Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baiskeli ni usafiri usiochafua mazingira na wa gharama nafuu:UN

Mwanamke akienda kuteka maji kwa kutumia Baiskeli karibu na Boromo nchini Burkina Faso
© CIFOR/Ollivier Girard
Mwanamke akienda kuteka maji kwa kutumia Baiskeli karibu na Boromo nchini Burkina Faso

Baiskeli ni usafiri usiochafua mazingira na wa gharama nafuu:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya baiskeli duniani na Umoja wa Mataifa unasema siku hii inaangazia faida za kutumia baiskeli  ambayo ni njia rahisi, nafuu, safi na inayofaa kimazingira ya usafiri.

Baiskeli huchangia katika hewa safi na msongamano mdogo na hufanya elimu, huduma za afya na huduma nyingine za kijamii kufikiwa zaidi na watu walio hatarini zaidi.

Pia Umoja huo umeongeza kuwa “baiskeli ni mfumo endelevu wa usafiri unaokuza ukuaji wa uchumi, unapunguza kukosekana kwa usawa huku ukiimarisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na ni muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG’s”.

Kwa nini kusherehekea baiskeli?

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mazoezi ya mara kwa mara ya nguvu ya wastani kama vile kutembea, kuendesha baiskeli, au kufanya michezo kuna manufaa makubwa kwa afya.

Katika umri wotewote, manufaa ya kuwa na shughuli za kimwili hupita madhara yanayoweza kutokea, kwa mfano kupitia ajali.

Baadhi ya shughuli za kimwili ni bora kuliko kutojishughulisha.  Umoja huo umesisitiza kuwa kwa kuwa hai zaidi siku nzima kwa njia rahisi, watu wanaweza kufikia viwango vya shughuli vilivyopendekezwa kwa urahisi.

Maeneo ambako magari hayawezi kufika, baiskeli zinatumika kufikisha vifaa vya shule kwenye majimbo 6 yaliyonufaika na mradi wa Kurejea Shuleni.
UNICEF Burundi
Maeneo ambako magari hayawezi kufika, baiskeli zinatumika kufikisha vifaa vya shule kwenye majimbo 6 yaliyonufaika na mradi wa Kurejea Shuleni.

Kulingana na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO, miundombinu salama ya kutembea na kuendesha baiskeli pia ni njia ya kufikia usawa zaidi wa afya.

Kwa sekta maskini zaidi za mijini, ambazo mara nyingi haziwezi kumudu magari binafsi, kutembea na kuendesha baiskeli kunaweza kutoa aina ya usafiri salama huku ukipunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, kiharusi, baadhi ya saratani, kisukari, na hata kifo.

Vilevile shirika hilo limeongeza kusema kwamba uboreshaji wa usafiri wa kazi sio afya tu, pia ni ya usawa na ni usafiri wa gharama nafuu.

Kukidhi mahitaji ya watu wanaotembea na waendesha baiskeli kunaendelea kuwa sehemu muhimu ya suluhisho la uhamiaji kusaidia miji kupunguza ukuaji wa watu kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji, na kuboresha ubora wa hewa na usalama barabarani.

Janga la COVID-19 pia limesababisha miji mingi kufikiria upya mifumo yao ya usafirishaji.

Baiskeli na maendeleo endelevu

Hapo tarehe 15 Machi 2022, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kujumuishwa kwa baiskeli katika mifumo ya uchukuzi wa umma kwa maendeleo endelevu.

Azimio hilo linasisitiza kuwa baiskeli ni chombo cha usafiri endelevu na kinachotoa ujumbe chanya wa kustawisha matumizi na uzalishaji endelevu, na kina athari chanya kwa hali ya hewa.