Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante TANBAT6 kwa kuchangia maendeleo yetu: Wananchi CAR

Afisa habari wa kikosi Cha sita kapteni mwijage inyoma akipokea zawadi kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa NOLA baada ya timu ya kikosi Cha TANBAT6 chini ya MINUSCA kupata ushindi wa michezo wa mpira wa miguu kati yake na Gender marine polisi NOLA.
© TANBAT 6
Afisa habari wa kikosi Cha sita kapteni mwijage inyoma akipokea zawadi kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa NOLA baada ya timu ya kikosi Cha TANBAT6 chini ya MINUSCA kupata ushindi wa michezo wa mpira wa miguu kati yake na Gender marine polisi NOLA.

Asante TANBAT6 kwa kuchangia maendeleo yetu: Wananchi CAR

Amani na Usalama

Katika wiki ya kulekea maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani kikosi cha sita cha walinda amani kutoka Tanzania TANBAT 6 kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA kimeanza shughuli mbalimbali za kuelekea kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Mei 29 jumatatu wiki ijayo . Shughuli hizo ni za maendeleo Kwa ajili ya wananchi wa BERIBERATI mkoani Mambele kadei nchini humo CAR.

Soundcloud

Asubuhi mapema katika kikosi hiki cha TANBAT 6 ni wakati wa kuwa na utayari kwa wajeshi na utimamu kwa ajili ya kutembelea sehemu mbalimbali Ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na amani katiki shughuli zao za kilasiku zikiwemo za maendeleo

Mbali ya doria wanajeshji hawa  wanashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na leo hii wanaanza kuitengeneza barabara ambayo imehaiibika  vibaya , na kwa wananchi wa eneo hili huu ni muziki masikioni mwao kama anavyo toa shukurani zake mama huyu Bi. Ester Wandwi mkazi wa Beriberati "shukurani zetu ziwafikie walinda Amani wote Kwa jinsi wanavyojitoa kutusaidia katika maendeleo ya miundombinu kama Leo walivyoonesha upendo wao hawa walinda amani toka Tanzania Kwa kututengenezea barabara iliyokuwa inapitika Kwa shida sana Asante sana Kwa kutujali"

Zana na mitambo ya walinda Amani ikiwa katika shughuli ukarabati wa barabara nchini CAR.
© TANBAT 6
Zana na mitambo ya walinda Amani ikiwa katika shughuli ukarabati wa barabara nchini CAR.

Kazi kubwa ya kikosi hiki ni kuhakikisha usalama , lakini shughuli za maendeleo pia ni moja ya majukumu yao kwani huduma za msingi zinapopatikana wanaamini zinachangia kudumisha Amani na usalama na hili linaishirikisha jamii na viongozi wao.

Hivyo waalinda amani hawa wakaonana pia na chiefu wa eneo hilo Evariste ambaye hakusita kuonyesha furaha yake na kutoa shukran zake za dhati kwa kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na  TANBAT6  ikiwa ni pamoja na ulinzi wa amani na na shughuli zingine za kijamii akisema Kuwa " walinda amani toka Tanzania  walio chini ya MINUSCA wametupatia maendeleo mengi sana ikiwemo kutufundisha kulima mahindi Kwa kutumia jembe la mkono, kutoa misaada ya madaftari, michezo na Leo tumeona kabisa katika maadhimisho ya kuelekea sherehe ya walinda amani wanatutengenezea barabara Asante sana”

Walinda Amani wa Tanzania, TANBAT6 wanaohudumu chini ya MINUSCA wakiwa katika utayari wa patrol nchini CAR.
© TANBAT 6
Walinda Amani wa Tanzania, TANBAT6 wanaohudumu chini ya MINUSCA wakiwa katika utayari wa patrol nchini CAR.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Beriberati Conal Francis Ndenawala mbali ya kutoa shukran kwa kazi kubwa inayofanywa na walinda amani wa TANBAT6 na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humu MINUSCA kwa aujumla  ameahidi kwamba wataendeleza ushirikiano kwani ni daraja la kufanikisha azma ya Umoja wa Mataifa nchini humo na matakwa ya wananchi “Ninawashukuru walinda amani kufanya ziara ya kufika hapa kama ziara ya wiki ya maadhimisho ya siku ya walinda amani duniani ninapenda kusema kuwa walinda amani duniani wanajitoa kuhakikisha mwannchi wa Jamhuri ya Afrika ya kati wanaishi kwa amani lakini pia nimepata taarifa kwa jinsi mlivyo saidia kuleta maendeleo ya kutusaidia kuitengeneza miundo mbini yetu ya barabara kadhaa ambazo zimeharibika, hivyo basi walinda amani chini ya MINUSCA mmesaidia miradi mingi  ikiwemo kusaidia kulima kwa majembe na hata kutoa matibabu kwa wananchi wetu asante  sana.”

Naye kamanda wa operesheni wa TANBAT6 Meja Chacha Matiku amesema kuwa ingwa jukumu lao kubwa ni ulinzi wa raia , kuchagia katika shughuli za maendeleo kumewasogeza walinda Amani karibu na wananchi na kusaidia kwa kiasi kikubwa operesheni zao “Katika kuhakikisha mahusiano mema na jamii…..

Siku ya walinda Amani wa umoja wa Mataifa huadhimishwa kila mwaka Mei 29 lengo likiwa kutanabaisha mchango mkubwa unaofanywa na walinda amani kote duniani katika jamii mbalimbali zinazopitia changamoto na mwaka huu maudhui yakiwa amani, watu na maendeleo.