Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP inazipiga jeki nchi wanachama kupambana na taka za plastiki: Clara Makenya

Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania, akizungumza kwenye jukwaa huku bendera za Tanzania na UN zikiwa nyuma.
© UNEP Tanzani Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia.

UNEP inazipiga jeki nchi wanachama kupambana na taka za plastiki: Clara Makenya

Tabianchi na mazingira

Wakati mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 umefungua pazia leo mjini Niece Ufaransa , tunakuletea sehemu ya mwisho ya mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.

Bi. Makenya amesema UNEP ina jukumu kubwa na muhimu katika kupambana na taka za plasitiki na inachukua hatua Madhubuti kwa kkushirikiana nan chi wanachama katika vita hivyo. Mathalani nchini Tanzania amesema “kama UNEP na naweza kusema kwamba tumechangia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na taka za plastiki hapa Tanzania. Hata lile ya katazo la taka za plastiki, mwaka elfu mbili na kumi na tisa lilotokea Tanzania kulikuwa na mchango mkubwa sana katika nyanja mbalimbali”

Ameongeza kuwa mbali ya kuandaa kanuni na kusaidia upande wa sheria lakini hata kutoa takwimu za kitaalamu au kutoa utaalam ambao uliwezesha kupelekea kwenye maamuzi ya mwisho kwao tulichangia na tulishirikiana na wadau wengine katika hilo.

Mvuvi aliyevaa fulana ya usalama na glavu nyekundu akivuta taka nyingi za plastiki kutoka majini katika ufuo mmoja jijini Mwanza, Tanzania.
UN News/Evarist Mapesa Taka ngumu za plastiki ikikokotwa kutoka majini ilipokuwa imetupwa na wavuvi wa ufukwe wa Mihama Jijini Mwanza Nchini Tanzania.

Kanuni na sheria za kupinga matumizi ya plastiki Tanzania

Ameendelea kusema kuwa UNEP kwa kipekee kabisa pia iliwezesha kutengeneza kanuni mbalimbali za kuwezesha katazo la sasa la matumizi ya mara moja ya plastiki kuweza kusimamiwa kwa sheria, taratibu na kanuni zilizotengenezwa na UNEP ilikuwa na mchango mkubwa sana hapa Tanzania.

Amesema mafanikio mengine yaliyopatikana katika ushiriki wa UNEP ni uelewa wa jamii, lakini pia lingine kubwa ni katika kuwezesha jamii sasa kuangalia namna mbadala au ubunifu wa kurejeleza plastiki.

Bi. Makenya amesema hapo nyuma kidogo UNEP tuliweza kufanya kazi na mashirika kama la ILO, ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani pamoja na ubalozi wa Sweden ambapo tulihamasisha vijana ambao walikuwa kwenye ujasiriamali wanaofanya kazi za urejelezaji wa taka za plastiki kwa kuhamasisha na kuwatia moyo kuendelea na hiyo kazi kwa kuleta tuzo, lakini pia tumeweze kuwaunganisha na elimu ya kuongeza ubora wa bidhaa zao ili kuweza kupata pesa zaidi nak wa wafanyabiashara wadogo na wa kati na kuweza kuona kwamba kuna fursa kwenye eneo hilo na kuweza kufanyia kazi.

Kundi la wanawake na vijana nchini Tanzania hupanga taka za plastiki ufukweni kwa ajili ya kuchakata tena kuwa vifaa vya ujenzi.
UN News/Evarist Mapesa Wanawake na vijana nchini Tanzania wakikusanya taka za plastiki ambazo zitakarabatiwa na kubadilishwa kuwa vifaa vya ujenzi kama vile Matofali.

Ushiriki wa vijana na wanawake

Kuhusu ushirikishwaji wa vijana na wanawake katika harakati za kupambana na taka za plastiki Bi. Makenya amesema “Kwa lweliI jitihada zetu kubwa zimejikita kwa vijana vijana wale vijana ambao walikuwa wanajitengenezea kipato kwa kupitia kurejeleza taka za plastiki. Tumekuwa tunawahamasisha kwanza kwa kuwatia moyo kuendelea na hiyo kazi kwa  kuleta tuzo lakini pili kuwezesha ubora wa bidhaa zao ili waweze kupata thamani ya pesa inayoendana na ubora wa bidhaa”.

Mbali ya hayo amesema lakini pia vijana wengine ambao walikuwa wanafikiria kuanza kuingia katika harakati hizo tumekuwa tunawatia moyo kwa kuona wenzao wanavyo wanavyopata msaada kwenda mbele ambapo wengi wanajiajiri ili wahamasikike zaidi kwani hilo eneo sio sawasawa na bure kabisa.

Bi. Makenya amehitimisha kwa ujumbe maalum, “Kwa nchi za Kanda ya Afrika Mashariki ni kwamba kwa pamoja tunaweza na hakutoshi kila mtu kivyake vyake, tuvunje kuta za kufanya kazi tofautitofauti kwenye taasisi zetu, lakini pia tuelimishe jamii tunaofanya nao kazi ili kuwe kuna mwendelezo wa kuona taka za plastiki zinakoma kabisa. Wadau mbalimbali kwa ujumla wake kuweza kufikiria teknolojia ambayo itapunguza gharama za kukusanya na za kubadilisha taka ziweze kuwa ni nzuri”.