Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitamani tena kuzamia kwenda Ulaya: Manusura kutoka Gambia

Amadou Jobe, mhamiaji ambaye alirejea Gambia kutoka Ulaya, akiangalia bahari ya Pasifiki kutoka pwani ya Gambia.
UN News/ Hisae Kawamori
Amadou Jobe, mhamiaji ambaye alirejea Gambia kutoka Ulaya, akiangalia bahari ya Pasifiki kutoka pwani ya Gambia.

Sitamani tena kuzamia kwenda Ulaya: Manusura kutoka Gambia

Wahamiaji na Wakimbizi

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka bahari ya Mediterania kwa lengo la kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. Evariste Mapesa anatupeleka nchini Gambia kusikia simulizi ya kijana ambaye chupuchupu apoteze maisha. 

 

Ni Amadou Jobe kijana ambaye akiwa na umri wa miaka 25 alianza safari ya hatari kutoka nchini Kwake Gambia kupitia kaskazini mwa Afrika lengo likiwa Kwenda nchini Italia kusaka maisha bora kwani alikuwa akiishi katika hali ya umasikini na alitamani kuja kuisaidia familia yake iwapo angefanikiwa kufika Ulaya.

Safari ya Amadou haikuwa rahisi kwa zaidi ya miaka miwili alikuwa safarini kutoka nchini mwake Gambia alienda mpaka nchi ya Mauritania, kisha Mali, akaingia Niger na mwisho nchini Libya nchi ambayo baada ya kukaa zaidi ya mwaka mmoja alifanikiwa kupata boti ambayo ndio ingetimiza ndoto yake ya Kwenda Ulaya.

Baada ya kujaribu na kushindwa kufika Italia kwa boti kutoka Tripoli, Amadou Jobe alirejea nyumbani Gambia, na sasa anajitahidi kujikwamua kimaisha na familia yake.
UN News/ Hisae Kawamori
Baada ya kujaribu na kushindwa kufika Italia kwa boti kutoka Tripoli, Amadou Jobe alirejea nyumbani Gambia, na sasa anajitahidi kujikwamua kimaisha na familia yake.

“Ndani ya boti yetu, kulikuwa na zaidi ya watu 100 kutoka Gambia, watu wengine niliowakuta ni Wanigeria na wengine wanatoka Liberia kiufupi kulikuwa na nchi  kutoka barani Afrika. Siku tulipojaribu kuvuka Kwenda Ulaya, boti yetu ilikuwa na matatizo na hali ya hewa pia haikuwa nzuri. Tuliona maji yakijaa ndani ya boti yetu. Kwa hivyo tuliamua kurudi kwa sababu kama tukitaka kuendelea, tungaweza wote kufamaji huko.”

Bahati haikuwa yake kwani alipojaribu kusafiri awamu ya pili walikamatwa na kufingwa jela nchini Libya anasema maisha jela yalikuwa mabaya na baadaye Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM liliwatembelea gerezani na kuwapatia fursa ya kurejeshwa makwao na Amadou naye alirejea nyumbani Gambia. 

Amadou Jobe (kushoto), mhamiaji ambaye alirejea nyumbani akitoa mafunzo kwa wanagenzi katika warsha huko Banjul, Gambia.
UN News/Conor Lennon
Amadou Jobe (kushoto), mhamiaji ambaye alirejea nyumbani akitoa mafunzo kwa wanagenzi katika warsha huko Banjul, Gambia.

“Sikuwa nataka kurudi hapa. Nilitaka kuendelea na safari yangu. Nina huzuni sana kwa sababu pesa zote nilizotumia, nilipoteza kila kitu na kuja kuanza upya kutoka sifuri. Nimetumia karibu dola 1700. Lakini hakuna la kufanya. Mahali tulipokuwa tusingeweza kwenda kokote na hauwezi kutoroka.”

Marie Stella Ndiaye ni meneja program wa IOM nchini Gambia anaeleza baada ya kuwajeresha makwao hawawaachi pia wa programu za kuwasaidia. 

“Tumejikita kwenye kuwatafuta na kuokoa maisha yao. Pia tunatoa usaidizi kwenye vituo vya rasilimali za wahamiaji vilivyo katika nchi ambazo wahamiaji hawa hupita wakitaka kusafiri Kwenda ulaya. Mara tu wanaporejea, IOM inatoa usaizi wa kila aina kuanzia masuala ya ushauri nasaha, ujumuishaji wa kiuchumi, ujumuishaji upya wa kijamii, lakini pia, muhimu zaidi, usaidizi wa kisaikolojia.”

Amadou Jobe, mhamiaji anayerejea kutoka Ulaya amepata kazi katika mji mkuu wa Gambia, Banjul.
UN News/ Hisae Kawamori

Mara bada ya kurejea nchini Gambia Amadou alipata ufundi stadi kutoka mashirika ya UN ambayo ni IOM na UNCDF na sasa anafanya kazi ya fundi uashi, ameoa na ana watoto wawili. Ameapa kutojaribu tena kuzamia kwenda ulaya, ataenda bara hilo kwa kupanda ndege kihalali nasi vinginevyo.