoto zinazoongezeka, ripoti inaonyesha mwelekeo chanya, na njia halali za uhamiaji zikitoa matumaini kwa mamilioni ya watu waliokimbia makazi duniani.
