Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa 85 wafanikiwa kutolewa Gaza kwenda kupatiwa matibabu UAE

Msichana mdogo aliyevaa gauni la waridi ameketi kwenye kitanda cha hospitali akiwa amevaa sasti na kifaa cha fremu ya chuma mguuni, baada ya kuhamishwa kutoka Gaza.
WHO Msichana aliyejeruhiwa vibaya amehamishwa kutoka Gaza kuelekea UAE

Wagonjwa 85 wafanikiwa kutolewa Gaza kwenda kupatiwa matibabu UAE

Afya

Tangu kuanza kwa mzozo huko Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba mwaka jana 2023 baina ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas mzozo ambao umesababisha vifo vingi, majeruhi, watu kupoteza kila kitu na wengine kutekwa, mwishoni mwa mwezi Julai, 2024 Ukanda huo umeshuhudia uhamisho mkubwa zaidi wa wagonjwa ambao wamepelekwa kupatiwa matibabu nje ya nchi.

Jumla ya wagonjwa na majeruhi walio mahututi 85 wamefanikiwa kuondolewa kutoka Ukanda wa Gaza kwenda Abu Dhambi katika Falme za kiarabu katika operesheni iliyotajwa kuwa “ngumu sana” iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO wakishirikiana na serikali ya Falme za kiarabu UAE pamoja na wadau wengine.

Wafanyakazi wa matibabu katika hema la hospitali ya shambani huko Rafah, Gaza, wakiwahudumia wagonjwa na watoto.
WFP Hospitali ya Kimataifa ya Kikosi cha Medical Corps huko Rafah, Gaza

Operesheni hiyo ilifanyikaje?

Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO ilianza kwa kuonesha mandhari ya hospitali ya madaktari wasio na mipaka wa Ubelgiji iliyoko katika kambi ya Al Zawaida huko Gaza, kundi kubwa la watu wanaonekana wakijadili kitu na Daktari bingwa wa upasuaji ambaye pia ni afisa wa dharura wa WHO Dkt. 

Athanasios Gargavanis akaeleza kwa kifupi kuwa tumefanikiwa kukusanya vitambulisho vya wagonjwa na wanawauguza na vilevile huduma muhimu ambazo zitawafanya wasafiri kwa usalama na wanafanya haya yote ili kuhakikisha wanafika UAE salama ili waweze kuendelea na matibabu.

Daktari Murad Abed ni daktari wa kiwewe wa WHO akaeleza kwa kifupi kuhusu wagonjwa walio kituoni hapa huku akiwa amesimama na watoto wawili waliokatwa viungo vya miguu. “Sara na Amir, tulifanikiwa kuwahamisha kutoka Kaskazini mwa Gaza mpaka kusini ili kutafuta fursa ya kuwasafirisha kuwapeleka nje ya nchi. Hatimaye, baada ya miezi mitatu ya kusubiri kufaa ya kwenda nje ya nchi, tunamatumaini tutafanikiwa kuhasafirisha kesho asubuhi kupitia kivuko cha Kerem Shalom kwenda UAE.”

Mtoto mdogo wa Kipalestina mwenye mguu uliokatwa ameketi kwenye kiti katika hospitali ya uwanja huko Gaza, akiwa amevaa kifaa cha matibabu kwenye kiungo chake kilichobaki. Mtoto mwingine aliyejeruhiwa anakaa kitandani nyuma.
© WHO/Christopher Black Watoto wanatibiwa katika hospitali ya muda huko Mouraj, kitongoji kilichoko kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Watoto Amir Marzouk na Sa Marzouk waanaeleza furaha waliyokuwa nayo

Amir Marzouk “Ninafuraha sana kwamba ninasafiri kwenda kupata matibabu, nakwenda kuwekewa viungo vya bandia na nitaweza tena kuwa nakimbia kila mahali.”

Sara Marzouk Nilipata majeruhi nikiwa Gaza, nilikwenda hospitali kupata matibabu na WHO ikanileta hapa ili niweze kusafiri nje ya nchi. Namshukuru Mungu baada ya kusubiri kwa muda mrefu, tutasafiri kesho.”

Hatimaye, machweo na msafara wa mabusi unaonekana ukiwasili katika kambi ya Al Zawaida.

Na kesho yake kabla ya jua kuchomoza video ya WHO inaonesha shughuli ya watu kuingia kwenye mabus hayo ikianza ikisimamiwa vyema na ukaguzi wa majina kabla ya watu kupanda kwenye mabus hayo.

Wagonjwa wasiojiweza wakiwa kwenye machela walibebwa na kuingizwa kwenye mabus tayari kuanza safari ya kuelekea katika kituo cha Kerem Shalom.

Wafanyakazi wa matibabu waliovaa vitambaa vya bluu humsafirisha mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati katika kifaa cha kuangulia mtoto mchanga kwenye machela ndani ya korido ya hospitali.
© UNICEF/Eyad El Baba Watoto wakihahamishwa kutoka hospitali ya Al-Shifa huko Kaskazini mwa Gaza kuelekea eneo la Kusini mwa ukanda huo wa Gaza huko Mashariki ya Kati kutokana na mapigano yanayoendelea hivi sasa kati ya Israel na wapiganaji wa kipalestina wa Hamas

Safari imeiva

Safari inaanza, ndani ya mabasi ni nyuso zenye furaha, amahakika safari imewadia, safarini ya kuelekea UAE.

Upande wa pili huko Jerusalem Mashariki video inaonesha ni usiku totoro, wafanyakazi wa WHO wanaonekana wakishughulika kuweka vifurushi kwenye mabus na viti vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa.

Tariq Al Shwaiki, ni afisa Uendeshaji, Usaidizi na Usafirishaji wa WHO na anasema “Saa hizi ni saa 9 usiku, na tuko hapa katika Hospitali ya Augusta Victoria, tunatayarisha mabasi yatakayoelekea kwenye kivuko cha Kerem Shalom. Tunasaidia na kusafirisha wagonjwa na kuhakikisha mabasi yamepakia chakula, maji, viti vya magurudumu na timu ya matibabu. Na watakuwa wakielekea uwanja wa ndege baada ya kupitia ukaguzi wa usalama na safari yao itaishia Abu Dhabi kupata matibabu.”

Msafara kutoka Gaza uliwasili kituo cha Kerem Shalom, watu wote walishushwa kwenye mabus na baada ya ukaguzi wakapanda mabus yaliyotoka Jerusalem Mashariki wakiwa na msafara wa WHO walielekea uwanja wa ndege wa Ramon huko Israel na kupanda ndege kuanza safari ya kuelekea Abu Dhabi katika Falme za Kiarabu.