Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UNICEF wa GEG umeokoa mustakbali wangu: Zainab

Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala, Uganda.
UNICEF
Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala, Uganda.

Mradi wa UNICEF wa GEG umeokoa mustakbali wangu: Zainab

Utamaduni na Elimu

Mradi wa Wasichana kuwawezesha wasichana wenzao GEG, ni mradi wa kwanza nchini Uganda wa ulinzi wa kijamii unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ushirikiano wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala kupitia ufadhili uliotolewa na serikali ya Ubelgiji ukiwalenga watoto wa kike na mustakbali wao. 

Mradi huo wa GEG unatekelezwa katika wilaya zote tano za Kampala na unahakikisha wasicha barubaru walio shuleni na nje ya shule wanakuwa na mabadiliko bora kutoka utotoni kuingia ukubwani kwa kupokea elimu, ushauri na mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wa kufikia malengo yao. Wengi walio katika mradi huu wamepitia changamoto lukuki na mfano halisi ni Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala.

“Siku moja nyanya yangu alipokea simu kutoka kijijini wakimwambia nahitajika kijijini. Na nilipowasili huko nilikuwa viroba vya sukari, mchele na kadhalika na nikamuuliza msichana niliyemkuta pale hivi vitu ni vya nani?  Kisha akaniambia haujui kwamba unaolewa? Nilikuwa na umri wa miaka 16 tu na walikuwa wananiambia mi ni mkubwa”

Familia ya Zainab ilipanga na kumuandalia ndoa bila ridhaa yake na baada ya kupokea mahari alilazimishwa kwenda kuishi na bwana na mambo yalikuwa mabaya anasema Zainab

Mwanaume huyo alitaka kulala nami kwa nguvu, alitaka kunibaka. Nilimwambia hapana nataka kurejea shuleni. Nilikuwa nalia kila siku , sikujua cha kufanya nilichanganyikiwa. Na hapo nikamkumbuka mshauri wangu aliniambia wakati wowote ukipata tatizo nipigie nitakusaidia. Basi nikampigia naye akampigia baba yangu sijui walichozungumza lakini baada ya siku moja, nilirejea Kampala nikarejea shuleni.”

Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala nchini Uganda, akiwa na wanafunzi wenzake baada ya kurejea shule.
UNICEF
Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala nchini Uganda, akiwa na wanafunzi wenzake baada ya kurejea shule.

Mshauri huyo ni kutoka mradi wa UNICEF wa GEG aliokoa Maisha ya Zainab ambaye baada ya kunusika ndoa ya utotoni na kubakwa ana matumaini ya muskabali wake

“Sasa niña furaha sana kwani nimekuwa shuleni na bado naendelea na shule. Nimemaliza darasa la saba, naenda sekondari na nitafaulu. Nataka kuwa mwanasheria niweze kupigania haki za watoto ili kusiwe na mtoto yoyote atakayelazimishwa kufanya asichotaka.”

Mradi wa GEG umegawanyika katika sehemu kuu tatu, mosi kuwawezesha wasichana kupitia mtandao wa washauri rika, pili kuwashirikisha wasichana kupitia elimu, mafunzo na kuwaelekeza kwa kupata msaada wa huduma na tatu kuwawezesha wasichana kutafuta fursa bora za maisha yao ya baadaye kupitia msaada mdogo wa fecha wanaopokea.