Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu 80,000 wamefungasha virago DRC kutokana na mapigano mapya na unyanyasaji wa kingono: UNHCR

Watu wanaerndcdelea kukimbia mapigano mashariki mwa DRC
© MONUSCO/Aubin Mukoni
Watu wanaerndcdelea kukimbia mapigano mashariki mwa DRC

Takriban watu 80,000 wamefungasha virago DRC kutokana na mapigano mapya na unyanyasaji wa kingono: UNHCR

Amani na Usalama

Hali ya ukosefu wa usalama na unyanyasaji wa kingono wa kutisha vimesababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbilia maeneo ya mipakani bila dalili ya uhamaji huo kukoma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,  limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR.

Katika taarifa yale iliyotolewa mjini Geneva na Kishasa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi wa Kimataifa cha UNHCR Patrick Eba, amesema "Karibu na maeneo ya mapigano, unyanyasaji wa kingono na ukiukwaji wa haki za binadamu bado umeenea, pamoja na uporaji na uharibifu wa nyumba na biashara za raia."
Akizungumza mjini Geneva, Bwana. Eba amewaambia waandishi wa habari kuwa majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini yanaendelea kuwa na hali ya kutokuwa na utulivu, huku "mamia ya maelfu ya watu wakiwa katika harakati ya kukimbia".
Karibu watu 80,000 wamekimbia mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda hadi nchi jirani, na takriban watgu 61,000 wamewasili Burundi tangu Januari, amesema Bwana. Eba.
Ugawaji wa dharura wa chakula unaendelea Mashariki mwa DRC
© WFP/Michael Castofas
Ugawaji wa dharura wa chakula unaendelea Mashariki mwa DRC

Waathirika 60 wa ubakaji kwa siku

Kwa mujib u wa UNHCR kesi 895 za ubakaji ziliripotiwa kwa wahudumu wa misaada katika wiki mbili za mwisho wa mwezi Februari pekee, ikiwa ni wastani wa zaidi ya wagtu 60 kwa siku.
Afisa huyo wa UNHCR amesisitiza hatari nyingine zinazowakabili raia, ikiwa ni pamoja na mabaki ya vilipuzi vinavyohatarisha maisha ya watoto na wakulima wanaojaribu kulima mashamba yao.
Jumatatu wiki hii, Ofisi ya Um oja wa M aztaifa hya kuratibu Masuala ya Kibinadamu na msaada wa dharura OCHA iliripoti kuwa watu wenye silaha walivamia angalau hospitali mbili katika mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma, na kuwateka nyara wagonjwa kadhaa.
Mapigano pia yamezuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa watu walioko njiani.
Shirika la Umoja wq Mataifa la Mpango wa Chakula WFP lim esema limesitisha shughuli zake za misaada katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro lakini lilikuwa linaanza tena misaada ya chakula ya dharura "katika baadhi ya maeneo ya Kivu Kaskazini kwa mujibu wa chapisho kwenye jukwaa lake la kijamii X lililolchapishwa leo Jumanne asubuhi, likilenga kuwafikia zaidi ya watu 210,000”.
Familia zilizokuwa zinaishi kwenye kambi za wakimbizi eneo la Goma, jimboni Kivu Kaskazini zikielekea kijiji cha Shasha jimboni humo humo.
UNICEF/Jospin Benekire
Familia zilizokuwa zinaishi kwenye kambi za wakimbizi eneo la Goma, jimboni Kivu Kaskazini zikielekea kijiji cha Shasha jimboni humo humo.

Kufutrushwa kwa lazima na kundi la M23

Ndani ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, uhamaji mkubwa wa watu umeendelea, kulingana na maagizo yaliyoripotiwa ya kundi la M23 kwa wakimb izi wa ndani  (IDPs) kuondoka katika kambi zilizo karibu na Goma, amesema Bw.ana Eba.
"Leo, ni karibu watu 17,000 pekee waliobaki wakikaa katika makambi ya wakimb izi wa ndani, shule na makanisa karibu na Goma, huku takriban watu 414,000 wamekuwa wakikimbia katika wiki nne zilizopita, wakihimizwa na mamlaka I;liyojitwalia madaraka kurudi katika vijiji vyao vya asili," ameeleza.
B wana Eba ameon hya kwamba “Kutokana na ukosefu wa usalama ulioenea mashariki mwa DRC, "watu wengi zaidi wanaweza kulazimika kuvuka mipaka wakitafuta usalama”.
Msimamo wa UNHCR kuhusu kurejea kwa wakimbizi hao ni kwamba "raia wa Congo wanaokimbia migogoro, pamoja na wale walio nje ya nchi, wanaotoka katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro, wanaweza kuhitaji ulinzi wa wakimbizi chini ya mifumo ya kisheria ya kimataifa na kikanda," amesema.
Afisa huyo wa UNHCR amesisitiza umuhimu wa "kufanya maamuzi yenye ufahamu kwa yeyote anayerejea kwa hiari katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro.”
Wakazi waliorejea makwao Sake DRC baada ya kukimbia mapigano M23.
UN News
Wakazi waliorejea makwao Sake DRC baada ya kukimbia mapigano M23.

Msamaha wa kusitisha ufadhili

Alipoulizwa kuhusu athari za kusitishwa kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu wa Marekani kwa shughuli nchini humo, msemaji wa UNHCR Eujin Byun amethibitisha kuwa shirika hilo lilipokea msamaha wa kuondoa kusimamishwa  kwa ufadhili kwa siku 90 kwa nchi chache zilizo na  dharura, ikiwa ni pamoja na DRC.
Msaada kwa ajili ya mgogoro wa sasa uliochochewa na mzozo wa muda mrefu katika eneo lenye utajiri wa madini umekuwa "daima ukifadhiliwa kidogo," amesema, akieleza matumaini kwamba UNHCR itaweza "kuendelea kusaidia dharura hii".
Kuna zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Congo kote barani Afrika, hasa katika nchi jirani.
Uganda inahifadhi zaidi ya nusu ya jumla hiyo, huku Burundi ikiwa imepokea idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wapya tangu mashambulizi ya ghafla ya M23 kuanza mwezi Januari.
Kabla ya mgogoro wa sasa, takriban watu milioni 6.7 walikujwa wakimbizi wa ndani nchini  DRC.