Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma yetu iko mikoni mwetu na muskbali  wa kidijitali ni sasa: ITU

Mkutano wa Zama Zijazo unalenga kupanga njia iliyo na usawa zaidi kwa vizazi vijavyo.
© Unsplash/Ben White Mkutano wa Zama Zijazo unalenga kupanga njia iliyo na usawa zaidi kwa vizazi vijavyo.

Hatma yetu iko mikoni mwetu na muskbali  wa kidijitali ni sasa: ITU

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ITU, Doreen Bogdan-Martin amesema, "Hatima yetu iko mikononi mwetu  na mustakabali wa kidijitali ni sasa."

Ameyasema hayo katika Mkutano wa Zama Zijazo, kwenye mjdala uliobeba  maudhui “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja wa Kidijitali: Kuimarisha Ubunifu Shirikishi na Ushirikiano ili Kupunguza Mgawanyiko wa Kidijitali' yalifanyika katika Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa  jijini New Yorkm Marekani.

Akiwa mwenyeji wa mazungumzo hayo, Rais wa Estonia Alar Karis amesema, "Tunaamini katika manufaa ya kuunda vitu kwa Pamoja, kurejeleza na kuendeleza suluhu zilizopo tayari ili kuokoa rasilimali na kuzuia kurudiwa. Hii inapaswa kuwa kanuni yetu ya kawaida ya mwongozo, ili kuziba migawanyiko haraka.”

Pia amesema, "Mashirikika ya wadau  na ushirikiano, ndani ya nchi na kimataifa, ni msingi wa jamii ya wazi ya kidigitali. Ushirikiano ni muhimu, kukusanya rasilimali na kushiriki katika kujenga uwezo, ndiyo njia ya haraka zaidi ya kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma, hasa katika nchi zinazoendelea.”

Wasichana huko Maldives wanashirikiana kwenye mradi.
© UNICEF/Maldives Wasichana huko Maldives wanashirikiana kwenye mradi.

Pengo la kidijitali ni kikwazo cha maendeleo

Mwenyeji mwenza wa majadiliano hayo Mohamed Muizzu, Rais wa Jamhuri ya Maldives, amesisitiza,kwamba  “Mgawanyiko huu wa kidijitali sio tu kuhusu ufikiaji wa mtandao, ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo, fursa na haki."

Doreen Bogdan -Martin, Katibu Mkuu wa ITU ameongeza kuwa "Katika ulimwengu huu, suluhu za kidijitali zinazobadilisha mwelekeo zinaweza kusongesha asilimia 70 ya malengo yote ya maedeleo endelevu, SDG. “

Lakini pia amesema kwa sasa tuna ulimwengu ambapo watu bilioni 2.6 bado hawako mtandaoni duniani kote.

Amehitimisha kwa kusema "Tunakimbizana na wakati. Hebu tulinganishe ujumuishaji wa kidijitali na kasi ya mabadiliko ya kidijitali. Wacha tusawazishe udhibiti na uvumbuzi. Na tumpe kila mtu kiti na sauti kwenye meza ya mazungumzo. Hili ni jaribu lililo mbele yetu, bado ni mtihani wetu mkuu! Hatima yetu iko mikononi mwetu na mustakabali wa kidijitali ni sasa.”