Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya Pamoja kuimarisha afya ya binadamu, wanyama na sayari

Msaidizi wa Afya ya Wanyama kutoka Kaunti ya Samburu akiwachanja mbuzi kama sehemu ya mpango wa chanjo ya PPR huko Wamba, Kenya. Wanawake watatu waliovalia mavazi ya kitamaduni ya Wamasai husaidia kwa kuwashikilia wanyama hao katika mazingira kame na ya mashambani.
©FAO/Luis Tato Programu ya kutoa chanjo dhidi ya PPR katika kauti ya Samburu nchini Kenya mnamo Septemba 2017

Afya ya Pamoja kuimarisha afya ya binadamu, wanyama na sayari

Afya
  • Mwaka wa 8 wa kampeni utashi wa kisiasa wahitajika
  • COVID-19 imedhihirisha umuhimu wa kampeni hii
  • Hatua za Afya Pamoja zimethibitishwa kisera
Tweet URL

Viongozi wa dunia waongeze dhamira ya kisiasa kuzuia na kukabili vitisho vinavyoathiri afya ya binadamu, wanyama na mazingira, amesema Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Afya, WHO.

Dkt. Tedros amesema hayo leo kupitia taarifa iliyotolewa leo jijini Geneva, Uswisi ikiwa ni leo ni mwaka wa nane wa kampeni ya Afya ya Pamoja, ikilenga kuonesha jinsi vitendo na sera za binadamu vinaweza kuathiri afya ya wanyama na mazingira

Kupitia siku hii ya Afya Pamoja kila mtu anapata fursa ya kujielimisha kuhusu uhusiano kati ya afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira”, amesema Dkt. Tedros.

Uhusiano wa afya ya binadamu, wanyama na mazingira

Athari za kiafya zitokanazo na janga la tabianchi, uchafuzi wa maji, usalama wa chakula na ongezeko la magonjwa ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili binadamu na sayari hivi sasa.

Mathalani uchafuzi wa hewa husababisha vifo vya watu milioni 7 kila mwaka na hasara ya dola trilioni 3.

Usugu wa viua vijiumbe maradhi husababisha vifo vya watu milioni 5 kila mwaka na hasara ya kiuchumi itafikia dola trilioni 100 mwaka 2050.

Makadirio ya vifo vya binadamu kutokana na coronavirus">COVID-19, gonjwa lililoibuka hivi karibuni yalikuwa milioni 6 mwaka 2022, sambamba na hasara ya kiuchumi ya dola trilioni 3.5.

Faida za Afya Pamoja

Amefafanua kuwa kampeni ya Afya Pamoja ni mbinu iliyothibitishwa ya utungaji sera na ushirikiano wa sekta mtambuka ili kuzuia magonjwa yanayoenezwa na wanyama na vimelea.

Halikadhlika kuepusha kuibuka mara kwa mara kwa magonjwa, kuhakikisha usalama wa chakula na kudumisha uzalishaji endelevu wa chakula; kupunguza usugu wa viua vijiumbe maradhi; na kushughulikia masuala ya mazingira ili kuboresha kwa pamoja afya ya binadamu, wanyama na mazingira, miongoni mwa maeneo mengine mengi

Afya ya binadamu italindwa iwapo tunalinda ya wanyama na mazingira

Wanawake wakifunga vyombo vya maji kwa punda kwenye sehemu ya maji katika kijiji kimoja katika Kaunti ya Marsabit, Kenya.
© WFP/Alessandro Abbonizio Wanawake wakikusanya maji katika eneo lililokumbwa na ukame Marsabit kaskazini mwa Kenya.

Ametamatisha kwa kusema ni dhahiri kuwa tunaweza kulinda na kuendeleza afya ya binadamu kwa kulinda afya ya wanyama na sayari dunia ambayo tunaitegemea. Tunakaribisha ongezeko la maridhiano ya kisiasa juu ya Afya ya Pamoja duniani kote na tumeazimia kusaidia nchi kutekeleza kwa vitendo suala la Afya ya Pamoja ili kuleta mabadiliko.”

Mashirika ya UN kwenye kampeni hii ni pamoja na FAO, UNEP, WHO na WOAH