Tumieni lugha za mama kufunza Kiswhaili wasema wadau kwenye kongamano la Kiswahili Uganda
Na Na John Kibego
Utamaduni na Elimu Kongamano la Kimataifa la Kiswahili linalofanyika mjini Kampala Uganda limewaleta pamoja wadau kutoka kila kona ya Afrika na kwingineko ili kujadili mikakati ya kukuza lugha hiyo adhimu ya Kiswahili.
Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu John Kibegoanashiriki katika kongamano hilo ili kupata maoni ya wadau mbalimbali.
Matumizi ya lugha za mama kufundisha Kiswhaili ni njia muhimu ya kuepuka hofu kuwa kusambaa kwa Kiswhaili kunaweza kuathiri au kuua lugha za mama barani Afrika, asema Prof. Aldin Kai. Mutembei.
Akiongea kwenye kongamalo la Kimataifa la Kiswhaili la mwaka 2025 mjini Kampala, Prof. Mutembei amesema, anafahamu kuwa baadhi ya watu hata katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajakumbatia lugha ya Kiswahili wakihofia kuwa lugha hiyo itasababisha au kutoweka kwa lugha zao mama.
“Lugha za mama zinaweza kutoweka lakini sio kwasababu ya kiswhaili. Unaweza kutumia lugha hizo kufundisha watu Kiswhaili na wala sio mpaka upitie Kingereza au lugha zingine,” asema.
Prof. Mutembai ambaye ni Mkurugenzi wa Tasisi ya Taaluma za Kiswahili kwneye Chuo Kikuu cha Dar-es-salam nchini Tanzania amewachagiza wapenzi wa lugha ya Kiswahli kutoka kila jamii washirikiane na wataalamu wa Kiswahili ili waandike vitabu wakitafsiri maneno ya lugha za mama kwa Kiswahili.
“Kwa njia hiyo jami haitakiona tena Kiswahili kama adui kwani kitakuwa pia kikisaidia kukuza na kulinda lugha zao. Munyoro anaadika Kinyoro, Munyankole kwa Kinyankole na Acholi akiandika lugha yake kwa mfano,” aongezea Prof. Mutembei.
Tusahau yaliyopita tugange yajayo: Dkt. Tendo
Dkt. Kisembo Ronex Tendo, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest, lilioongoza mandalizi ya kongamano hilo amewaomba viongozi wa vyombo vya usalama kuhakikisha kwamba hawatumii lugha ya kiswhaili wanapowakamata washukiwa kama njia ya kufuta kabisa historia ya chuki dhidi ya Kiswahili miongoni mwa Waganda.
“Unapokwenda kumkamata mshukiwa, kwa nini lazima utumie Kiswahili, ‘kaa chini, usikimbie’ tumieni kingereza,” amesema Dkt, Kisembo.
Katika hotuba yake, amesema, Waganda wengi walichukia lugha ya Kiswahil kutokana na unyanyasaji uliofanywa wakati wa vta vya Kagera.
“Hatuwezi kukumbatia hisoria hiyo. Ni lazima tuchukuwe mkondo mpya,” amesema Dkt. Kisembo.
Fikra za Waganda kuhusu Kiswahili zimebadilika: Mwesigye
Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Msitaafu Fred Mwesigye anasema kuna nuru sasa kwani mtazamo wa Waganda umeanza kubadilika kutokana na jeshi la wanainchi wa Uganda, (UPDF) kuwa rafiki kwa wanchi.
“Wanajeshi wa zamani walitumia vibaya Kiswahil lakini chini ya utawala wa raisi wetu sasa, wanajeshi ni rafiki wa wanchi na wanawafunza,” amesema Balozo Mwesiye.
Amewambia wadau kuwa serikali ya Uganda imepga haua kubwa na wala haitorudi nyuma katika suala la kukuza kiswahili.
“Nataka niwambie kuwa kwa sasa Kiswahili kinafuzwa kuanzia darasa la kwanza kwenda juu kwneye shule zote. Kipindi cha saa moja kimetengwa kwa ajili ya mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa baraza la mawaziri kila Jumaatatu,” ameeleza.
Tukienzi Kiswahili kitakua zaidi ya lugha ya Afrika: Pfof. Lumumba
Kwa upande wake, Prof. P.L.O Lumumba kutoka Kenya ameeleza matumaini kuwa endapo hatua zinazopigwa na nchi mbali mbali zitaendelezwa, basi Kiswahili kitasambaa haraka barani Afrika na duniani kote.
“Kiswahili kimeanza kunoga. Ni lugha rasmi Kenya, ni lugha rasmi Tanzania, Uganda na hata kinafundishwa Africa Kusini. Kazi tulionayo sisi ni kuona kwamba kiswahil hakizungumzwi tu bali pia kinaandikwa,” amesema Prof. Lumumba.
Kiswahili ni zaidi ya miundombinu ya mawasiliano: Kisesa
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Maj. Jenerali Paul Kimuli Kisesa amesema Kiswahili sio tu miundombinu ya mawasiliano bali pia ni nguzo ya utambulisho, ukuaji wa kuchumi na kijamii.
“Kma tunavyofahamu kuwa kuna watu zaidi ya milioni 500 wanaozungmuza Kswahili duniani kote, ni lazima tujitahidi kueneza lugha yetu ili tupate manufaa kamili kiuchumi na kijamii,” amesema Balozi Kisesa.
Bwana Samuel Kasero, Mwalimu wa lugha ya Kiswahili kwneye shule ya upili ya Green Field wilayani Mashindi ameelezea furaha yake kwani kongamano hilo limemuunganisha na watu kutoka nchi mbali mbali barani Africa.
“Nafurahi sana kwani nimejifunza mengi na kukutana na wau wengi,” amesema Kasero.
Bi. Ana Manyirika kutoka Dar-es-salam nchini Tanzania alijtokeza na bidhaa zake ikiwemo aina mbali mbali za korosho ili kunufaika kuchumi kutokana na kongamano hilo.
Kogamano la Kimataifa la kiswhail 2025 jijini Kmapla limewalea pamoja tagriban wanafunzi 10,000 kutoka nchini wanachama, wawakilishi wa nachi na serikali pamoja na wadau wengine wapenzi wa Lugha ya Kiswahili.
Kongamano hilo litahitimishwa tarehe 17 mwezi huu wa Aprili kwa ziara za kitalii kwenye mbuga za wanyama na chanzo cha Mto Nile mongoni mwa vivutio vingne vya watali.