Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TANLAP tunasongesha SDGs kupitia msaada wa kisheria – Christina Kamili Ruhinda

Christina Kamili Ruhinda (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, akizungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UN News

Haki za binadamu

Kuelekea mwaka 2030, kote duniani, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kitaifa, taasisi na watu binafsi wote kwa namna tofautitofauti wanatekeleza majukumu mbalimbali ili kuhakikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo endelevu, SDGs yanafanikiwa.

(TANLAP) ni mtandao wa kitaifa wa unaofanya kazi katika sekta ya sheria nchini Tanzania. Ni mtandao wa wanachama unaojumuisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), Mashirika ya Kijamii (CBOs), Mashirika ya Kidini (FBOs) na taasisi nyingine zinazotoa msaada wa kisheria nchini Tanzania.

Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP.
UN News
Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP.

Ulianzishwa mwaka 2006, lengo kuu likiwa kushirikiana na kuungana na Asasi nyingine za Kiraia ili kutoa msaada wa kisheria wa hali ya juu na kutetea upatikanaji wa haki kwa watu wasio na uwezo wa kumudu huduma za kisheria na walio  katika jamii za pembezoni nchini Tanzania.

TANLAP ilianzishwa baada ya kubainika kuwa kuna haja ya kuwa na mtandao huru na unaofanya kazi kikamilifu wa watoa msaada wa kisheria, ili kujenga uwezo wa watoa msaada wa kisheria, kuoanisha huduma za msaada wa kisheria na maadili ya watoa msaada huo, pamoja na kuwa na jukwaa la pamoja kwa ajili ya ushiriki katika sera na mabadiliko ya sheria.

Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa hii anazungumza na Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP. 

Christina Ruhinda, Mwanasheria mbobevu nchini Tanzania hivi karibuni alikuwa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kushiriki mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW 69.