Miaka 30 ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji: Vita dhidi ya ukatili wa kijinsia imebadilika vipi
Miaka 30 ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji: Vita dhidi ya ukatili wa kijinsia imebadilika vipi
Miaka 30 iliyopita, katika Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Wanawake mwaka 1995, viongozi kutoka mataifa 189 na zaidi ya wanaharakati 30,000 walikutana na kutengeneza na kupitisha mpango wenye dira ya kufanikisha haki sawa kwa wanawake na wasichana. Mpango huo ulitambuliwa kama Azimio la Beijing na Jukwaa la Hatua za Utekelezaji, na imekuwa ni nyaraka iliyoidhinishwa zaidi duniani kuhusu ajenda ya haki za wanawake.
Ikijikita katika uzoefu na matakwa ya wasichan na wanawake, Azimio la Beijing limeweka bayana maeneo 12 muhimu ya kuchukuliwa hatua ikiwemo ukatili dhidi ya wanawake
Gertrude Mongella (kushota akiwa amesimama kwenye mimbari), Katibu Mkuu wa Mkutano huo, akihutubia kikao cha tarehe 4 Septemba 1995. UN Photo/Milton Grant
Tunapokaribia kuadhimisha miaka 30 mwaka huu wa 2025, Azimio la Beijing linasalia kuwa nyaraka kuu ya harakati za haki za wanawake na usawa wa kijinsia, ambapo serikali, wanaharakati, na Umoja wa Mataifa wanatathmini maendeleo yaliyofikiwa, wanatatua changamoto na kuahidi kutenga rasilimali za kuwezesha kutekeleza ajenda hiyo.
Kwa Siku 16 za Harakati za Kupinga Ukatili wa Kijinsia fahamu jinsi Azimio la Beijing na Jukwaa la Hatua kwa utekelezaji lemebadili ajenda ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, na kwa zama za sasa kitendo hicho kinamaanisha nini.
Haki za wanawake ni haki za binadamu: Ni historia katika usawa wa jinsia
Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu mwaka 1993 uliofanyika Vienna, Uswisi, ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa haki za wanawake kutambuliwa bayana kabisa kuwa ni haki za binadamu.
“Haki za binadamu ni haki za wanawake, na haki za wanawake ni haki za binadamu,” iligeuka kuwa kilio cha cha vuguvufu kwa wanaharakati wa haki za wanawake katika Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa WAnawake huko Beijing, China. Hiyo ilikuwa ni kaulimbiu iliyotokana na hotuba iliyotolewa na Mke wa Rais wa Marekani, Hillary Rodham Clinton. Jukwaa la Hatua kwa Utekelezaji lilithibitisha suala la wanawake kutokumbwa na ghasia au ukatili.
Mkutano ulikuwa ni jukwaa kwa wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake kujipanga na kuchechemua ili kupitishwa kwa Mkataba mwingine muhimu wa kimataifa— Mkataba wa Kutokomeza Aina zote za Ukatili dhidi ya Wanawake, (CEDAW), uliopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1979, na Itifaki ya Ziada—hatua ambayo ilihitimishwa mwaka 1999 na kuwezesha watu binafsi kuripoti moja kwa moja ukatili mbele ya kamati ya CEDAW. Hii iliunda shinikizo la kisiasa kwa serikali kusaka njia za kutatua ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Suala kwamba haki za wanawake ni haki za binadamu, sio tena hoja, lakini wakati huu ambapo mwanamke 1 kati ya 3 anakumbwa na ukatili katika kipindi cha maisha yake yote, na mwanamke mmoja anauawa kwa makusudi na mpenzi wake au mwanafamilia katika kila dakika 10 ina maana kwamba hakuna nchi ambaye imetimiza ahadi ya mwanamke kuwa huru dhidi ya ukatili au ghasia yoyote ile.
Wanaharakati wakiwa kwenye maandamano huko Cox’s Bazar, nchini Bangladesh, wakiwa wamebeba mabango ya kupinga ukatili wa kingono na wa kijinsia wakati wa Siku 16 za Kupinga Ukatili dhidi ya kijinsia mwezi Novemba mwaka 2022. UN Women/Sultan Mahmud Mukut
Sheria dhidi ya ukatili wa majumbani :Zimeongezeka baada ya Beijing
Mwaka 1994, takribani nchi 12 zilikuwa na sheria dhidi ya ukatili wa majumbani.
Baada ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Hatua za Utekelezaji,, idadi hii iliongezeka kwa kasi kubwa. Leo hii, , Kanzidata ya UNWomen kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake imeorodhesha sheria 1,583 katika nchi 193,, zikiwemo 354 mahsusi kabisa dhidi ya ukatili wa majumbani.
Utafiti unadokeza kwamba kupitishwa kwa makubaliano ya kimataifa na kikanda kuhusu haki za binadamu na uhamasishaji kutoka mashirika ya utetezi wa haki za wanawake kulichochea hatua za kuanzisha na kutunga sera hizo madhubiti.
Leo hii, kuna ushahidi bayana kuwa sheria dhidi ya ukatili wa majumbani zimepunguza ukatili kutoka kwa mwandani au mpenzi. Nchi zenye sheria hizo zimeripoti kiwango cha kutokea kwa matukio hayo kuwa ni asilimia 9.5 ikilinganishwa na asilimia 16.1 kwa nchi zisizo na sheria. Hata hivyo bado changamoto ni usimamizi wa sheria zilizoko, kuna pengo la ulinzi wa kisheria na pia huduma kwa manusura.
Kubadilika kwa mila na kupanuaka kwa huduma muhimu kwa manusura
Azimio la Beijing lilikuwa ni hatua muhimu ya kutatua ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Lilitaka kupanuliwa kwa huduma muhimu ikiwemo makazi, msaada wa kisheria, huduma ya matibabu na ushauri nasaha. Kabla ya 1995, kulikuwa na mifumo 19 tu ya kitaasisi dhidi ya ukatili wa majumbani; zaidi ya asilimia 95 ya mifumo hiyo ilianzishwa baada ya Jukwaa la Utekekelezaji wa Hatua la Beijing.
Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji wa hatua vilisisitiza pia kuzuia, kwa kusihi serikali na wanaohusika na maendeleo ya kimataifa kuwekeza kwenye elimu na kampeni za uhamasishaji dhidi ya mila na fikra potofu zinazoimarisha ukatili dhidi ya wanawake.
Mwanaharakati kutoka shirika la kiraia akiwe nje ya jengo la Bunge huko Beirut, nchini Lebanon akifurahia kufutwa kwa Ibara ya 522 ya Kanuni ya Makosa ya Adhabu ya Lebanon. Hii ni taraehe 17 Agosti mwaka 2017.Baada ya Jordan na Tunisia kufuta sheria za kibaguzi kuhusu ubakaji, Bunge la Lebanon nalo lilikubali tarehe 16 Agosti kufuta Ibara ya 522 ya Kanuni ya Makosa ya Adhabu ikijulikana kama sheria ya ubakaji, au sheria ya ubakaji kwenye ndoa, ambayo ilimuepusha mbakaji dhidi ya adhabu iwapo atamuoa manusura. Picha: Hisani ya ABAAD
Kwa nini takwimu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake ni muhimu
Kisichohesabika, kinakuwa hakijulikani. Bila takwimu bora kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, sera na sheria haziwezi kutosheleza kutatua uhalisi wa kile kinachokumba wanawake na wasichana kila siku.
Kabla ya 1995, takwimu nyingi kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, zilitoka katika tafiti ndogo ndogo za hapa na pale. Azimio la mwaka 1993 kuhusu Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake lilitaka serikali kukusanya taarifa za ukatili dhidi ya wanawake, hasa ukatili wa majumbani. Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji wa hatua nalo pia lilitaka kuweko kwa mfumo mahsusi wa kuwezesha tafiti za kitaifa na za kimataifa kama vile tafiti za kimataifa za shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, kuhusu ukatili wa majumbani.
Kuanzia mwaka 1995 hadi 2014, nchi 102 zilifanya tafiti za kitaifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake.
Hii leo, kuna mipango ya kimataifa kama vile ives like UN Women’s WProgramu ya Kuhesabu Wanawake ya UN Women, na Kanzidata ya kimataifa kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake ambazo zinafuatili maendeleo na kumulika maeneo ambayo yanahitaji hatua za dharura. Tangu kuanzishwa mwaka 2016, Programu ya Kuhesabu Wanawake, imekuwa inasaidia nchi kukusanya zaidi takwimu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na pia imekuwa mstari wa mbele kuanzisha mfumo wa kupima ukatili unaochochewa na ghasia.
Hapa ni Montevideo, Uruguay maandamano mawili yakiwa sambamba yaliandaliwa na vikundi vya wanaharakati wanawake yakileta pamoja zaidi ya watu 6,000 wakipinga mauaji ya wanawake. Ni tukio la mwezi Novemba 2017: UN Women/Sahand Minae
Nguvu ya harakati za watetezi wa haki za wanawake na mashirika ya wanawake
Jukwaa la Utekelezaji wa Hatua la Beijing linatambua nguvu ya harakati za watetezi wa haki za wanawake na mashirika ya wanawake pamoja na mashirika ya kiraia katika kutunga sera na kusaidia manusura. Tafiti zimethibitisha kwamba uwepo wa mavuguvugu huru na thabiti ya watetezi wa haki za wanawake ni kigezo muhimu sana katika kuchochea mabadiliko na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
Hata hivyo, mwaka 2022, nchi zilitumia chini ya asilimia 1 ya misaada yao ya maendeleo katika kutatua ukatili wa kijinsia, na sehemu ndogo mno ya kiasi hicho ilifikia mashirika ya wanawake.
Mfuko wa UN wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, unaosimamiwa na UN Women kwa niaba ya mfumo wa UN, ndio mfumo pekee wa kimataifa wa kutoa misaada ya kifedha kwa mipango inayolenga kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Mwaka 1996, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 50/166 likitaka kuanzishwa kwa Mfuko huo kwa mujibu wa vipengeleo vilivyoainishwa kwenye Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji wa Hatua. Hadi leo hii, mfuko huo umetoa kati ya dola milioni 225 hadi milioni 670 kwa nchi 140 na maeneo.
Halikadhalika, Usawa wa Kizazi, Ushirika wa Hatua kuhusu Ukatili wa Kijinsia unafanya kazi kuongeza ufadhili wa kitaifa kwa mashirika yanayoongozwa na wasichana na wanawake hadi dola milioni 500 ifikapo mwaka 2026. Hii imewezesha kuleta mabadiliko makubwa kwenye ahadi kama vile mpango mpya wa UN Women wa ACT ambao unalenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake kupitia uwekezaji wa Euro milioni 22 kutoka Muungano wa Ulaya ili kuimarisha vuguvugu na harakati za wanawake za uchechemuzi.
Septemba 1995: Mkutano wa Nne wa Kimataifa kuhusu wanawake ukifunguliwa huko Beijing, China, Nana Konadu Agyeman Rawlings, Mke wa Rais wa Ghana, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano kuhusu Elimu, Afya na Maendeleo Endelevu. Photo: UN Photo/Chen Kai Xing.
Kusongesha haki za wasichana: Wakati huo na sasa
Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji wa Hatua lilikuwa nyaraka ya kwanza ya sera ya kimataifa kuhusu wanawake iliyojumuisha mkazo maalum juu ya haki za wasichana na kushughulikia ukatili dhidi ya wasichana.
Liliitaka serikali kuridhia Mkataba wa Haki za Mtoto, (CRC) kuhakikisha usajili wa kuzaliwa na kitambulisho cha kitaifa kwa wasichana, na kuendeleza ujumuishaji wa wasichana katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) pamoja na mafunzo ya ujuzi. Pia liliweka hatua za kuwalinda wasichana dhidi ya ukatili wa kijinsia, ikiwemo vitendo kama ndoa za utotoni, ukeketaji wa wasichana, na mimba za utotoni—masuala ambayo bado yanadhoofisha haki, afya, na ustawi wa wasichana hadi leo.
Ingawa maendeleo yamepatikana, changamoto mpya kama mabadiliko ya tabianchi na unyanyasaji wa mtandaoni zinazidisha ukatili dhidi ya wasichana, kama inavyooneshwa kwenye ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wakati huu ambapo wasichana milioni 9 wako katika hatari ya kuwa wameolewa wakiwa watoto ifikapo mwaka 2030, na msichana 1 kati ya 4 wa umri wa ujana akipata unyanyasaji kutoka kwa mwenza wake ifikapo miaka 19, Jukwaa la Utekelezaji la Beijing linabaki kuwa mwongozo muhimu wa kulinda haki za wasichana na kuhakikisha sauti zao zinasikika.