Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilani hatutowasahau waliouawa na manusura wa mauaji ya kimbari Rwanda: Guterres

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Tafakari ya Mauaji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yanafanyika mjini Geneva. (Maktaba)
UN Photo/Violaine Martin
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Tafakari ya Mauaji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yanafanyika mjini Geneva. (Maktaba)

Asilani hatutowasahau waliouawa na manusura wa mauaji ya kimbari Rwanda: Guterres

Haki za binadamu

Ikiwa leo ni miaka 30 tangu kutokea mauaji mbaya zaidi ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa waliopoteza maisha na wale walionusurika hawatosahaulika kamwe.

Kupitia ujumbe wake maalum kwa siku hii Antonio Guterres amekumbusha kwamba ’’Siku kama hii mwaka 1994 na karibu siku 100 zizlizofuta Watuts milioni moja watoto, wanawake na wanaume waliuawa na Wanyarwanda wenzao. Familia zilizigeuka familia zingine, marafiki wakawa maadui, na roho mbaya ya unyanyasaji wa makusudi na ya kikatili ililikumba taifa.”

Katika ujumbe huo Katibu Mkuu amesisitiza kwamba ’’Hatutawasahau wahanga wa mauaji haya ya kimbari. Wala hatutausahau kamwe ushujaa na uthabiti wa wale walionusurika, ambao ujasiri na utayari wao wa kusamehe unasalia kuwa chachu ya nuru na matumaini katikati ya sura hii ya giza katika historia ya mwanadamu.”

Kijana mwenye umri wa miaka 14 wa Kinyarwanda kutoka mji wa Nyamata,. Alipigwa picha mwaka 1994. Aliponea chupuchupu kuuawa  katika mauaji ya kimbari kwa kujificha katikati  ya maiti kwa siku mbili
UNICEF/UNI55086/Press
Kijana mwenye umri wa miaka 14 wa Kinyarwanda kutoka mji wa Nyamata,. Alipigwa picha mwaka 1994. Aliponea chupuchupu kuuawa katika mauaji ya kimbari kwa kujificha katikati ya maiti kwa siku mbili

Chuki ndio mzizi wa fitina

Guterres amesema katika kumbukumbu ya mwaka huu, tunajikumbusha kuhusu mzizi wa mauaji ya kimbai ambao ni chuki.

Ameongeza kuwa ’’Tunaweza kuchora mstari ulionyooka kati ya mauaji ya yasiyokuwa na maana ya Watutsi milioni moja pamoja na baadhi ya Wahutu na watu wengine waliopinga mauaji ya kimbari na miongo kadhaa ya kauli za chuki ziliyotangulia, zilizochochewa na mivutano ya kikabila na kivuli kirefu cha ukoloni.”

Ameendelea kusema leo, kote ulimwenguni, misukumo mibaya zaidi ya kibinadamu inaamshwa kwa mara nyingine tena na sauti za misimamo mikali, migawanyiko na chuki.

Amesisitiza kwamba ’’Kwa wale wanaotaka kutugawa, ni lazima tutoe ujumbe ulio wazi, usio na shaka na wa dharura kamwe haitotokea tena.”

Katika siku hii adhimu ya kumbukumbu Guterres ameitaka dunia na kila mtu, ’’Kuahidi kusimama pamoja dhidi ya aina zote za chuki na ubaguzi. Hebu tuhakikishe kwamba vitendo vilivyoanza Aprili 7, 1994 havisahauliki kamwe na havirudiwi tena popote.” 

Maudhui ya kumbukumbu ya mwaka huu ni "Kumbuka, shikamana, Ibuka upya.”