Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake na watoto wasaka hifadhi UN Maimoya DRC kufuatia operesheni ya kijeshi

Doria ya pamoja kati ya jeshi la serikali ya DRC, FARDC na MONUSCO huko jimboni Kivu Kaskazini.
MONUSCO/Alain Wandimoyi
Doria ya pamoja kati ya jeshi la serikali ya DRC, FARDC na MONUSCO huko jimboni Kivu Kaskazini.

Wanawake na watoto wasaka hifadhi UN Maimoya DRC kufuatia operesheni ya kijeshi

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO,  leo umesema idadi kubwa ya wanawke na watoto wamekimbilia kwenye kituo cha MONUSCO kilichoko Maimoya , Kijiji kilicho karibu na mji wa Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa mpango huo wa Umoja wa Mataifa nchini Congo ni kufuatia operesheni ya kijeshi inayoendelea ambayo ni ya Pamoja ya MONUSCO na jeshi la serikali ya DRC ya kuyafurusha makundi ya waasi yenye silaha likiwemo kundi la Allied Democratic Forces ADF. 

Walindamani wa MONUSCO wameongeza doria katika eno hilo na watu taratibu wameanza kurejea makwao.