Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je wafahamu kuhusu Tsunami?

Watoto katika darasa moja nchini Indonesia wanajificha chini ya meza zao wakati wa mazoezi ya kujitayarisha dhidi ya tsunami.
UNDRR/Antoine Tardy Watoto katika shule mjini Bali, nchini Indonesia wakishiriki mafunzo ya kujikinga wakati wa tsunami

Je wafahamu kuhusu Tsunami?

Masuala ya UM
  • Asili ya neno ni Japani
  • Matetemeko ya ardhi huweza kusababisha tsunami
  • Tsunami kubwa zaidi ilikuwa mwaka 1883 nchini Indonesia
Mtazamo wa angani wa mashua ikipita kwenye maji ya bahari ya zumaridi na bluu yenye kina kirefu, ikiacha mkondo mweupe dhidi ya upeo wa macho ulio wazi.
Ocean Image Bank/David Gross Kuna programu mpya ya UNESCO ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 wakazi wa pwani wanakuwa wamejiandaa dhidi ya tsunami.

Neno "tsunami" linaundwa na maneno ya kijapani "tsu" (maana ya bandari) na "nami" (maana ya wimbi), hivyo ni wimbibahari. Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya baharí.

Wavuti wa Umoja wa Mataifa  kwa kawaida huhusishwa na matetemeko ya ardhi yanayotokea chini ya baharí au karibu na bahari. Vile vile milipuko ya volkano, maporomoko makubwa ya miamba ndani ya baharí kutoka eneo lenye kiwango kidogo cha maji hadi eneo lenye kina kikubwa cha maji.

Maporomoko ya miamba iliyo pwani nayo huweza kusababisha tsunamirdhi yasababishwayo na  nyambizi, na maporomoko ya miamba ya pwani pia yanaweza kusababisha tsunami, halikadhalika vimondo vinaweza kuathiri baharí.

Mawimbi hayo huanza kwa mwenendo wa wima kwenye sakafu ya baharí na kisha kusukuma kiwango kikubwa cha maji.

Muonekano wa mawimbi ya tsunami

Mawimbi ya tsunami mara nyingi huonekana kama kuta za maji na yanaweza kushambulia fukwe na kuwa hatari kwa saa nyingi, huku mawimbi yakija kila baada ya dakika 5 hadi 60. 

Wimbi la kwanza linaweza lisiwe kubwa zaidi, na mara nyingi ni mawimbi ya 2, 3, 4 au hata baadaye ambayo ni makubwa zaidi. 

Wanajamii wa eneo hilo wanafanya mazoezi ya njia ya uokoaji wa tsunami nchini Mauritius.
UNDRR Jamii nchini Mauritius wakifanya mazoezi ya kuhama pindi tsunami inatokea.

Baada ya wimbi moja kupungua nguvu au kusababisha mafuriko eneo la bara, hurejea baharini na kusonga mbali kwa kadri ya upeo wa macho na hapo sakafu ya baharí huweza kuonekana.

Kisha wimbi linalofuata huelekea ufukweni ndani ya dakika chache na kubeba taka nyingi zinaozelea zinazotokana na uharibifu wa wimbi la awali.

Nini husababisha tsunami?

Matetemeko ya ardhi

Huweza kuchochewa na mwenendo kwenye maeneo yaliyoharibiwa kutokana na kusogea kwa mipaka ya bamba la ardhi baharini.

Matetemeko mengi makubwa hutokea kwenye eneo hilo la chini ya baharí baada ya bamba moja kupandia bamba lingine ambalo ni changa.

Ingawa hivyo si matetemeko yote ya ardhi ambayo yanasababisha tsunami. Kuna vigezo vinne ambavyo lazima vitokee chini ya baharí ndipo tetemeko lisababishe tsunami.

Vigezo vya tetemeko kusababisha tsunami
  • Tetemeko lazima litokee chini ya baharí au lisababishe itu vitumbukie baharini.
  • Tetemeko la ardhi lazima liwe kubwa, angalau ukubwa wa 6.5 katika kipimo cha Ritcher.
  • Tetemeko lazima lichane uso wa dunia na lazima liwe limetokea kwenye kina kidogo – liwe chini ya kilometa 70 kutoka uso wa dunia.
  • Tetemeko lazima lisababisha mienendo ya mawimbi wima kwenye sakafu ya baharí kwa mita kadhaa.

Maporomoko ya ardhi

Maporomoko ya ardhi pia husababisha tsunami hasa yakitokea kando ya pwani, yanaweza kusukuma kiasi kikubwa cha maji ndani ya bahari, kuvuruga maji na kusababisha tsunami. Maporomoko ya ardhi chini ya maji vile vile yanaweza pia kusababisha tsunami wakati vifusi iliyotolewa na maporomoko ya ardhi vinasonga kwa nguvu, na kusukuma maji mbele yake.

Manusura akitembea kwenye vifusi vya kijiji kilichoharibiwa huko Mamboro, Indonesia, baada ya tsunami kufuatia tetemeko la ardhi.
OCHA/Anthony Burke Kijiji kimoja katika kisiwa chaSulawesi, Indonesia kiliharibiwa kabisa.Wakati tetemeko la ardhi lilipotokea watu walikimbilia kwenye bahari wakiogopa nyumba zao zitawangukia. Tena tsunami ikafuatia.

Milipuko ya volkano

Ingawa milipuko ya volkeno haifanyiki mara kwa mara, milipuko yenye vurugu pia huleta misukosuko ya ghafla, ambayo inaweza kusukuma kiasi kikubwa cha maji na kutoa mawimbi ya tsunami yenye uharibifu sana katika eneo la chanzo cha karibu.

Je wajua?

Tsunami kubwa na mbayá zaidi kuwahi kurekodiwa ilitokea tarehe 26 Agosti mwaka 1883 nchini Indonesia. Ilitokana na mlipuko wa volkano yam lima Krakatoa (Krakatau) nchini Indonesia. Mlipuko huo wa volkano ulisababisha wimbi la ukubwa wa futi 135 na kuharibu miji na vijiji vya pwani kando ya mfereji wa Sunda kwenye visiwa vyote vya Java na Sumatra na kuua watu 36,417.

Migongano kutoka anga za juu

Tsunami zinazosababishwa na migongano ya vitu vilivyoko anga za juu kama vile vimondo hutokea mara chache. Ijapokuwa hadi sasa hakuna tsunami zilizochochewa na vimondo, wanasayansi wanabaini kuwa iwapo vitu hivyo vya anga za juu vitatumbukia baharini, kiwango kikubwa cha maji bila shaka kitasukumbwa na kusababisha tsunami.