Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya kiuchumi yanapunguza matarajio ya ajira katika nchi masikini: ILO

Wafanyakazi wa sekta ya ushonaji nguo nchini Bangladesh wakitoka kiwandani mwisho wa siku
© ILO/ Marcel Crozet
Wafanyakazi wa sekta ya ushonaji nguo nchini Bangladesh wakitoka kiwandani mwisho wa siku

Matatizo ya kiuchumi yanapunguza matarajio ya ajira katika nchi masikini: ILO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kuongezeka kwa viwango vya madeni vilivyochangiwa na mfumuko mkubwa wa bei na kupanda kwa viwango vya riba kumekatisha matumaini ya wanaosaka ajira katika nchi zinazoendelea, limeonya leo shirika la kazi la Umoja wa Mataifa  duniani (ILO).

Katika ripoti yake mpya ya “Ufuatiliaji wa mwenendo wa ajira Ulimwenguni”, ILO inaonyesha kuwa wakati katika nchi zenye kipato cha juu, ni asilimia 8.2 tu ya watu walio tayari kufanya kazi hawana ajira, idadi hiyo inaongezeka hadi zaidi ya asilimia 21 katika nchi zenye kipato cha chini au mtu moja katika kila watu watano.

Nchi zenye kipato cha chini zilizo katika changamoto ya madeni zimeathirika zaidi, huku zaidi ya mtu mmoja kati ya watu wanne wanaotaka kufanya kazi wakishindwa kupata ajira.

Kupanuka kwa pengo la ajira

Mkurugenzi mkuu msaidizi wa ajira na hifadhi ya jamii wa ILO, Mia Seppo, amesema ukosefu wa ajira duniani unatarajiwa kushuka chini zaidi ya viwango vya kabla ya janga la COVID-19, na makadirio ya kiwango cha asilimia 5.3 mwaka 2023, sawa na watu milioni 191.

Hata hivyo, nchi za kipato cha chini, hasa zile za Afŕika na ukanda wa nchi za Kiarabu hazikuwa na uwezekano wa kuona upungufu huo wa ukosefu wa ajiŕa mwaka huu.

Pengo la ajira duniani la mwaka 2023, ambalo linahusu wale wanaotaka kufanya kazi lakini hawana kazi, linatarajiwa kuongezeka hadi watu milioni 453, amesema Seppo na kuongeza kuwa na wanawake wanathirika mara 1.5 zaidi kuliko wanaume.

Uchumi utokanao na shughuli zisizorasimishwa kama hapa nchini Madagascar, ni hali ya kawaida katika mazingira ambamo hakuna ajira zisizo na staha na zenye ujira mdogo
ILO/Marcel Crozet
Uchumi utokanao na shughuli zisizorasimishwa kama hapa nchini Madagascar, ni hali ya kawaida katika mazingira ambamo hakuna ajira zisizo na staha na zenye ujira mdogo

Afrika inaathirika zaidi

Shirika hilo la ajira la Umoja wa Mataifa limeonyesha zaidi kuwa soko la ajira la Afrika ndilo lililoathirika zaidi wakati wa janga la COVID-19, ambalo llilionyesha kasi ndogo yakujikwamua katika bara hilo.

Tofauti na mataifa tajiri, tatizo la madeni katika bara zima na nafasi ndogo sana ya kifedha na sera, inamaanisha kuwa nchi chache barani Afrika ndizo zinaweza kuweka fecha zinazohitajika kama kichocheo ili kufufua uchumi wake, limeeleza shirika la ILO.

Ulinzi duni wa hifadhi ya jamii

Bi. Seppo amesisitiza kuwa bila kuboreshwa kwa matarajio ya ajira ya watu, hakutakuwa na ufufuaji mzuri wa kiuchumi na kijamii.

Afisa huyo mkuu wa ILO amesisitiza kuwa umuhimu ni sawa na uwekezaji katika hifadhi ya ustawi wa jamii kwa wale wanaopoteza ajira ambao mara nyingi hautoshi katika nchi za kipato cha chini.

Kulingana na utafiti wa ILO kuimarisha ulinzi wa hifadhi ya jamii na kupanua wigo wa kiinua mgongo kwa wazee kungeongeza pato la taifa (GDP) kwa kila mtu katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati kwa karibu asilimia 15 katika muongo mmoja.

Faida za uwekezaji wa kijamii

Gharama ya kila mwaka ya hatua kama hizo itakuwa karibu asilimia 1.6 ya Pato la Taifa ni uwekezaji mkubwa lakini usioweza kushindwa.

Bi. Seppo amependekeza kuwa kiasi hicho kinaweza kufadhiliwa na mchanganyiko wa michango ya kijamii, kodi na usaidizi wa kimataifa.

Baba asiye na ajira akipokea msaada kutoka UNICEF nchini Afghanistan.
© UNICEF/Omid Fazel
Baba asiye na ajira akipokea msaada kutoka UNICEF nchini Afghanistan.

"Kuna faida za kiuchumi kwa kuwekeza katika hifadhi ya jamii", amesema.

Bi. Seppo pia amesisitiza kwamba haja ya kuunda fursa za kifedha kwa ajili ya uwekezaji wa kijamii katika nchi za kipato cha chini na zinapaswa kuzingatiwa "kwa haraka kama sehemu ya mjadala unaoendelea wa kimataifa kuhusu mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa."

Jiandae kwa mustakabali wa ajira

Ingawa mgawanyiko wa wasio na ajira uliokadiriwa na ripoti ulikuwa wa kutisha, hauwezi kuepukika amesema, Bi. Seppo na kuongeza kuwa hatua sahihi za pamoja juu ya kazi na ufadhili wa ulinzi wa hifadhi ya jamii unaweza kusaidia ufufuaji na ujenzi ambao haumwachi mtu yeyote nyuma.

Katika kutoa wito wa kuboreshwa kwa uwezo wa kuunda sera za soko la ajira zenye ufahamu na takwimu ambazo zinalinda walio hatarini zaidi, afisa huyo mkuu wa ILO amesisitiza kwamba “hizi zinapaswa kutilia mkazo katika kuongeza ujuzi na kuwapa nguvu kazi upya ili kujitayarisha kwa mazingira mazuri katika ulimwengu wa kazi wa kidijitali”.