UN WOMEN waanzisha wavuti maalum wa stori za wanawake wa Afghanistan
Tarehe 15 Agosti 2021, kila kitu kilibadilika kwa wanawake na wasichana nchini Afghanistan. Kwanza ilianza vikwazo vya elimu ya wasichana na haki ya wanawake kufanya kazi, kisha utekelezaji wa kanuni kali kuhusu mavazi na kuweka kanuni kwenye uhuru wa wanawake kutembea na kuendelea na maisha yao kwenye maeneo ya umma.
Miaka miwili baada ya uongozi wa Taliban kutwaa madaraka nchini Afghanistan, zaidi ya amri 50, kanuni na vizuizi zimewekwa kwa utaratibu seti za sera zilizoundwa kwa uangalifu ambazo zinakosesha usawa na zinaathiri kila sehemu ya maisha ya mwanamke.
Sera hizo zina dhibiti mahali ambapo mwanamke anaweza kwenda na jinsi gani anapaswa kuvaa.
Tangu siku ya kwanza, uongozi wa Taliban umeonekana kuwabana, kuleta uwoga na ukandamizaji lakini umekabiliwa na ujasiri usio na woga kutoka kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan ambao wanaendelea kupinga, na kupaza sauti.
After August
Kupigania haki za wanawake ni mapambano makali kila mahali duniani. Lakini Afghanistan kwa sasa ni sehemu ambayo inategemea sana kupigania haki zao ili waweze kupata ahueni.
Shirika la Umojawa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN wametengeneza wavuti mahususi kwa ajili ya stori za wanawake wa Afghanistan iitwayo “After August”.
Mkurugenzi Mkuu wa UN WOMEN Sima Bahous akizungumzia hali ya wanawake wa Afghanistan amesema “Ingawa wapp katika hali ya uhasama zaidi wanawake wa Afghanistan wanazungumza dhidi ya ukiukaji, wanatoa huduma za kuokoa maisha, wanamiliki na kuendesha biashara, na kuendesha mashirika ya wanawake. Ushujaa wao lazima ututie moyo kuchukua hatua kubwa zaidi.”
Taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa UN WOMEN imeelezakuwa “Tuliunda "After August" (Baada ya mwezi Agosti) tukiwa na imani kuwa, wakati ukosefu wa haki ni kawaida, ukimya haukubaliki. "After Agust" ni uwanja wa kidijitali wa kuandika na kushirikisha ulimwengu uzoefu wa wanawake wa Afghanistan wanaoishi na kupinga yale yanayoendelea nchini Afghanistan hivi sasa.
Wavuti huo umesheheni simulizi za kupinga kampeni ya Taliban kuwafanya wanawake wa Afghanistan wasionekane.
Kama umewahi kudhulumiwa kwa ajili ya kutetea haki zako, kuambiwa unyamaze unapozungumza, au kushambuliwa kwa kuishi maisha uliyochagua wewe mwenyewe, basi “After August”, ni sehemu nzuri ya kusoma na pia usisahau kusambaza kwa wengine ili nao wapate kufahamu kinachoendelea kwa wanawake wa Afghanistan.