Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasudan wako kwenye uwanja wa vita, hakuna mahali salama kwao

Martha Ama Akyaa Pobee, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN kwa ajili ya  Afrika katika Idara za Siasa na Masuala ya Ujenzi wa Amani na Operesheni za Amani akitoa taarifa kwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Sudan na Sudan Kusini. (Juni 18, 2024)
UN Photo/Manuel Elías
Martha Ama Akyaa Pobee, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN kwa ajili ya Afrika katika Idara za Siasa na Masuala ya Ujenzi wa Amani na Operesheni za Amani akitoa taarifa kwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Sudan na Sudan Kusini. (Juni 18, 2024)

Wasudan wako kwenye uwanja wa vita, hakuna mahali salama kwao

Amani na Usalama

Bila hatua za haraka, Sudan iko kwenye hatari ya kutumbukia katika ghasia zaidi za kikabila na kugawanyika hata zaidi. Hatari ya kutokea kwa migogoro bado iko juu, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika Martha Ama Akyaa Pobee amelieleza leo Juni 18 Baraza la Usalama jijini New York, Marekani.

Martha Ama Akyaa Pobee amewaeleza wajumbe kwamba, mapigano kati ya pande zinazopigana yanaendelea kupamba moto, “na kwa kweli yanaongezeka, katika maeneo mengine kadhaa ya Sudan, ikiwa ni pamoja na Khartoum, mikoa ya Kordofan, na Jimbo la Gezira."
 
Ameripoti kwamba kuanzia tarehe 16 Aprili hadi 9 Juni, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu iliandikisha takribani vifo vya raia 192 huko El Fasher. Tangu wakati huo, makumi ya raia zaidi, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wameripotiwa kuuawa.
 
Amesisitiza, "Wananchi wako kwenye uawanja wa mapambano. Hakuna mahali salama kwao.”
 
Bi. Pobee amesema, "kusitishwa kwa mapigano huko El Fasher kunahitajika sasa ili kuzuia ukatili zaidi, kulinda miundombinu muhimu, na kupunguza mateso ya raia. Inaweza na inapaswa pia kufungua njia ya kukomesha kwa kiwango kikubwa uhasama.”
 

OCHA

 
Naye Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Uchechemuzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na kuratibu masuala ya dharura, (OCHA) Edem Wosornu, amehutubia Baraza la Usalama na kusema, “tuko katika mbio dhidi ya wakati ili kuepusha hasara kubwa ya maisha katika mzozo huu wa ulinzi na usalama wa chakula ambao haujawahi kutokea nchini Sudan.”
 
Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Uchechemuzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na kuratibu masuala ya dharura, (OCHA) Edem Wosornu, akitoa maelezo kwa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Sudan na Sudan Kusini. (Juni 18, …
UN Photo/Manuel Elías
Bi. Wosornu amesisitiza, masuala matatu muhimu: kulinda raia na miundombinu wanayohitaji kwa ajili ya kuishi; kuhakikisha upatikanaji misaada usiozuiliwa, endelevu na uliopanuliwa kwa watu wenye uhitaji; na kuongeza fedha kwa ajili ya uendeshaji wa misaada. “Lakini napenda kuwa wazi. Suala la mwisho ni mzozo huu wa kutisha ukome.