Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya miezi tisa ya vita Gaza, shule nyingine ya UN yashambuliwa na Israel

Takriban shule 190 na mijengo mengine inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, vimeharibiwa vibaya katika mashambulizi ya anga ya Israel tangu vita vilipozuka tarehe 7 Oktoba.
© UNRWA/Mohammed Hinnawi
Takriban shule 190 na mijengo mengine inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, vimeharibiwa vibaya katika mashambulizi ya anga ya Israel tangu vita vilipozuka tarehe 7 Oktoba.

Baada ya miezi tisa ya vita Gaza, shule nyingine ya UN yashambuliwa na Israel

Amani na Usalama

Vita huko Gaza jana jumapili vimetimiza miezi tisa tangu uzuka huku wahudumu wa kibinadamu wakiachwa kutathmini uharibifu wa shambulio jipya la anga la Israeli kwenye shule ya Umoja wa Mataifa.

"Siku nyingine. Mwezi mwingine. Shule nyingine imegongwa na shambulizi la anga," amesema Philippe Lazzarini, mkuu wa , shirika kubwa zaidi la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina  huko Gaza UNRWA, katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani Twitter, baada ya shule huko Nuseirat, katikati mwa Gaza, "kupigwa kombora na vikosi vya Israeli siku ya Jumamosi.”

Shule hiyo UNRWA inasema ilikuwa nyumbani kwa karibu watu 2,000 waliofurushwa kwa nguvu kutokana na uhasama huo unaoendelea Gaza, amesema Kamishna Mkuu huyo wa akiongeza kuwa makumi ya majeruhi wameripotiwa katika shambulio hilo.

Hatua hiyo inakuja wakati mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka yaliripotiwa kutarajiwa kuanza tena katika siku zijazo.

Jitihada za mara kwa mara za awali za kupata mafanikio zimeanzishwa, licha ya shinikizo endelevu la kimataifa kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zenye ushawishi kwa pande zote mbili.

Kwa mujibu wa UNRWA mafanikio katika mazungumzo ya wiki hii yatategemea kukidhi wito wa Hamas wa kukomesha kabisa mapigano na mashambulizi makali ya anga ya Israel ambayo yamesambaratisha maeneo makubwa ya Ukanda wa Gaza, na lengo la vita la serikali ya Israel la kuharibu uwezo wa kijeshi wa Hamas baada ya kundi hilo kushambulia maeneo mengi Kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana na kuua karibu watu 1,250 na kuwakamata mateka zaidi ya watu 250.

Macho yote yako kwenye mpaka wa Lebanon na Israel

Hadi sasa, makumi ya maelfu ya Wapalestina wameuawa, kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Gaza na takwimu za hivi karibuni kutoka UNRWA zinaonyesha kuwa takriban watu 520 waliokuwa wakihifadhiwa katika makaazi ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa wameuawa na takriban 1,602 kujeruhiwa tangu kuanza kwa vita.

Katika taarifa ya hali ya kawaida, ofisi ya kuratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa, OCHA imesema kwamba hadi watu milioni 1.9 huko Gaza wamefurushwa na vita, ikiwa ni pamoja na wengine waliokimbia "mara tisa au mara 10".

Makadirio ya hapo awali yalikuwa watu milioni 1.7 lakini hii ilikuwa kabla ya operesheni ya Israeli huko Rafah mapema mwezi Mei, ambayo ilisababisha watu wengine kuhama kutoka Rafah na maeneo mengine katika Ukanda wa Gaza. Msukumo mpya wa kumalizika kwa vita unakuja huku kukiwa na majibizano ya kila siku ya mapigano kati ya wanamgambo wa Lebanon na Israel na mshirika mkuu wa Hamas, Hezbollah, katika mstari wa Blue unaofuatiliwa na Umoja wa Mataifa ambao unawatenganisha nchi hizo.

Jana Jumapili, kundi hilo lenye makao yake makuu nchini Lebanon lilidai kuhusika na shambulio lililoripotiwa na ndege zisizo na rubani kwenye mlima Hermoni katika Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa na Israel.

Hezbollah imesema kwamba itasimamisha operesheni tu wakati vita huko Gaza vitakapomalizika.

"Kupanuka kwa taratibu kwa wigo na ukubwa wa makabiliano zaidi kwenye msitari wa Blue kwa kiasi kikubwa kunaongeza hatari ya kukokotwa na kuzorota zaidi kwa hali ambayo tayari inatisha," Ujumbe wa Muda wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL umeiambia UN News, kabla ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa mvutano.

Ukitaja takwimu za hivi karibuni za OCHA, ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umesema kuwa karibu watu 97,000 wamekimbia makazi yao kutoka kusini mwa Lebanon kwa sababu ya uhasama unaoendelea kufikia tarehe 25 Juni, zaidi ya majeruhi 1,800 wameripotiwa ikiwa ni pamoja na vifo 435 kati yao 97 walikuwa ni raia.

"Suluhu ya kisiasa na kidiplomasia ndilo suluhu pekee inayowezekana na ya muda mrefu," ilimesisitiza shirika la OCHA.

Uchunguzi unaendelea

Akizungumzia shambulio hio dhii ya shule na madai ya jeshi la Israel kwamba ilikuwa inatumiwa na makundi yenye silaha ya Palestina, mkuu wa UNRWA Bwana Lazzarini amesema kwamba ameyachukulia madai hayo kwa uzito mkubwa.

"Ndio maana nimekuwa nikiitisha mara kwa mara uchunguzi huru ili kubaini ukweli na kubaini wale waliohusika na mashambulizi dhidi ya majengo ya Umoja wa Mataifa au matumizi yake mabaya ," amesema akimaanisha uchunguzi unaoendelea wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu madai ya Israel kwamba wafanyakazi 12 wa UNRWA walihusika katika mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyoongozwa na Hamas.

Wafanyakazi wanane wa UNRWA bado wanachunguzwa na hadi sasa, zimeahirishwa kesi nyingine tatu ikitoa ushahidi wa kutosha kutoka kwa mamlaka ya Israel na kufunga kesi moja kwa sababu Israel ilikuwa haijatoa ushahidi wowote.

Miezi tisa kwenye vita hivi vya kikatili, natoa wito kwa mara nyingine kusitishwa kwa mapigano ambayo watu wa Gaza na Israel hatimaye watapata ahueni na ulinzi na mateka wote wangeachiliwa mara moja,” amesema Lazzarini.

Ameongeza kuwa "Vita hivi vikiendelea kwa muda mrefu, ndivyo mpasuko unavyozidi kuwa mkubwa, na watu wanaovulia ndivyo watakavyoendelea kuteseka zaidi.”