Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jukwaa la vijana laanza rasmi makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Wanafunzi wa shule ya msingi katika jimbo la Sulawesi Kusini, Indonesia wanarejea darasani Machi 2022 kufuatia janga la virusi vya corona.
© UNICEF/Hafiz Al Asad
Wanafunzi wa shule ya msingi katika jimbo la Sulawesi Kusini, Indonesia wanarejea darasani Machi 2022 kufuatia janga la virusi vya corona.

Jukwaa la vijana laanza rasmi makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa Jukwaa la Vijana lililong’oa nanga leo Aprili 25, amesema “Ulimwengu wetu unakuhitaji (nyinyi vijana) zaidi kuliko hapo awali. Kuanzia kwa mabadiliko ya tabianchi hadi migogoro. Kwa umaskini na ukosefu wa usawa. Kwa ukweli kwamba Malengo ya Maendeleo Endelevu yanatoroka bila kufikiwa.  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (katikati kulia) na Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed (katikati kushoto) wakikutana na Viongozi Vijana kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.
UN Photo/Manuel Elías
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (katikati kulia) na Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed (katikati kushoto) wakikutana na Viongozi Vijana kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa ajili ya jukwaa hilo litakalodumu hadi tarehe 27, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesema, "Kukuza suluhu za changamoto hizi  bega kwa bega na vijana  ndio nguvu ya majadiliano ya Jukwaa hili. Ndio sababu iliyoko nyuma ya Ofisi mpya ya Vijana ya Umoja wa Mataifa ambayo itafanya kazi kikamilifu mwaka huu. 

Kwa upande wake Rais wa Baraza Kuu Csaba Kőrösi amesema, "Sioni kitu chochote ambacho kingekuwa cha dharura zaidi kuliko kutengua angalau baadhi ya uharibifu unaosababishwa na binadamu kwa maliasili zetu." 

Kőrösi ameendelea akisema, “Kwa sayari yetu, makazi pekee tuliyo nayo. Kumbuka hili; jielimishe na kuwawajibisha viongozi kwa ahadi zilizotolewa." 

Akifungua Jukwaa hilo, Lachezara Stoeva, Rais wa sabini na nane wa Baraza la Uchumi na Kijamii na Mwakilishi wa Kudumu wa Bulgaria kwenye Umoja wa Mataifa, kwa upande wake amesema, "Jukwaa la Vijana linafanyika wakati wa migogoro, inayojumuisha migogoro ya kiuchumi na kijamii, ukosefu wa usalama duniani, matokeo ya janga la COVID-19, na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa. 

Amesisitiza, "Ulimwengu tunaoishi leo unahisi kuwa hauko salama na sawa." 

Viongozi Vijana wa SDGS Paul Ndhlovu, Mayada Adil, na Gibson Kawago ((Kushoto hadi Kulia)
UN News/ Conor Lennon
Viongozi Vijana wa SDGS Paul Ndhlovu, Mayada Adil, na Gibson Kawago ((Kushoto hadi Kulia)

Jayathma Wickramanayake, Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Vijana, kwa upande wake amesema, "Katika miaka michache iliyopita, Umoja wa Mataifa umechukua hatua muhimu katika mwelekeo huo. Mnamo mwaka wa 2018, Katibu Mkuu alizindua Mkakati wa Vijana wa Umoja wa Mataifa wa kwanza kabisa wa mfumo mzima, Youth2030, unaoleta pamoja Timu 131 za Umoja wa Mataifa na Mashirika zaidi ya 50 ya Umoja wa Mataifa ili kuimarisha kazi ya Umoja wa Mataifa na kwa vijana. 

Mjumbe wa Vijana ameendelea kusema, “Na kama mlivyoona katika miaka minne iliyopita, tumepata maendeleo thabiti katika njia ambazo UN inashirikiana na vijana katika ngazi mbalimbali na idadi ya vijana tuliojihusisha nao katika ngazi mbalimbali. kutoka nchi hadi eneo hadi ngazi ya kimataifa.” 

Akizungumza katika ufunguzi huo, Henry Jevanic, Mshauri wa Vijana wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, amesema, “Ingawa hatuna muda mwingi wa kutimiza malengo ya dunia, tulichonacho ni wingi wa ubunifu na uwezo ambao haujatumiwa na kizazi chetu kipya.” 

Jevanic ameongeza, “Mara nyingi mimi husema kichocheo cha ushirikiano wenye mafanikio kwa Agenda ya 2030 kinahusisha B hizi 3: Hebu TUVUNJE vizuizi vyote vinavyozuia ushiriki wa wote (vijana kutoka makundi ya kiasili, jamii zilizotengwa n.k). TULETE suluhu, mawazo na rasilimali. Wacha tuwe wajasiri katika juhudi zetu na kuwatia moyo wengine kwa vitendo." 

“Hata hivyo hatuwezi kufanya hivyo peke yetu.” Amehitimisha Jevanic.