Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi ziziso na bahari zina changamoto kubwa za kibiashara na mawasiliano: UN

Wanaume wakipakua magunia ya vitunguu kutoka kwa lori huko Bamako, Mali, nchi inayoendelea isiyo na bandari. Ukosefu wao wa ufikiaji wa moja kwa moja kwa viungo muhimu vya biashara mara nyingi husababisha nchi zisizo na bandari kulipa gharama kubwa za us…
World Bank/Dominic Chavez
Wanaume wakipakua magunia ya vitunguu kutoka kwa lori huko Bamako, Mali, nchi inayoendelea isiyo na bandari. Ukosefu wao wa ufikiaji wa moja kwa moja kwa viungo muhimu vya biashara mara nyingi husababisha nchi zisizo na bandari kulipa gharama kubwa za usafiri na usafirishaji.

Nchi ziziso na bahari zina changamoto kubwa za kibiashara na mawasiliano: UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kamati ya Umoja wa Mataifa kwa ajili yan chi zisizo na bahari, LLDCs leo imekutana mjini  kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa ajili ya mkutano wa maandalizi wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea zisizo na bandari (LLDCs).

Mkutano huo umesema nchi hizo kwa kukosa fursa ya moja kwa moja ya kuwa na bahari  zinakabiliwa na vikwazo vikubwa vya kibiashara, mawasiliano na maendeleo. 

Umeongeza kuwa kwa kukosa bandari nchi hizo zinalazimika kutegenmea nchi nyingine kupitisha bidhaa zake na hivyo kuongeza gharama za biashara na ucheleweshwaji.  

Mkutano huu wa maandalizi unatoa fursa ya kusaka suluhu, ushirikiano na kushughulikia changamoto ili kuzifanya nchi hizo kuwa na mustakbali bora. 

LLDCs zina uwezo mkubwa wa kushamiri

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa licha ya changamoto kubwa zinazozikabili nchi hizo zisizo za bandari, nchi hizo zina jamii ambazo ni mahiri na uwezo mkubwa ambao haujatumiwa.

Rabab Fatima mwakilisi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mataifa yaliyo hatarini zaidi amesisitiza umuhimu wa kushikamana na mataifa hayo akisema “Hebu tutumie dhamira yetu ya pamoja ya kuleta mabadiliko ya mageuzi katika maisha ya watu milioni 570 wanaoishi katika nchi za LLDCs 32 ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.”

Kuna jumla yan chi 32 duniani zisizo na baharí au bandari duniani.

Mkutano wa tatu wa UN LLDCs3 Rwanda

Mkutano wa tatu wa kilele wa nchi zisizo na bandari LLDC3 mwaka huu utafanyika Kigali Rwanda kuanzia tarehe 18 hadi 21 Juni.

Umoja wa Mataifa unasema kwa sababu nchi za LLDCs, zinategemea zaidi majirani zao kushiriki katika biashara, usafiri na uwekezaji ushirikiano ni kila kitu.

Ndiyo maana Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa utashirikiana sana na vikundi tofauti, ambavyo kila kimoja kinawakilisha mitazamo tofauti na suluhu za kibunifu ili kusaidia kufungua uwezo wa nchi zinazoendelea zisizo na bandari.

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa “LLDC3 ni fursa ya hali ya juu kwa makundi haya kushirikiana na viongozi wa dunia, Wakuu wa Umoja wa Mataifa, Watendaji wakuu, viongozi wa ngazi za chini, wawekezaji, wawakilishi wa vijana na wadau wengine kuweka mikakati ya kukuza ujumuishaji wa masuala yasiyo na bandari katika uundaji wa sera za kimataifa, mipango ya uwekezaji na kuunda sera ya kimataifa na ajenda ya maendeleo endelevu kufikia SDGs.”