Muhtasari wa Habari: Mama Dunia; DRC; Papa Francis
Muhtasari wa Habari: Mama Dunia; DRC; Papa Francis
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa’ kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka.
Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.
DRC
Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.
Katika mji wa Mbandaka, mji mkuu wa jimbo la Equateur, wanahabari Watoto waliofundishwana shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF wanatumia radio, video na uandishi wa Habari kusambaza ujumbe muhimu wa watu kuchukua hatua kulinda misitu badala ya kukata miti kiholela.
Papa Francis
Na kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kukumbuka mchango wake wa kutetea walio taabuni.
Mathalani shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekumbukawito wake wa kutaka kila mtu kukaribisha, kusindikiza na kujumuisha wale wote wanaobisha hodi kwenye milango yao.