Gaza: Watoto 31 wafanikiwa kuondolewa katika hospitali ya Al-shifa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limesema limefanikiwa kuwahamisha watoto 31 walio katika hali mbaya kwenye hospitali ya Al-Shifa huko katika Ukanda wa Gaza na mkuu wa shirika hilo kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas kwa sababu za kibinadamu .
Wito huo umekuja wakati kuna ongezeko la vifo, mashambulizi dhidi ya shule na maeneo wakimbizi wanapopatiwa hifadhi ikiwa ni pamoja na kifo cha mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, na uhaba wa mafuta unaozuia utoaji wa misaada kote katika Ukanda wa Gaza.
Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa waliunga mkono wito wa kuboreshwa kwa hali za watu milioni 2.3 wa Gaza, milioni 1.7 ambao wamekimbia makazi yao tangu shambulio la Oktoba 7 la Hamas nchini Israeli lililo sababisha mauaji ya Waisraeli 1,200 na 240 kuwakamata mateka. Tangu wakati huo, zaidi ya watu 11,000 wameuawa huko Gaza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika taarifa yake aliyoitoa hii leo jijini New York Marekani amesema “Vita hivi vina idadi kubwa na isiyokubalika ya raia majeruhi, wakiwemo wanawake na watoto, kila siku. Hii lazima ikome. Narudia wito wangu wa kusitisha mapigano mara moja kwa sababu za kibinadamu.”
Hospitali ya Al-Shifa
Operesheni za kijeshi zinazoendeshwa na Israel zimekuwa zikiendelea ndani na karibu na Hospitali ya Al-Shifa, huku wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliotembelea eneo hilo hapo jana wakielezea eneo hilo kama “eneo la kifo”.
WHO na wadau wake wa masuala ya kibinadamu walisaidia kuwahamisha watoto wachanga katika hali mbaya.
Wahudumu wa afya, wagonjwa na raia walikimbia hospitali mwishoni mwa juma, walioamriwa kuondoka , UNRWA inasema amri hiyo ilitolewa na jeshi la Israeli, na kwamba mamia ya watu walionekana wakielekea kusini mwa Gaza kwa miguu, katika hatari kubwa kwa maisha, afya na usalama wao.
WHO iliripoti hii leo kuwa magari sita ya kubebea wagonjwa ya Shirika la kimataifa la Hilali Nyekundu yaliwasafirisha watoto hao hadi katika Hospitali ya Wazazi ya Al-Helal Al-Emirati, ambako wanapata huduma ya haraka.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X amesema “Misheni zaidi zinapangwa kusafirisha kwa haraka wagonjwa waliosalia na wafanyakazi wa afya nje ya Hospitali ya Al-Shifa.”
Sheria za kimataifa ziheshimiwe
Naye Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu OHCHR Volker Türk katika taarifa yake aliyoitoa hii leo huko Geneva Uswisi amesema matukio yaliyotokea huko Gaza ndani ya saa 48 zilizopita yanaodnoa Imani
Türk amesema “Mauaji ya watu wengi katika shule ambazo zimegeuzwa makazi, mamia wakikimbia kuokoa maisha yao kutoka Hospitali ya Al-Shifa huku mamia kwa maelfu wakihama makazi yao kusini mwa Gaza ni vitendo ambavyo vinaendana na ulinzi wa kimsingi ambao raia wanapaswa kulipwa chini ya sheria za kimataifa.”
Ameeleza kwamba kushindwa kutekelezwa kwa sheria za kimataifa kunaweza kujuishwa huu kuwa uhalifu wa kivita.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA, takriban wakimbizi wa ndani 884,000 wanahifadhiwa katika vituo 154 vya UNRWA katika majimbo yote matano ya Ukanda wa Gaza.
“Kuingia tu katika moja ya makazi hukufanya ulie machozi,” alisema mfanyakazi wa UNRWA nakuelezea hali iliyopo huko ni kuwa “Watoto wanatafuta chakula na maji na kusimama kwenye foleni kwa zaidi ya saa sita ili tu kupata kipande cha mkate au chupa ya maji. Watu wanalala barabarani hapa Khan Younis huku maelfu wakiendelea kutoroka kutoka kaskazini.”
UNRWA pia imesema chini ya saa 24, shule mbili za UNRWA zinazohifadhi familia za wakimbizi wa ndani zilishambuliwa na kusababisha “vifo vingi” na majeruhi, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, pamoja na matukio mengine mabaya kote Gaza na Ukingo wa Magharibi, hali hii pia imeongeza dhidi ya mahitaji ya kibinadamu.

Mapigano lazima yakome sasa hivi
Kamishna Türk amesema takriban shule nyingine tatu zinazohifadhi wakimbizi wa kipalestina pia zimeshambuliwa. “Hii lazima ikome.”. Ubinadamu lazima utangulie. Kusitishwa kwa mapigano - kwa misingi ya kibinadamu na haki za binadamu - kunahitajika sana hivi sasa.”
Kamishna Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini, naye ametoa taarifa yake hii leo kueleza mashambulizi yanayoendelea huko Gaza ni “ya kikatili tu”. “Nimetazama taarifa za kutisha kutoka kwenye shambulio la shule ya Al-Fakhoura shule ambayo iasimamiw ana UNRWA huko Kaskazini mwa Gaza.”
Akielezea zaidi amesema madarasa yanayohifadhi familia za wakimbizi wa ndani yalishambuliwa na takriban watu 24 waliripotiwa kuuawa katika tukio hilo. Takriban watu 7,000 walikuwa wanapata hifadhi shuleni hapo.
Siku ya Ijumaa, kufuatia tukio hilo katika shule ya UNRWA Al-Falah/Zeitoun, magari ya kubebea wagonjwa hayakuweza kufika shuleni hapo, ambapo watu 4,000 walikuwa wamejihifadhi.
Mkuu huyo wa UNRWA ametoa takwimu zinazoeleza kuwa tangu tarehe 7 Oktoba, takriban watu 176 waliokuwa wakihifadhi katika shule za shirika hilo waliripotiwa kuuawa na 800 kujeruhiwa wakati wa mashambulizi ya Israel.
“Idadi kubwa ya vituo vya UNRWA vilivyoathiriwa na idadi ya raia waliouawa haiwezi tu kuwa “dhamana ya uharibifu” na kwani mashirika ya Umoja wa Mataifa mara kwa mara wamekuwa yakitoa taarifa sahihi za wapi majengo yalipo kwa wahusika kwenye mzozo huko.
“Vita hivi vikali vinafikia hatua ya kutorudi nyuma wakati sheria zote zinapuuzwa, kwa kupuuza kabisa maisha ya raia,” na kutoa wito “kwa mara nyingine tena kwa ubinadamu kushinda na kwa usitishaji wa mapigano kwasababu za kibinadamu sasa hivi.”
Ukingo wa Magharibi
Kulingana na ripoti zilizotolewa na UNRWA Matukio ya vurugu, vifo na majeraha yalmeumba maeneo kadhaa ya Ukingo wa Magharibi katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabau, ikiwa ni pamoja na kambi za wakimbizi za Fara'a na Jenin.
Shirika la Umoaj wa Mataifa la kuratibu misaada ya dharura OCHA illiripoti kuwa tangu tarehe 7 Oktoba, Wapalestina 198, wakiwemo watoto 52, wameuawa na vikosi vya usalama vya Israel na wanane, akiwemo mtoto mmoja, na walowezi wa Israel.
Katika kambi ya wakimbizi ya Balata huko Nablus hapo jana, vikosi vya usalama vya Israel vilianzisha operesheni, vikiingia na tingatinga lililokuwa la kivita na kuhamasisha ndege isiyo na rubani iliyorusha makombora kuelekea ofisi ya Fatah, na kuua watu watano, kujeruhi wengine wawili na kuharibu nyumba na maduka.