Zambia: Migogoro inayoendelea duniani imeiathiri sana Afrika
Zambia: Migogoro inayoendelea duniani imeiathiri sana Afrika
Masuala ya UM
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Zambia Mulambo Hamakuni Haimbe akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumamosi jijini New York, Marekani, amesema migogoro iliyoshika kasi sehemu mbalimbali za dunia kuanzia Sudan, DR Congo, Mashariki ya Kati na Ukraine imesababisha changamoto kubwa duniani.
Amesema hususan Afrika ambako bara hilo limeshuhudia ongezeko kubwa la bei za chakula, mafuta na bidhaa zingine muhimu, hivyo ameiomba jumuiya ya kimataifa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha migogoro hii mikubwa inapatiwa utatuzi haraka.
Kuhusu mabadiliko ya tabianchi Waziri Haimbe amesema Zambia ni muathiriwa mkubwa wa janga hilo na mwaka huu imekabiliwa na ukame ambao haujawahi kushuhudiwa na kulifanya taifa hilo kutangaza hali ya dharura.
Kwa muktadha huo ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi hususan kwa nchi za Afrika ambazo mchango wake wa zahma hiyo ni mdogo.
Malengo ya maendeleo endelevu SDGs
Bwana Haimbe amesema ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu umeendelea kuwa changamoto kwa nchi nyingi ikiwemo Zambia.
Na kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa ni asilimia 17 pekee ya malengo hayo ndio yatakayo fikiwa.
Hivyo ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutathimini umpya kiwango cha riba ya madeni inayokopesha hasa kwa nchi masikini ili badala ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kulipa madeni wazieleeze fedha hizo katika kusongesha SDGs.
Ameendelea kuongeza kuwa teknolojia ni nyenzo muhimu ambay inaweza kuwa dawa mujarabu ya kufikia malengo hayo ya maendeleo yanayosuasua hasa katika sekta za kilimo, elimu, miundombinu, afya na malengo mengineyo na kutoa wito wa kuziba pengo la upatikanaji wa teknolojia ikiwemo akili mnemba au AI, kuzisaidia nchi zinazoendelea kutumia fursa hiyo kufikia malengo hayo ya maendeleo.
Changamoto nyingine ambayo imekuwa ikisumbua Zambia ni ndoa za utotoni ambapo ammesema hivi sasa Zambia imechukua hatua ikiwemo kuweka sheria ya kutokomeza mila potofu na mikakati ya kotokomeza janggi hilo linalopora muskabali wa watoto wengi wa kike barani Afrika.
Amezitaka nchi nyingine zenye changamoto hiyo kuchua hatua zote
Kulinda mustakbali wa wasichana na kutokomezandoa za utotoni ifikapo mwaka 2030.
Amehitimisha kwa kusema kuwa baada ya kupitishwa kwa mkataba wa Zama Zijazo sasa ni jukumu la kila nchi kuutekeleza kwa uthabiti endapo dunia inataka kuwa na mustakbali bora kwa vizazi vijazo, ulio na amani, usawa na kufaidisha watu wote.