Harakati za TEDI-Tanzania kusongesha TEHAMA katika maeneo ya pembezoni
Harakati za TEDI-Tanzania kusongesha TEHAMA katika maeneo ya pembezoni
Malengo ya Maendeleo Endelevu
Ikiwa imesalia takribani miaka mitano na miezi michache kuelekea kilele cha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, wadau mbalimbali wanaendelea kuhakikisha muda huo mfupi uliosalia unatumika vizuri ili kufikia mwaka 2030 hatua kubwa ziwe zimepigwa katika malengo hayo 17.
TEDI-Tanzania, shirika lisilo la kiserikali nchini Tanzania linalojishughulisha na miradi ya maendeleo ya elimu na vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo kwa kuwawezesha wananchi kiteknolojia katika zama hizi ni kuwapa nyenzo ya kujikwamua katika umaskini ni miongoni mwa wadau hao.
Gloria Anderson Mwanzilishi na Mkurugenzi wa TEDI yaani Tanzania Enlightment and Development Innovation hivi karibuni alihudhuria moja ya mikutano kandoni mwa Mkutano wa Zama Zijazo yaani Summit of The Future uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata wasaa wa kuzungumza na Gloria kuhusu TEDI – Tanzania inavyoendelea kutekeleza SDGs na Gloria anaanza kwa kueleza ushiriki wake katika Mkutano wa Zama Zijazo.