Tutahakikisha Kiswahili kinasambaa duniani na kusongesha ajenda za UN: Waziri Ndumbaro
Tutahakikisha Kiswahili kinasambaa duniani na kusongesha ajenda za UN: Waziri Ndumbaro
Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa lugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu.
Kongamano hilo la siku nne litakalokunja jamvi Jumapili tarehe 10 Novemba limeandaliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano na wenyeji Cuba.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kongamano hilo Waziri wa utamaduni, sana ana michezo wa Tanzania Dkt Damas Daniel Ndumbaro amesema hili ni kongamano la kimataifa la Kiswahili na ajenda yake kuu ni kukifanya Kiswahili kivike mipaka , kiende kimataifa na kibebe jumbe tofauti kuwapelkea Waswahili popote walipo duniani waweze kuelewa dunia inaendaje, jumuiya ya kimataifa inaamua nini kwa lugha yao na wao waweze kushiriki michakato ya kimataifa.
Kwa nini kongamano hili linafanyika Havana Cuba
Dkt. Ndumbaro amesema kongamano hili la Kiswahili limeshazunguka maeneo mbalimbali na lina kududi la kusema tunakuletea Kiswahili kwa lugha yako .
Ameongeza kuwa sasa safari hii ni zamu ya Wahispaniola, watu ambao wanaongea lugha ya kihispania hivyo Kiswahili kinakwenda kwa Wahispaniola.
Amesema na Cuba ni moja ya nchi zinazozungumza Kihispania na nchi zinazozungumza ugha hiyo ziko nyingi kwa nini Cuba? amesema ni kwa sababu Kiswahili ni lugha ya Afrika, lugha ya kimataifa ya asili ya Afrika na Cuba ina mchango Mkubwa katika ukombozi wa bara la Afrika.
Na kwa mantiki hiyo amesema “Waafrika wamesema kwamba tunakuja kufanyia Cuba ambao tulishirikiana nao kukomboa bara la Afrika na kwakua Kiswahili ilikuwa lugha ya ukombozi kwa hiyo Wahispaniola wote tukutane Cuba kwa sababu hizo.”
Kiswahili ni Lugha ya ukombozi na lugha ya amani?
Waziti Ndumbaro amebainisha kuwa “Ajenda ziko nyingi lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha sasa Kiswahili kinakuwa sehemu muhimu ya lugha zinazotambulika kimataifa.”
Akaenda mbali zaidi na kusema kuwa hususan katika Umoja wa Afrika na katika Umoja wa Mataifa ili Waswahili popote walipoduniani takriban milioni 500 waweze kushughulika na shughuli mbalimbali za kimataifa.
Akizungumzia mchango wa Kiswahili katia ajenda za Umoja wa Mataifa amesema “Kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya ukombozi, lugha ya amani ajenda kkubwa pia ni kuhakikisha kwamba tunakitumia Kiswahili katika kuleta amani na kuifanya dunia iwe salama zaidi.”
Kiswahili na malengo ya maendeleo endelevu SDGs
Waziri Ndumbaro amekumbusha kwamba Umoja wa Mataifa na malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja huo yanasisitiza kwamba hakuna mtu yeyote anayepaswa kuachwa nyuma, yaani kila mtu awepo kwenye boti hiyo, kwenye meli hiyo, kwenye Safina hiyo ili tusonge mbele.
Hata hivyo amesema “Sasa hivi watu takribani milioni 500 duniani wameachwa nyuma kinyume kabisa na malengo hayo endelevu .”
Hivyo amesema “Ili tutekeleze vizuri malengo hayo ya maendeleo endelevu chini ya Umoja wa Mataifa lazima tukitumie Kiswahili na yale malengo yatafsiriwe Kiswahili na Waswahili waweze kuyasoma, kuyaelewa na ujume waipate kwa lugha yao wanayoijua ya Kiswahili, hivyo hapa pia Kiswahili kinatekeleza malengo ya maendeleo endelevu.”
Je waalikwa katika kongamano hii ni kina nani?
Waziri huyo wa utamaduni , sana ana michezo wa Taanzania amesema katika kongamano hili zaidi ya wageni 400 wanatarajiwa kutoka katika pande zote za dunia.
Amesema wako wanaotoka Tanzania ambako ndio makao makuu ya Kiswahili, wanatoka barani Ulaya nchi nyingi zimeleta watu wao, kutoka Amerika Kaskazini ambbapo watu wamekuja kutoka Marekani na Canada na tuko Cuba maana yake Amerika ya Kati nay a Kusini watu wamekuja na Afrika pia.
Kwa hivyo amesema hili ni kongamano la kimataifa na sit u kwa kuwa linafanyika Cuba lakini pia hata wahudhuriaji wake, watoa mada wake wana akisi ule umataifa wake.
Nini ujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili
Dkt. Ndumbao amehitimisha akisema “Ujumbe wangu kwa waswahili na wasio waswahili. Kwa waswahili sasa wajue lugha yao pendwa imekuwa na sasa imevuka mipaka.”
Kwani amesema imetambuliwa na Umoja wa Mataifa na imepewa siku mahsusi Pamoja na UNESCO kuiadhimisha tarehe 7 mwezi wa 7 hii ni heshima kubwa duniani.
Na kwa wasio waswahili amesema “Wajue kwamba zaidi ya watu milioni 500 wanaongea Kiswahili ukitaka kuwasiliana nao na wewe ongea Kiswahili.”