Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa kidijitali ni lulu lakini pia unaathari za kimazingira hasa kwa nchi zinazoendelea: UNCTAD

Mfanyikazi wa taka za kielektroniki anakagua taka hizo nchini Ghana.
© WHO/Abraham Thiga Mwaura
Mfanyikazi wa taka za kielektroniki anakagua taka hizo nchini Ghana.

Uchumi wa kidijitali ni lulu lakini pia unaathari za kimazingira hasa kwa nchi zinazoendelea: UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu “Uchumi wa kidijitali 2024” imeweka bayana kuhusu athari za kimazingira za sekta ya kimataifa ya kidijitali na mzigo mkubwa wa athari hizo unaobebwa na nchi zinazoendelea.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mjini Geneva Uswisi imetanabaisha kwamba kuanzia kwa uchimbaji wa malighafi na matumizi ya teknolojia za kidijiti hadi uzalishaji taka, inachunguza asili na ukubwa wa athari za kimazingira za sekta hii.

Kinachoonekana karika ripotihiyo ni kwamba nchi zinazoendelea zinateseka kupita kiasi kutokana na athari mbaya za mazingira za uwepo na ukuaji wa sekta ya kidijitali, huku zikikosa fursa za maendeleo ya kiuchumi kutokana na pengo kubwa la kidijitali.”

Ripoti hii ya kina inaangazia kwamba ingawa uboreshaji wa kidijitali huchochea ukuaji wa uchumi duniani na kutoa fursa za kipekee kwa nchi zinazoendelea, athari zake za kimazingira zinazidi kuwa kubwa na mbaya.

Imesisitiza kuwa Nchi zinazoendelea zimesalia kuathiriwa kwa njia isiyo sawa kiuchumi na ikolojia kutokana na pengo liliopo la kidijitali na maendeleo lakini zina uwezo wa kutumia fursa ya mabadiliko haya ya kidijitali ili kukuza maendeleo.

Lazima tuwe na sera madhubuti

Katibu Mkuu wa UNCTAT Rebeca Grynspan, amesema “Kuhusu athari za Uchumi wa kidijitali ni lazima tujumuishe masuala ya mmazingira katika sera za kidijitali. Tukumbtie Uchumi wa mzunguko, tutoe kipaumbele katika ujerejelezaji wa bidhaa, utumiaji tena wa bidhaa za kidijitali, kutekeleza mikakati ya matumizi ikiwemo mufa wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki tunavyotumia.”

Amesisisitiza kuwa “Kuna haja ya kuwa na mtazamo wenye uwiano, ni lazima tukumbatie nguvu ya kidijitli ili kusongesha ujumuishaji na maendeleo endelevu huku tukikabiliana na athari za kimazingira za sekta hiyo hasa kwa kubadili mwelekeo na kuwa na Uchumi wa kidijitali wa mzunguko ukijumuisha uwajibikaji wa matumizi na uzalishhaji, matumizi ya nishati jadidifu na udhibiti wa taka za kielektroniki kwani athari za kimazingiza zinaweza kudhibitiwa.”

Ripoti hiyo pia inasisitiza haja kubwa ya kushughulikia gharama za kimazingira za mabadiliko ya haraka ya kidijitali.

Hofu katika ukuaji  wa uchumi wa kidijitali

Wasiwasi mkubwa ni pamoja na kupungua kwa malighafi za teknolojia ya kidijitali na matumizi madogo ya hewa ukaa, kuongezeka kwa matumizi ya maji na nishati na suala linalokua la taka zinaohusiana na masuala ya  kidijitali.

Kadiri uboreshaji wa kidijitali unavyoendelea kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kuelewa uhusiano wake na uendelevu wa mazingira kunazidi kuwa muhimu

UNCTAD inatoa wito wa kuwepo kwa sera za kimataifa zinazohusisha wadau wote kuwezesha uchumi wa kidijitali wa mzunguko zaidi na kupunguza athari za kimazingira kutokana na mfumo wa kidijitali, huku zikihakikisha matokeo ya maendeleo jumuishi.