Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HABARI KWA UFUPI

Wajumbe wawasili katika mkutano wa COP28 kuhusu hatua za hali ya hewa.
© UNFCCC/Kiara Worth
Wajumbe wawasili katika mkutano wa COP28 kuhusu hatua za hali ya hewa.

HABARI KWA UFUPI

Tabianchi na mazingira

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 umefungua pazia rasmi mjini Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu kwa kuwaleta Pamoja wajumbe zaidi ya 60,000 kuangalia jinsi ya kuongeza hatua, fursa ya nyenzo za kujenga mnepo ikiwemo makubaliano ya kuanzishwa mfuko wa hasara na uharibifu ambayo yamepitishwa kwenye mkutano huo na pia kutumia ubunifu kudhibiti janga hilo.

Akizungumza katika ufunguzi sagini mkutano huo Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi Simon Stiell amewataka wajumbe wanaoshiriki COP28 kuharakisha hatua ya dhidi ya mabadiliko ya tabianchi akisema "Ikiwa hatutaonyesha ishara ya kupunguza matumizi ya mafuta kisukuku kama tujuavyo basi tunakaribisha kupungua kwetu. Na tunachagua kulipa gharama kwa maisha ya watu. 

Naye Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO Petteri Taalas amesema “Kiwango cha hewa ukaa kiko asilimia 50 juu ya ilivyokuwa kabla ya maendeleo ya viwanda na kuendelea kwa viwango hivyo vya gesi chafuzi inamaanisha kuendelea kwa ongezeko la joto duniani kwa miaka mingi ijayo.”

Ametoa wito “Kuchukua hatua kupunguza haraka matumizi ya mafuta kisukuku ili kuepusha janga kubwa la tabianchi katika karne hii na zijazo.” Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasili Dubai kwa ajili ya kushiriki mkutano huo

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.
© WMO/Fouad Abdeladim
Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.

Hali ya Hewa 

Tukisalia ma mabadiliko ya tabianchi ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu hali ya hewa duniani na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO, imethibitisha kwamba mwaka 2023 utavunja rekodi ya kuwa mwaka wenye joto zaidi katika historia huku shirikika hilo likionya kuhusu mwenendo unaoashiria kutokea kwa mafuriko zaidi, moto wa nyika, kuyeyuka kwa barafu na joto la kupindukia katika siku zijazo. 

Takwimu za hadi mwezi Oktoba mwaka huu za shirika hilo zinaashiria kwamba wastani wa joto umekuwa ni nyuzi joto 1.40C zaidi ya ilivyokuwa kabla ya maendeleo ya viwanda.

Mama na mwanaye wakiwa katika kitanda chenye chandarua chenye dawa ya mbu katika jimbo la Kassala Sudan
© UNICEF/Mojtba Moawi Mahmoud
Mama na mwanaye wakiwa katika kitanda chenye chandarua chenye dawa ya mbu katika jimbo la Kassala Sudan

Ugonjwa wa malaria

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO, limesema katikia ripoti yake mpya iliyotolewa leo kwamba licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kupanua wigo wa kupata vyandarua vya mbu vyenye dawa pamoja dawa za kusaidia kuzuia malaria kwa watoto na kina mama wajawazito, watu wengi zaidi wamekuwa wakiugua malaria. 

Kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo mwaka 2022 kulikuwa na wagonjwa wa malaria milioni 249 duniani kote ikiwa ni wagonja milioni 16 zaidi ya ilivyokuwa kabla ya janga la coronavirus">COVID-19.