Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ateta na Rais wa Brazili mjini Rio de Janeiro
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ateta na Rais wa Brazili mjini Rio de Janeiro
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ambaye yuko mjini Rio de Janeiro nchini Brazili kwa ajili ya mkutano wa mataifa 20 tajiri duniani au G20 amekutana na kuzungumza na Rais wa Brazili Luiz Inácio Lula da Silva.
Katika mkutano wao leo mjini Rio de Janeiro Guterres na Lula da Silva wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo “umuhimu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kurekebisha usanifu wa masula ya fedha wa kimataifa, na kushughulikia changamoto kubwa za kimataifa.”
Pia wawili hao walikubaliana juu ya udharura wa kutekeleza hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu na Rais wa Brazil kwa Pamoja wmesisitiza haja ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza azma ya kuhakikisha mafanikio ya mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa mkataba wa mkataba Umoja wa Mataifa wa mabadiliiko ya tabianchi COP29 na COP30, pamoja na kujitolea kwa malengo ya kitaifa ya kulabili mabadiliko ya tabianchi NDCs yanayoambatana na kupunguza kiwango cha joto duniani na kusalia nyuzi joto 1.5C.
Katibu Mkuu ameshukuru kwa mchango mkubwa wa Brazil katika ajenda ya kimataifa.