Baraza Kuu la UN lafanya tena kikao maalum cha dharura kuhusu Palestina
Baraza Kuu la UN lafanya tena kikao maalum cha dharura kuhusu Palestina
Amani na Usalama
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeanza tena kikao chake maalum cha kumi cha dharura kuhusu hatua haramu za Israel katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Rais wa Baraza Kuu aliamua kurejesha kikao hiki maalum cha kumi cha dharura kwa ombi la Wenyeviti wa Kundi la Waarabu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Ofisi ya Uratibu ya Jumuiya Zisizofungamana na Upande wowote.
Ili kushuhudia mjadala huu bofya hapa
Jinamizi la Gaza lazima likomeshwe, amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Philemon Young, akifungua kikao hicho maalum cha dharura kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati. Amekumbushia kuwa zaidi ya raia 43,000 wameuawa na karibu 100,000 wamejeruhiwa wakati wa vita katika ukanda huo.
Wanaongoza, mtawalia, Kundi la Nchi za Kiarabu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Ofisi ya Uratibu ya Harakati Zisizofungamana na Siasa.
Rais wa Baraza
"Mahitaji ya jumuiya ya kimataifa yako wazi," Young amesema, akiongeza kuwa Baraza la Usalama "limepooza" na haliwezi kutekeleza kazi yake ya msingi, ambayo ni kudumisha amani na usalama.
Young amesema kuwa "mgogoro huo utaisha pale tu Waisraeli na Wapalestina watakapoweza kuishi bega kwa bega katika mataifa yao huru kwa amani, usalama na utu."
Pia amesisitiza jukumu muhimu la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) katika eneo hilo. "Shirika hilo linatoa ulinzi, makazi, chakula na maji, pamoja na huduma za matibabu kwa mamilioni ya Wapalestina, hasa wale walio katika hali ngumu zaidi katika Ukanda wa Gaza," alisema.
"Kwa hiyo sina budi kwa mara nyingine tena kueleza wasiwasi wangu mkubwa juu ya uamuzi wa hivi karibuni wa bunge la Israel wa kupitisha sheria mbili ambazo zikitekelezwa, zitazuia UNRWA kufanya kazi yake muhimu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki. ,” Rais wa Baraza Kuu amesema.
Ameongeza kuwa ikiwa UNRWA haitaweza kutekeleza operesheni zake, hali ya kibinadamu katika ardhi za Palestina itazidi kuwa mbaya.
Kikao hiki kimepangwa kufanyika katika sehemu mbili, ya kwanza ni hii iliyifanyika leo Desemba 4 na ya pili itakuwa tarehe 11mwezi huu hu wa Desemba.