Rwanda na DRC zashutumiana ndani ya Baraza la Usalama kuhusu mapigano Goma
Rwanda na DRC zashutumiana ndani ya Baraza la Usalama kuhusu mapigano Goma
Amani na Usalama
Katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokaa jana Jumapili Januari 26 kuanzia asubuhi hadi majira ya mchana kwa saa za New York, Marekani, nchi majirani; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda zimeshutumiana vikali kuhusu mapigano yanayoendelea mashariki mwa DRC.
Katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokaa jana Jumapili Januari 26 kuanzia asubuhi hadi majira ya mchana kwa saa za New York, Marekani, nchi majirani; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda zimeshutumiana vikali kuhusu mapigano yanayoendelea mashariki mwa DRC.
Wakati DRC inaishutumu Rwanda kwama inawaunga mkono wapiganaji wa M23, Rwanda inakanusha ikisema M23 ni tatizo la ndani ya DRC kama yalivyo makundi mengine ya waasi nchini humo na pia inaishutumu DRC kuwaunga mkono kundi na FDLR ambalo Rwanda inadai lina lengo la kuishambulia Rwanda kwa misingi ya ukabila.
Waziri wa Mambo ya Nje wa DR Congo: 'Ulimwengu Unatazama; Ni Wakati wa Kuchukua Hatua'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thérèse Kayikwamba Wagner, alisema Rwanda inapanga "ukatili" dhidi ya nchi yake, hali inayoipeleka kanda hiyo kwenye ukingo wa janga.
"Kila dakika inayopita bila hatua za kimaamuzi na Baraza hili ni ushindi kwa mvamizi," alisema. "Ulimwengu unawatazama. Ni wakati wa kuchukua hatua."
Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) limeongeza mashambulizi, likikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano, na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu.
Ikiwa Goma, RDF imezuia barabara, kuhatarisha safari za ndege za kiraia na za kibinadamu, na kuendelea kushambulia kambi za watu waliokimbia makazi yao, alisema.
Aliongeza kuwa Mchakato wa Luanda, ulioidhinishwa na Muungano wa Afrika, umevurugwa na Rwanda, akisisitiza uporaji wa madini ya Congo na mashambulizi dhidi ya raia, walinda amani, na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu. DR Congo itakataa jaribio lolote la kuwajumuisha M23 katika Mchakato wa Luanda, ambao ni makubaliano kati ya Mataifa.
“Baraza la Usalama halipaswi kubaki kimya”, alisema, akilitaka kuchukua hatua za kimaamuzi, ikiwa ni pamoja na kuamuru kukomesha mapigano, kudai Rwanda iondoe wanajeshi wake katika ardhi ya Congo, na kuweka vikwazo pamoja na marufuku ya madini yote yanayodaiwa kutoka Rwanda.
Pia alitoa wito kwa Baraza hilo kuanzisha mfumo wa kushughulikia uvunjaji wa sheria za uhamishaji silaha kwa Rwanda na kuiondoa nchi hiyo katika orodha ya mataifa yanayochangia wanajeshi.
Rwanda yasema DR Congo haiwezi ‘kuchukua nje’ juhudi za kumaliza mgogoro
Katika Baraza la Usalama, mwakilishi wa Rwanda Ernest Rwamucyo alisema kuongezeka kwa shughuli za kijeshi DRC kunawakilisha tishio kubwa la usalama kwa nchi yake. Uwepo wa vikosi vya Congo na mamluki ni "hali isiyokubalika," alisema. Wakati huo huo, Rwanda si tishio kwa MONUSCO.
Ingawa vikosi vya Umoja wa Mataifa vilianza kutumwa miaka 26 iliyopita, MONUSCO sasa inavuka mamlaka yake, alisema na kuongeza kuwa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kinatoa msaada kwa mamluki na kinahusishwa kwenye mgogoro kwa njia inayokiuka sheria za kuunga mkono makundi ya silaha.
Balozi Rwamucyo alisema, “kwa kweli, jumuiya ya kimataifa inapaswa kubeba lawama kwa sehemu kwa mgogoro wa sasa kutokana na kushindwa kutatua mizizi ya tatizo na kutoa suluhisho la vitendo, aliongeza.”
"Tumejitolea kupata suluhisho la amani," alisema na kuongeza kwamba hata hivyo, DRC inapaswa kuchukua jukumu la kutatua mambo yake yenyewe na haiwezi "kuchukua nje" juhudi za kutatua yanayoendelea ndani ya nchi.