Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dhahabu na Koltani vyazidi kushamirisha mapigano Mashariki mwa DRC - Keita

Bintou Keita atoa taarifa kwa Baraza la Usalama UN kuhusu hali ilivyo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UN Bintou Keita, Mwakilishi Maalum Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC akizungumza katika Baraza la Usama Mjini New York Marekani.

Dhahabu na Koltani vyazidi kushamirisha mapigano Mashariki mwa DRC - Keita

Amani na Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wameelezwa jinsi ushindani wa uchimbaji kupita kiasi na biashara ya maliasili huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unavyozidi kuchochea mapigano kwenye eneo hilo, madini kama vile dhahabu na Koltani. 

Hayo yamo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama na Mwakilishi wake Maalum nchini DR Congo, Bintou Keita, ikianzia tarehe 20 Juni hadi 19 mwezi huu wa Septemba.

Bi. Keita amesema “jimboni Ituri, mapigano yaliyoshamiri hivi karibuni yamechochewa na vikundi vilivyojihami vikijaribu kudhibiti machimbo ya madini. Kwa kuwa faida imeongezeka kwa kupanua machimbo ya dhahabu, vikundi vilivyojihami vimegeuka kuwa wajasiriamali wa madini. Vikundi ya kijamii na jeshi la serikali lisilo na uwezo kifedha wakihaha kudhibiti makundi ambayo yameimarika kijeshi na kifedha.”

Mwakikilishi huyo ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe waUmoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MMONUSCO, amesema jimboni Kivu Kaskazini, M23 inazidi kuimarisha udhibiti wake wa maeneo ya Masisi na Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini, na hivyo wameweza kudhibiti kabisa uzalishaji wa madini  ya Koltani.

Madini ya Tantalum yawapatia waasi wa M23 dola 300,000 kila mwezi

Ameongeza kuwa “biashara kutoka eneo la Rubaya linalokadiriwa kuchangia zaidi ya asilimia 15 ya uzalishaji wa madini ya Tantalum, imepatia M23 dola 300,000 kila mwezi. Hii inatia hofu na lazima ikomeshwe,.”

Wajumbe pia walipata ripoti kutoka kwa Thérèse Nzale-Kove, mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mfuko kwa Ajili ya Wanawake wa DRC au FFC.

Bi. Nzale-Kove amesema kuondoka kwa MONUSCO jambo ambalo limesharidhiwa lazima kuzingatie changamoto za mifumo ya ulinzi wa haki za binadamu na ukosefu wa haki za kijamii na madhara yake.

Ametaka kuzingatiwa kwa tathmini za kile walichojifunza baada ya MONUSCO kuondoka majimbo ya Tanganyika na Kivu Kusini.

Kwa sasa MONUSCO imesalia jimbo la Kivu Kaskazini na inatakiwa iwe imeondoka kabisa DRC ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Mwanaharakati wa haki za wanawake ataka mambo 3 yazingatiwe

Wajumbe pia walipata ripoti kutoka kwa Thérèse Nzale-Kove, mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mfuko kwa Ajili ya Wanawake wa DRC au FFC.
 
Amemulika maeneo makuu matatu. Mosi; Athari hasi zitokanazo na janga la kibinadamu hivi sasa Mashariki mwa nchi; Pili, ushiriki wa wanawake kwenye michakato ya kisiasa na amani; na Tatu, umuhimu wa kuchukua hatua mahsusi kulinda rai ana wanawake watetezi wa haki za binadamu mara baada ya MONUSCO kuondoka kabisa DRC ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
 
Bi. Nzale-Kove akifafanua jambo la kwanza amesema janga la kibinadamu nchini DRC limeathiri Vinaya wanawake, wasichana na watoto likiwa viwango vikubwa vya wakimbizi wa ndani, ongezeko la ukosefu wa usalama na  uhaba wa chakula.
 
Zaidi ya hapo ni ongezeko la ukatili wa kingono na kijinsia pamoja na ndoa za lazima kwa watoto wa kike na watoto hao kujikuta wanalazimika kujitumbukiza kwenye biashara ya ngono ili kujikimu kimaisha.
Amegusia ubakaji wa magenge uliofanywa kwa wanawake na wasichana 268 kwenye gereza la Makala mjini Kinshasa akisema, “kwa bahati mbaya, idadi kubwa ya  manusura wa tukio hilo hawawezi kupata huduma muhimu. Sababu ni uoga, unyanyapaa na ukosefu wa mfumo wa huduma hizo ndani ya mfumo wa afya nchini DRC.”
 

Michakato yote ya amani na kisiasa wanawake wawemo

Akageukia ujumuishaji wa wanawake na wasichana kwenye michakato ya amani na kisiasa  nchini humo akisema, “wanajitahidi bila kuchoka kuchangia katika juhudi za amani na kukabiliana na janga la kibinadamu. Mchango wao uko dhahiri ijapokuwa juhudi zao hazitoshelezi na sio endelevu.”
 
Bi Nzale-Kove amesema ndio maana, FFC imeunda tanuru la fikra la wanawake likijulikana kama  Ushirikiano wa Wanawake kwa ajili ya Amani na Usalama. “Ni vema wanawake walio kwenye mashirika ya kiraia waweze kushiriki kikamilifu na kwa ufanisi kwenye maeneo yote ya michakato ya sasa ya amani. Mchakato wa Nairobi na Mchakato wa Luanda pamoja na fursa zingine za kikanda za kuleta amani.”
 
Amesema Makubaliano ya Amani ya Angola yaliyoratibiwa na Rais João Lourenço wa Angola, ni hatua muhimu ambayo wanawake wa DRC wanaiunga mkono kwa sababu wana hamu ya kuwa na jawabu la kudumu kwenye mzozo Mashariki ya DRC ali mradi jawabu hilo linaheshimiwa.
 

MONUSCO kuondoka DRC jambo muhimu ni lipi?

Kuhusu kuondoka kwa MONUSCO, Bi. Nzale-Kove amesema ni  jambo ambalo limesharidhiwa lazima kuzingatie changamoto za mifumo ya ulinzi wa haki za binadamu na ukosefu wa haki za kijamii na madhara yake.
 
Ametaka kuzingatiwa kwa tathmini za kile walichojifunza baada ya MONUSCO kuondoka majimbo ya Tanganyika na Kivu Kusini.
 
Kwa sasa MONUSCO imesalia jimbo la Kivu Kaskazini na inatakiwa iwe imeondoka kabisa DRC ifikapo mwisho wa mwaka huu.