Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yasisitiza ujumuishwa wa wanawake katika mkutano wa The Africa Soft Power Rwanda

Mkutano wa pili ambao ulifanyika Kigali kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2023, na kuvutia washiriki kutoka kote ulimwenguni kujadili masuala muhimu yanayohusu bara moja kwa moja.
© RCO/Aristide Muhire

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Viongozi, watafiti, vijana, na wanawake kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika Kigali kwa ajili ya mkutano wa pili wa Africa Soft Power kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2023.

Mkutano huu umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa nchini Rwanda. Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Rwanda ni Ozonnia Ojielo anasema

“ Mkutano wa Soft Power Africa, ni mradi mzuri unaohusu ukweli kwamba tunahitaji wote wanaume na wanawake ili kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii, ni kuhusu kuwawezesha wanawake kufikia uwezo wao na hivyo majadiliano haya yanaangazia machaguo mbalimbali lakini hususani kuhusu jukumu la sekta binafsi , nafasi ya uwezeshaji wa kiuchumi kama nyenzo kwa ajili ya mabadiliko, na ndio sababu mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda unafuha kushirikiana na mradi huu wa Soft Power Africa “

Mkutano wa Africa Soft Power ni tukio kuu ambalo lengo lake ni kukuza viwanda vya ubunifu vya Afrika, uchumi wa maarifa, na kutumia nguvu yake laini kwa maendeleo. Balozi Amina Mohamed kutoka Kenya alikuwa na haya ya kusema kuhusu mradi huu

" Nadhani hili ni jukwaa zuri sana na ninafurahi kwamba hii ni mara ya pili tu linafanyika, na hivyo matarajio yangu ni kwamba nitahudhuria pia lijalo, ili tuweze kuona kwamba tunachokizungumzia ni athari za maendeleo katika bara zima.”

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda aliongoza majadiliano ya jopo ambalo lilichunguza jukumu la taasisi za jadi za Kiafrika katika kukuza maendeleo ya bara hilo, na mifano ni mingi kama asemavyo Mfalme wa Onitsha jimbo la Anambra Kusini Mashariki mwa Nigeria Mfalme Nnaemeka Alfred Achebe

“ Tukisukumwa na janga la COVID-19 tuliharakisha mpango tulioanzisha mnamo 2017 mwanzoni mwa jukwaa la maendeleo yetu ya jamii. Tulipata takriban vijana 100 wa kike na wa kiume, ambao miaka minne iliyopita, walikuwa hawafanyi lolote, leo wanaendesha biashara zao kwa mafanikio.”

Mkutano wa pili ambao ulifanyika Kigali kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2023, na kuvutia washiriki kutoka kote ulimwenguni kujadili masuala muhimu yanayohusu bara moja kwa moja.
© RCO/Aristide Muhire
Mkutano wa pili ambao ulifanyika Kigali kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2023, na kuvutia washiriki kutoka kote ulimwenguni kujadili masuala muhimu yanayohusu bara moja kwa moja.

Majadiliano ya kushirikiana katika Mkutano wa Africa Soft Power yalilenga maeneo ya mada matatu: uongozi wa wanawake, nguvu ya ubunifu na uchumi wa kisasa, na kusherehekea sauti za Kiafrika na za diaspora ya kisasa.

Mimi ni Eugene Uwimana kwa UN Kiswahili hapa Kigali, Rwanda.