Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wavumbuzi wa Uchina Wanajaza Hati miliki Nyingi zaidi za akili mnemba (GenAI) kulingana na takwimu za WIPO

Utafiti wabaini kuwa ajira na viwanda vingi kunufaika na Akili Mnemba lakini ajira kama za ukarani zitachukuliwa na Akili Mnemba kwa kiasi fulani.
© Unsplash/Steve Johnson Utafiti wabaini kuwa ajira na viwanda vingi kunufaika na Akili Mnemba lakini ajira kama za ukarani zitachukuliwa na Akili Mnemba kwa kiasi fulani.

Wavumbuzi wa Uchina Wanajaza Hati miliki Nyingi zaidi za akili mnemba (GenAI) kulingana na takwimu za WIPO

Ukuaji wa Kiuchumi

Wavumbuzi wa Uchina wanawasilisha idadi kubwa zaidi ya hati miliki za akili mnemba (GenAI), wakipita kwa umbali wavumbuzi nchini Marekani, Jamhuri ya Korea, Japani na India ambao wanajumuisha maeneo mengine matano bora, kwa mujibu wa ripoti mpya ya WIPO iliochapishwa tarehe 3,2024.

Ripoti hii ya  WIPO Patent Landscape Report on Generative AI imerekodi uvumbuzi 54,000 wa akili mnemba katika muongo hadi 2023, huku zaidi ya 25% yao ikiibuka katika mwaka wa huo huo.

Akili mnemba inaruhusu watumiaji kuunda maudhui ikiwa ni pamoja na maandishi, picha, muziki na msimbo wa kompyuta. Hii inawezesha bidhaa mbalimbali za viwandani na za watumiaji ikiwa ni pamoja na programu zenye uwezo wa kiteknolojia wa kuwasiliana kwa njia ya maneno (chatbots) kama vile ChatGPT, Google Gemini au ERNIE ya Baidu.

Kati ya 2014-2023, zaidi ya uvumbuzi 38,000 wa akili mnemba ulitoka Uchina, ambao ni mara sita zaidi ya Amerika iliyoshika nafasi ya pili. India, ambayo ni eneo la tano kwa ukubwa kwa uvumbuzi wa akili mnemba,ilipata (56%) kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa kila mwaka kati ya viongozi watano wa juu. Kwa mujibu waripoti hii, akili mnemba tayari inaenea katika tasnia zote ikijumuisha sayansi ya maisha, viwanda, usafirishaji, usalama na mawasiliano ya simu.

Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Daren Tang, anasema "akili mnemba imeibuka kama teknolojia inayoweza kubadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kuishi na kucheza. Kupitia kuchanganua mitindo ya hati miliki na takwimu, WIPO inatumai kumpa kila mtu ufahamu bora zaidi wa wapi teknolojia hii inayokua kwa haraka inatengenezwa, na inakoelekea. Hii inaweza kusaidia watunga sera kuchagiza maendeleo ya akili mnemba kwa manufaa yetu sote na kuhakikisha kuwa tunaendelea kumfikiria binadamu wakati wa uvumbuzi na mifumo yetu bunifu ya ikolojia. Tuna imani kwamba ripoti hiyo itawawezesha wavumbuzi, watafiti na wengine kuabiri mandhari ya akili mnemba inayobadilika kwa kasi na athari zake kwa ulimwengu,”