Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yafanya uhamishaji mkubwa zaidi wa wagonjwa Gaza

Mwanamke Mpalestina na msichana mdogo wameketi pamoja ndani ya gari la wagonjwa. Mwanamke huyo amemshikilia mtoto, ambaye amevaa kifuniko cheupe cha kichwa.
© WHO Wagonjwa waliohamishiwa hospitalini kusini mwa Gaza na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (Maktaba))

WHO yafanya uhamishaji mkubwa zaidi wa wagonjwa Gaza

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na wadau wake, jana Septemba 11 huko Gaza wamefanikiwa kuhamisha wagonjwa 97 na watu wengine 155 wenye majeraha makubwa zaidi.

Katika unaotajwa kuwa uhamishaji mkubwa wa wagonjwa tangu ule wa Oktoba 2023 wagonjwa walisafirishwa kupitia Kerem Shalom hadi Uwanja wa Ndege wa Ramon nchini Israel kwa safari ya kuelekea Abu Dhabi, Falme za Kiarabu. Wagonjwa walijumuisha waliokuwa na saratani, magonjwa ya moyo na mishipa, magonjwa ya damu na ini na majeraha.

Licha ya changamoto kali za uendeshaji na ukosefu wa usalama, WHO na wadau wake walihakikisha uhamisho wa wagonjwa na kuweka kituo cha kupokea wagonjwa katika Hospitali ya inayosimamiwa na Ulaya huko Gaza ambapo wagonjwa walikusanyika kabla ya kuondoka.

“Operesheni hii ngumu sana ilikamilishwa chini ya shinikizo kubwa la musa kuwaleta pamoja wagonjwa wote.” Imesema taarifa ya WHO iliyosambazwa jana.

Aidha safari nyingine maalum kuelekea kaskazini ilifanywa ili kuhakikisha wagonjwa 8 na wenzao 12 wanahamishwa kutoka mji wa Gaza hadi katika Hospitali ya inayosimamiwa na Ulaya hapo Gaza  kwa wakati ufaao kwa ajili ya kuhamishwa, pamoja na kupeleka mafuta kwa ajili ya chanjo ya polio inayoendelea.