UN yakaribisha kufunguliwa mpaka wa Adre kati ya Chad na Sudan ili kunusuru waathirika wa vita
Amani na Usalama
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WHO leo limekaribisha taarifa kwamba kivuko cha Adre mpakani mwa Chad na Sudan kitafunguliwa likisema ni habari njema kwani lilikuwa likikimbizana na muda ili kuokoa maisha ya mmaelfu ya watu walioathirika na vita nchini Sudan.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Nairobi
Leni Kinzli mkuu wa wa mawasiliano wa WFP nchini Sudan amesema , “Nchini kote, WFP imekuwa ikiongeza msaada kwa maeneo 14 ama yenye njaa au yenye hatari ya njaa, ambayo kwa kiasi kikubwa yanapatikana Darfur, Kordofan, Khartoum na Gezira, kwa lengo la kusaidia hadi watu milioni 8.4 ifikapo mwisho wa mwaka.”
WFP imekuwa ikihamasisha kusafirishwa mara moja kwa vifaa muhimu vya chakula na lishe kupitia ukanda wa Adre katika wiki zijazo.
Kinzli ameongwza kuwa “Malori yalilazimika kuvuka mpaka huu kila siku ili kupata mtiririko thabiti wa misaada katika eneo hilo. Hivi sasa, misafara miwili, yenye takriban tani 6,000 za chakula na lishe kwa ajili ya watu wapatao nusu milioni zinapakiwa, zikilengwa katika maeneo yenye hatari ya njaa katika majimbo ya Darfur Kaskazini, Kati na Magharibi mara tu baada ya mawasiliano rasmi ya serikali na vibali kupokelewa.”
Wakimbizi wa Sudan wakiishi katika mahema katika mji wa mpakani na Chad wa Andre
Hatua hii imekuja wakati muafaka
Kwa mujibu wa WFP hatua hii imekuja wakati muafaka kwani kivuko kingine cha mpaka kutoka Chad hadi Darfur kupitia Tine kilikuwa hakipitiki kwa kiasi kikubwa kutokana na mvua kubwa, ambapo karibu malori 30 yaliyojaa msaada wa WFP hayakuweza kuvuka mto uliofurika kwa msimu kwa takriban mwezi mmoja.
‘Nchini Sudan, matumaini kidogo ambayo Wasudan walikuwa wameshikilia baada ya miezi 16 ya vita yalikuwa yakisombwa na mvua kubwa na mafuriko. Msimu wa mvua ulikuwa ukizidisha hali mbaya ya uhakika wa chakula nchini Sudan. Mafuriko yamelazimisha watu zaidi kukimbia kwa nyumba zao, kuongeza mahitaji ya kibinadamu, na kukataza jamii kupata usaidizi muhimu. Pia mvua imeharibu madaraja muhimu na kuifanya kuwa vigumu sana kwa misafara ya misaada kupita kwenye barabara zenye matope, zilizofurika.”
Bi. Kinzli amesisitiza kuwa ni wakati wa wahusika wote, haswa wahusika katika mzozo, kuja pamoja na kuchukua hatua kwa maslahi ya watu wa Sudan.
Wakimbizi wa Sudan wakisubiri kupokea chakula huko Adre, karibu na mpaka wa Chad na Sudan.
Mazungumzo ya Sudan Geneva
Amesema mazungumzo ya amani yanayoendelea Geneva yanatoa fursa muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kushughulikia changamoto zilizoenea za kiutendaji na vikwazo vya kufikia moja kwa moja na pande zinazozozana zinazozuia utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Kinzli amesisitiza kuwa “likuwa muhimu kwa pande zinazopigana kuondoka kwenye uwanja wa vita na kujitokeza kwenye meza ya mazungumzo, ili chakula kiweze kuhamia kwa jamii zilizokumbwa na njaa nchini kote kwa wakati na kabla hatujachelewa.”
Ameongeza kuwa “Mazungumzo ya Geneva yalilenga kutatua baadhi ya changamoto za kibinadamu zinazojitokeza sana. Sudan imekuwa janga kubwa zaidi la njaa duniani, na asilimia 54 ya watu hawawezii kula chakula cha kutosha kila siku. Watu 755,000 sasa wako katika kiwango cha juu zaidi cha uhaba wa chakula.”
WFP imeweka chakula cha msaada nchini Chad tayari kwa kukisambaza Darfur mji ambao eneo lake lina una ukubwa wa nchi ya Hispania, amesema na ndani ya Darfur kuna maeneo kadhaa makubwa ambayo yalikuwa katika hatari ya baa la njaa na kwa sasa Barabara nyingi hazipitiki kwa sababu ya mvua.
Mtoto nchini Sudaa akipokea lishe ya karanga kwa ajili ya matibabu ya utapiamlo
Kivuko cha Adre ni muhimu kwa huduma za afya: WHO
Akiunga mmkono umuhimu wa kufunguliwa kivuko cha Adre Margaret Harris, kutoka shirika la Afya Duniani WHO amesema “Bila fursa ya kuwafikia waathirika, hakuna msaada ungeweza kutolewa. Utapiamlo unaweza kuwa na madhara makubwa sana kiafya, hii ni hatari hasa kwa watoto. Upatikanaji wa huduma za afya pia ulikuwa na kikwazo sana kwa sababu ya ukosefu wa usalama, kulikuwa na uhaba wa dawa na vifaa, na wahudumu wa afya walikuwa hawalipwi. Watu walikuwa wakifa kutokana na ukosefu wa upatikanaji wa dawa za msingi.”
Kulikuwa na ripoti nyingi za mlipuko wa kipindupindu, homa ya dengue, surua, uti wa mgongo, na magonjwa mengine.
Watu wanaokimbia ghasia wanapitia Kituo cha muda huko Renk kaskazini mwa Sudan Kusini
Wakimbizi hawajaongezeka sana: UNHCR
Olga Sarrado, kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, amebainisha kuwa UNHCR haijaona ongezeko la wanaowasili kutoka Sudan kuingiaChad, ambayo bado imekuwa ikipokea karibu wakimbizi 1,300 wanaowasili kwa siku.
Watu waliokuwa wakivuka na kuingia Chad wamesema walikuwa wakikimbia njaa.
Watu hao walikuwa wakiishi katika maeneo yenye migogoro kwa zaidi ya mwaka mmoja, jambo ambalo lilikuwa limewazuia kwa kiasi kikubwa kupata riziki na msaada wa kibinadamu.
UNHCR imekaribisha kufunguliwa kwa kivuko cha Adre, na baadhi ya malori yake yalikuwa yakihamia Adre.
Shirika hilo linasema fursa ya kuendelea kuvuka mpaka na harakati zisizozuiliwa za misaada ndani ya Darfur zinahitajika.