Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yasikitishwa na ukosefu wa mafuta Gaza na kuonya juu ya athari zake ikiwemo uhaba wa maji

Mtoto mdogo wa Kipalestina aliyevaa shati jekundu ameketi kwenye ukingo wa zege huku wengine wakiwa wamemzunguka wakichota maji kwenye mitungi.
© UNRWA Mtoto ameketi karibu na kituo cha maji huko Gaza.

UN yasikitishwa na ukosefu wa mafuta Gaza na kuonya juu ya athari zake ikiwemo uhaba wa maji

Amani na Usalama

Wakati makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa huko Gaza na Hamas yakionekana kukaribia kufikiwa, operesheni za kibinadamu bado "ziko kwenye hatihati ya kuporomoka, na kuwaweka raia waliozingirwa kwenye uhaba unaokaribia wa maji ya kunywa kutokana na ukosefu wa mafuta ya kutosha yameonya leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu  na misaada ya dharura OCHA, vifaa muhimu vya maji, usafi na usaf wa mazingira na shughuli ziko hatarini kusitishwa ikiwa hakuna mafuta ya ziada yatakayopokelewa kwa haraka Gaza.

Changamoto ya uhaba wa mafuta inaendelea kutishia utendakazi wa huduma muhimu za afya, kuanzia mashine za kuongeza hewa ya oksijeni katika vitengo vya wagonjwa mahututi hadi mashine za kusafisha damu, limeonya shirika la OCHA.

Kulingana na huduma za Umoja wa Mataifa za maji na usafi wa mazingira WASH, ukosefu wa mafuta unatishia kusimamisha huduma muhimu katika sekta hiyo katika Ukanda mzima wa Gaza.

Mashirika hayo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yameonya kwamba "Endapo mafuta hayatapekelewa kwa haraka, huduma zote za WASH kaskazini na kusini mwa Gaza zitakoma mara moja".

Tishio kwa shughuli za usimamizi na udhibiti wa maji taka

Kwa sasa, ukiacha kiwanda cha kuondoa chumvi kusini mwa Gaza, ambacho Novemba mwaka jana kiliunganishwa tena kwa njia ya umeme kutoka Israel na na kufanya hakitegemei tena mafuta kufanya kazi kwingine kote ni changamoto. "Washirika wa WASH pia hawataweza kusafirisha na kusambaza maji," limeongeza shirika la OCHA katika ripoti yake ya hivi karibuni ya hali Gaza.

Kwa kuongezea, shughuli zote za usimamizi wa maji taka na taka ngumu zitasimama.

Kulingana na OCHA, janga la sasa ni "kilele tu cha uhaba wa mafuta wa muda mrefu ambao umeathiri vibaya shughuli zote za WASH katika mwaka wa 2024 kwenye eneo la Palestina.

Kwa nguzo ya WASH, kiwango cha kila siku cha mafuta kilichopokelewa na washirika kilishuka hadi wastani wa lita 8,700 mwezi Novemba na chini ya lita 12,000 mwezi Desemba, ikilinganishwa na lita 70,000 zinazohitajika kwa siku angalau kwa shughuli muhimu za WASH, kama vile usukumaji wa maji, huduma  za matibabu na usambazaji, kusukuma, kumwaga na kuhamisha maji taka, pamoja na udhibiti wa taka ngumu.

Zaidi ya hayo, tangu tarehe 6 Oktoba 2024, upatikanaji wa vituo vya kuzalisha maji kaskazini mwa Gaza na mashariki mwa Gaza umekuwa ukikataliwa mara kwa mara na mamlaka ya Israeli, na kupunguza zaidi uwezo wa muhimuli wa kutoa maji kwa wakazi wa Gaza.

Sehemu ya ndani ya jengo lililoteketea huko Gaza, ikiwa na vifusi, uchafu, na kuta zilizoungua.
© UNRWA Kituo cha huduma za afya ya akili kwa watoto wenye ulemavu wa macho katika Jiji la Gaza kiko magofu. (Maktaba)

Tishio kwa shughuli za usimamizi wa maji machafu na taka

Kwa sasa, isipokuwa ni kiwanda cha kuondoa chumvi kusini mwa Gaza, ambacho mnamo Novemba kiliunganishwa tena kwa njia ya umeme kutoka Israel na hakitegemei tena mafuta kufanya kazi. "Washirika wa WASH pia hawataweza kusafirisha na kusambaza maji," OCHA iliongeza katika ripoti yake ya hivi punde ya hali.

Kwa kuongezea, shughuli zote za usimamizi wa maji machafu na taka ngumu zingesimama. Kulingana na OCHA, mzozo wa sasa ni "kilele tu cha uhaba wa mafuta wa muda mrefu ambao umeathiri vibaya shughuli zote za WASH katika mwaka wa 2024" katika eneo la Palestina.

Kwa nguzo ya WASH, kiwango cha kila siku cha mafuta kilichopokelewa na washirika kilishuka hadi wastani wa lita 8,700 mwezi Novemba na chini ya lita 12,000 mwezi Desemba, ikilinganishwa na lita 70,000 zinazohitajika kwa siku angalau kwa shughuli muhimu za WASH, kama vile uzalishaji wa maji; matibabu na usambazaji. kusukuma, kumwaga na kuhamisha maji machafu, pamoja na udhibiti wa taka ngumu.

Zaidi ya hayo, tangu tarehe 6 Oktoba 2024, upatikanaji wa vituo vya kuzalisha maji kaskazini mwa Gaza na mashariki mwa Gaza ya Gaza umekuwa ukikataliwa mara kwa mara na mamlaka ya Israeli, na kupunguza zaidi uwezo wa Nguzo wa kutoa maji kwa wakazi.

Hatari za kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza

Ukosefu wa mafuta na vikwazo vya ufikiaji umewalazimu watendaji wa WASH kufanya uchaguzi usiowezekana, kulazimika kuamua kila siku kati ya kutoa maji, kusukuma maji machafu, kurekebisha maji au uvujaji wa maji machafu, au kuhamisha taka ngumu.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ynasema watu waliokimbia makazi yao, haswa kaskazini mwa Gaza, wamelazimika kuishi kwa kiwango kidogo sana cha maji ya kunywa, kupikia, na usafi binafsi.

Kwa kawaida wanalazimika kufanya "safari ndefu na hatari Kwenda kuchota maji, au hata kutumia vyanzo vya maji visivyo salama."

Masharti haya yanachangiwa na ukosefu wa mafuta kwa ajili ya udhibiti wa maji taka na taka ngumu, ambao unaendelea kusababisha umwagikaji wa maji taka na kuongezeka kwa mkusanyiko wa taka ngumu ndani au karibu na maeneo ya watu waliofurushwa mwakao.

Hali kama hiyo inazidisha kusambaa kwa wadudu, magonjwa ya kuambukiza na hatari nyingine za afya ya umma, imeonya OCHA.

Mgogoro wa ukosefu mafuta pia ni tishio kwa hospitali.

Kwa upande wake, kikundi cha sekta ya Afya kinaripoti kuwa “hospitali zote ambazo bado hazifanyi kazi zimemaliza akiba yao ya mafuta. Sasa wanategemea kiasi cha mafuta yanayotolewa kwa msingi wa kesi kwa kesi kujaribu kulinda huduma muhimu zaidi".

Tatizo la mafuta ambalo limechangiwa zaidi na uporaji wa meli za mafuta, linaendelea kutishia utendakazi wa vituo vya afya.

OCHA imesema “Hii inaathiri moja kwa moja wagonjwa wapatao 2,000 katika Deir al Balah, Khan Younis na Rafah, asilimia 10 kati yao wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi (ICUs), na takriban wagonjwa 220 kutoka kaskazini mwa Gaza, 70 kati yao wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.”

Shirika hilo limesema , tatizo la mafuta pia linatishia kuendelea kufanya kazi kwa mashine 75 za Gaza za kusafisha damu, ambazo ni njia ya kuokoa maisha kwa wagonjwa wapatao 700 wanaougua magonjwa ya figo, wengi wao wakiwa katika maeneo ya kati na kusini mwa Gaza.

Kabla ya uhasama uliopo sasa kuzuka, mashine 198 za kusafisha damu zilipatikana katika Ukanda wa Gaza.