Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya: UNICEF

Agnes Juma na watoto wake wawili, yeye ni mama wa watoto watano kutoka Kilifi Kenya,  ambaye ni mnufaika wa mradi wa NICHE.
UNICEF Kenya
Agnes Juma na watoto wake wawili, yeye ni mama wa watoto watano kutoka Kilifi Kenya, ambaye ni mnufaika wa mradi wa NICHE.

Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya: UNICEF

Msaada wa Kibinadamu

Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF unafanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya  ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.

Soundcloud

Mradi huu umeleta faraja kubwa kwa familia nyingi za kauti hiyo ikiwemo ya mama huyu.

“Hapa nyumbani tuko mimi na mume wangu na watoto wangu ni watano.”

Kutana na Agnes Juma mama mnufaika wa programu ya NICHE inayoendeshwa na UNICEF katika kaunti hii ya Kilifi. Anasema “Muhudumu wa jamii yetu wa kujitolea wa ulinzi wa watoto ni Janet Bahati , anatutembelea kila mara .”

Kwa Janet kupita nyumba kwa nyumba ni sehemu ya kazi yake kupitia mradi huu “Mimi nahudumia kaya 68 na zinaendelea vyema, na pia nahakikisha naangali endapo kuna kesi yoyote maana wakati mwingine watoto huwa wanadhulumika na kutelekezwa. Katika nyumba hii ya Agnes huwa nakuja mara moja kwa mwezi, na kama kuna suala lolote au dharura huwa ananipigia.”

Mradi wa NICHE unahakikisha baba na mama wote wanashirikishwa ili kuleta tija zaidi kama anavyodhihirisha Daniel Katana mumewe Agnes “Kutakapokuwa na uhusiano mwema baina ya baba na mama kunakuwa na urahisi shida inapojitokeza kujulikana. Kitu kingine ni kwamba hupenda sana hawa madaktari kwa sababu huwa wanatuelimisha kwa mafunzo ambayo wanatupa.”

Lengo la mradi huu wa UNICEF ni kuwafikia watu wengi zaidi na kila wiki kuna mafunzo maalum yanayoandaliwa na kundi la wataalam kwa jamii ili kuwapa mafunzo ya malezi kulingana na kanuni na mwongozo wa kitaifa wa malezi bora.

Mafunzo pia huwapa fursa wazazi kubadilisha uzoefu, kuzungumzia changamoto na kusaka suluhu kwa pamoja.

Everlyne Bosso (Kulia), Afisa Maendeleo ya Jamii katika Kaunti ya Kilifi na Judy Muyuki, Afisa wa watoto kaunti ndogo ya kaloleni nchini Kenya wakiwa katika ziara ya ya kutembelea jamii na kuwajulia hali.
UNICEF Kenya
Everlyne Bosso (Kulia), Afisa Maendeleo ya Jamii katika Kaunti ya Kilifi na Judy Muyuki, Afisa wa watoto kaunti ndogo ya kaloleni nchini Kenya wakiwa katika ziara ya ya kutembelea jamii na kuwajulia hali.

Afisa maendeleo ya jamii wa kaunti ya Kilifi Everlyne Bosso anasema mradi huu ambao uko chini ya mpango wa maendeleo ya kijamii pia unaleta tija kwani  ni wa “Kuwasaidia wazazi kulea watoto vizuri na pia tuna visa vingi vya ukatili katika familia na ndio sababu serikali iliona ni muhim kuufanyia majaribio hapa mKilifi na Garisa.”

Hali katika ameneo kama ya Kaloleni kwenye kaunti hii nilikuwa mbayá sana hasa katika ulinzi wa waatoto kama anavyosema Judy Muyuku afisa wa masuala ya watoto “Tulikuwa na jumka ya kesi 588 ofisini kwetu na asilimia 72 zilikuwa za ukatili dhidi ya watoto. Na asilimia 60 miongoni mwa kesi hizo zilikuwa ni zile za watoto kutelekezwa na wazazi.”

Kupitia mradi wa NICHE mambo yameanza kubadilika na wazazi kuelewa umuhimu wa lishe na malezi bora  kwa watoto wao, na pia kuleta faraja kwa familia zao. Asante kwa wadau na UNICEF inayoshiriki kwa kiasi kikubwa . Mtaalam wa ulinzi wa watoto wa UNICEF Kenya ni Yoko Kobayashi Jukumu la UNICEF limekuwa kutoa msaada wa kiufundi ili kufanikisha programu hii ya kitaifa ya malezi, na kutoa mitazamo inayotokana na ushahidi na miongozo ya kuandaa programu ya malezi yenye ufanisi katika mzunguko mzima wa Maisha ya mtoto kuanzia utotoni hadi anapokuwa barubaru.”

Mbali ya UNICEF na serikali ya Kenya mradi unapigwa jeki pian a wahisani mbalimbali ukiwemi ushirikiano wa kimataifa wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto, USAID, , serikali ya Japan na Benki ya Dunia.