Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shamrashamra za siku ya Kiswahili duniani zafanyika leo makao makuu ya UN New York

Maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika.
UN News
Maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika.

Shamrashamra za siku ya Kiswahili duniani zafanyika leo makao makuu ya UN New York

Utamaduni na Elimu

Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.

Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili.

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga akizungumza katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga akizungumza katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Sherehe hizi zimeandaliwa kwa pamoja na uwakilishi wa kudumu wa  Tanzania, Kenya, Qatar na Oman kwenye Umoja wa Mataifa pamoja na kundi la nchi za Afrika kwenye Umoja wa Mataifa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.

Maadhimisho haya yanafanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa siku mbili tu baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha Azimio la kutambua tarehe 7 Julai kuwa siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili, ambapo awali ilikuwa inatambuliwa na UNESCO pekee.

Viongozi wa nchi kuhutubia

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na waandaaji, tukio hilo la maadhimisho kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa litahusisha mijadala, tumbuizo za kitamaduni na hotuba kutoka kwa viongozi akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa TAnzania, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mshindo watuzo ya Nobel Profesa Abdulrazak Gurnah,. 

Kwa watakaozungumza kiingereza kutakuweko na tafsiri ya papo kwa papo kwa lugha ya Kiswahili. Maadhimisho yatarushwa mubashara  na televisheniya mtandao ya Umoja wa Mataifa. 

Maadhimisho ya tatu ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa
Maadhimisho ya tatu ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mambo yanayoangaziwa

Maadhimisho haya yatapatia msisitizo umuhimu wa kujenga mifumo ya elimu yenye mnepo kwa kutumia utajiri uliomo kwenye utamaduni wa lugha ya Kiswahili.

Washiriki watafanya hivyo wakimulika masuala ya msingi kama vile

  • Kwa nini elimu ya sanaa ni muhimu na ni kwa vipi inaweza kusaidia kuendeleza lugha ya Kiswahili?
  • Hali ya sasa ya ujumuishaji wa elimu ya sanaa kwenye nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili. Je inawezaje kuimarishwa zaidi ili kukuza utambulisho wa kitamaduni wa Kiswahili na urithi?
  • Ni changamoto zipi na mahitaji yapi yanahusiana na kujumuisha elimu ya sanaa ya kiswahili katika mitaala ya shule. Je ni manufaa yapi yamebainika kwa ujumuishaji wa aina hiyo?
  • Ni kwa vipi wasanii na wabobezi wa utamaduni wanaweza kuchangia kwenye kuendeleza na kuhifadhi lugha ya kiswahli, na ni dhima ipi wanayo katika kukuza ubunifu na kuimarisha utofauti wa kujieleza kitamaduni?
  • Mshiriki kijana kwenye maadhimisho ya pili ya siku ya kiswahili duniani mwaka 2023.
    UN /Manuel Elias
    Mshiriki kijana kwenye maadhimisho ya pili ya siku ya kiswahili duniani mwaka 2023.

Mwezi Novemba mwaka 2021, UNESCO kupitia azimio namba 41 C/53 ilitangaza Julai 7 kuwa siku ya Kiswahili duniani kwa kutambua mchango wa lugha hiyo katika kusongesha tamaduni tofauti, kujenga hamasa na kukuza mazungumzo baina ya staarabu mbali mbali.