Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN wakunja jamvi kwa wito wa kuipa fursa amani

Rais wa Baraa Kuu Philémon Yang akifunga mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79
UN Photo/Loey Felipe
Rais wa Baraa Kuu Philémon Yang akifunga mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la UN wakunja jamvi kwa wito wa kuipa fursa amani

Masuala ya UM

Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha ulihitimishwa umekunja jamvi leo Jumatatu jioni, ambapo waliohudhuria wamewasikiliza wawakilishi wa nchi 190, wakiwemo wakuu wa nchi 71, wakuu wa serikali 42, makamu 6 wa rais na wana wafalme , manaibu waziri mkuu 8, mawaziri wakuu 53, manaibu waziri 3, wakuu wa ujumbe 7 na waangalizi 3.

Akifunga mjadala huo Rais wa Baraza Kuu, Philemon Yang, “ameelezea kusikitishwa na uwakilishi mdogo wa wanawake katika mijadala mkuu wa mwaka huu, akibainisha kuwa karibu asilimia 10 pekee ya wawazungumzaji ndio walikuwa wanawake, akisema tofauti hii kubwa inaashiria changamoyo ya kina zaidi ambayo hatuwezi kuipuuza, huku akisisitiza haja ya juhudi zaidi kufikia usawa wa kijinsia.”

Haja ya kuchukua hatua kuzuia vita kusambaa kote Mashariki ya Kati

Yang pia amezungumzia machafuko yanayoongezeka katika maeneo mengi ya dunia, ikiwa ni pamoja na Gaza, Lebanon na Sudan.
Ameongeza kuwa amani katika Mashariki ya Kati iko hatarini, akitoa wito kwa ulimwengu kutoruhusu vita vinavyoendelea kusambaa kote Mashariki ya Kati eneo ambalo ni tete.
Alitoa wito kwa pande zote Israel, Hamas na Hizbullah kufikia usitishaji mapigano kama jambo la dharura na kuwaachilia mateka wote ambao bado wako kizuizini mara moja.
Pia ametoa wito kwa wale wenye ushawishi kwa pande husika katika mzozo kudai usitishaji vita na mazungumzo mara moja, na kuzitaka nchi zote zinazosambaza silaha katika eneo hilo kujiepusha na vitendo hivyo na kuyapa kipaumbele mazungumzo na suluhu za kidiplomasia.
Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu UNGA79 wafunga pazia
UN Photo/Mark Garten
Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu UNGA79 wafunga pazia
Yang amesisitiza kile alichokisema katika ufunguzi wa mjadala mkuu kwamba ni suluhu ya Serikali mbili tu, kwa kuzingatia maazimio husika ya Umoja wa Mataifa, ndilo linaloweza kuhakikisha amani na usalama wa kudumu kwa watu wote wa Israel na Palestina na maeneo mengine ya kanda hiyo.

Kudumisha umoja katika utofauti wetu

Bwana Philemon Yang alichagua mada "Umoja katika utofauti wetu, kwa ajili ya kukuza amani, maendeleo endelevu na utu wa binadamu kwa wote, kila mahali" kuwa maudhui ya urais wake wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha 79.
Amesema kauli mbiu hiyo haikuwa mwongozo tu. Ni wito wa kuchukua hatua," na inatukumbusha kuwa nguvu zetu zinatokana na utofauti wetu, uwezo wetu wa kuwaunganisha wadau kwenye malengo yetu ya pamoja. Sote tusonge mbele kwa moyo wa umoja na uwajibikaji wa pamoja. Tuendelee na kazi yetu na lengo la wazi la kujenga mustakabali wenye amani, usawa na heshima kwa wote."