Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa FAO wa kugawa mbegu na pembejeo umenikomboa mimi na familia yangu: Mkulima Noor Ahmed

Wakulima wa ngano nchini Afghanistan
UNAMA
Wakulima wa ngano nchini Afghanistan

Mradi wa FAO wa kugawa mbegu na pembejeo umenikomboa mimi na familia yangu: Mkulima Noor Ahmed

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika jimbo la Kandahar nchini Afghanistan Noor Ahmen mkulima wa ngano amenufaika na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO unaotoa mafunzo ya kilimo, kugawa  mbegu na pembejeo kwa wakulima

Mradi huu ambao unafadhiliwa pia na Benk ya Dunia umezisaidia familia nyingi za wakulima sio tu kuinua kipato bali pia kuboresha lishe na kukabili changamoto ya kutokuwa na uhakika wa chakula.
 
Katika jimbo la Kandahar nchini Afghanistan wanaume wakulima wa ngano wanakusanyika kwenye kituo cha shirika la FAO ili kupokea mbegu za ngano na pembejeo zingine ili kwenda kupanda katika mashamba yao ambayo yameshatayarshwa.
Ngano ni uti wa mgongo kwa watu wa Afghanistan kwani inawapa uwezo wa kuishi, kujikimu na kuhakikishia uhakika wa chakula kwa mamilioni ya watu. Noor Ahmed mmoja wa maelfu ya wakulima wa Kandahar maisha yake yamebadilika baada ya mradi wa FAO kuwasili “Nilikuwa masikini, lakini nilikuwa na ardhi na maji, hata hivyo sikuwa na pesa ya kununua mbolea na mbegu. Sikuweza kumudu kununua mbolea hivyo nililazimika kukopa fedha ili ninunue Na siku hizi hakuna mtu anayetaka kukopesha mtu pesa na wanakopesha ni kwa faia kubwa hivyo ningekopa ningekuwa kwenye madeni hivi sasa “
Mkulima wa ngano akitoka shambani kuvuna na mwanaye
FAO
Mkulima wa ngano akitoka shambani kuvuna na mwanaye
Kwa bahatti nzuri mradi wa FAO wa ugawaji pembejeo za kilimo na kutoa mafunzo ulimfikia Noor kabla hajatumbukia kwenye lindi la madeni. FAO ilinunua tani 42,000 za mbegu za ngano zilizotosheleza kusaidia maisha ya watu milioni 5.88 kwa mbegu na lishe , na mradi huo umekuwa mkombozi wa Noor “FAO ilitugawia sio tuu ngano ya chakula na mbegu bali pia mbolea, walitupatia mafunzo ya jinsi ya kuhifadhi mbegu za ngano na mbinu mbalimbali za kilimo, na pia kutuelekeza kuhusu wakati na matumizi ya mfumo wa umwagiliaji.”
Mbegu hizo kutoka FAO zimetiwa dawa hivyo ni bora kuhimili magonjwa ya mazao lakini pia kutoa mavuno mengi na matokeo yake ni faida za kipato na uhakika wa chakula. Kwa Noor hii ni neema “Mbugu hizo zilizoboreshwa zinazaa mara mbili ya mbegu za asili . Ngano tunayoipata inaweza kutumika kuoka mikate yenye lishe na tukaiuza kwa bei kubwa”
Na kwa kuwa mavuno apatayo ni mengi anatekeleza usemi wa akiba haiozi “Tunapovuna ngano yetu tunaweka nyingine kwa ajili ya mbegu. Na mtu anapotaka mbegu hizo kutoka kwetu tunabadilishana naye na ngano ya matumizi ya chakula. Na mbegu hizi tunaweza kuzihifadhi kwa mwaka mmoja hadi minne.”
Kilichosalia kwa Noor ni kutoa asate kwa FAO kwani anasema mradi huu usingekuwepo “Ingeathiri vibaya maisha yetu kwa sababu mbegu zetu hazikuweza kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili yetu. Lakini mbegu hizi tulizopokea ni za ubora wa hali ya juu na zinakuja na mbolea ambayo inaongeza mara mbili au mara tatu ya mavuno.”
Kwa mujibu wa FAO, kwa wakulima wa Kandahar kukumbatia mbegu hizi bora sio tu wanachagiza mazao yenye afya bali pia kilimo endelevu.